NDUGU WAGENI WAALIKWA, MABIBI NA MABWANA



Ndugu Wageni Waalikwa, Mabibi na Mabwana,

Napenda kumalizia kwa kusisitizia kuwa kamati ya Uendeshaji na Wajumbe wake juu ya umuhimu wa kuwa makini, waadilifu na wawazi katika kuidhinisha miradi itakayofadhiliwa na Mfuko huu. Mafanikio ya Mfuko huu yatategemea sana ubora wa miradi itakayoidhinishwa na Kamati ya uendeshaji kwa ajili ya kupatiwa ufadhili. Hata hivyo, natambua uzito wa majukumu yanayoikabili Kamati hiyo ya Uendeshaji. Lakini nina imani kubwa na wajumbe wa Kamati hiyo pamoja na usimamizi makini wa Sekretarieti ya Maadili ya Vion gozi wa Umma, kwamba majukumu hayo yatatekelezwa kwa ufanisi. Kwa hiyo, ni matumaini yangu ya dhati kuwa mafanikio yatapatikana katika utekelezaji wa miradi kutokana na ufanisi huo wa kuyashughulikia maombi ya ufadhili wa miradi hiyo. Lakini, sina budi pia kuiasa Kamati ya Uendeshaji kuwa isichukue muda mrefu katika kufikia na kutoa maamuzi yake kuhusu miradi inayoombewa ufadhili. Maamuzi yanayochukuwa muda mrefu kutolewa siyo tu yatawakatisha tama waombaji bali pia yatakwenda kinyume na maadili ya uwajibikaji. Aidha, Kamati ya Uendeshaji inapaswa kufuatilia kwa karibu zaidi utekelezaji wa miradi itakayofadhiliwa, pamoja na kufanya tathmini ya mafanikio ya kila mradi unaotekelezwa. Ni matumani yangu kuwa mfanikio ya miradi itakayofadhiliwa ni Mfuko huu yatakuwa chachu katika juhudi za Serikali na wahusika wengine za kuimarisha Uadilifu, Uwajibikaji na Uwazi katika nchi yetu. Mwisho, napenda kuwashukuru kwa mara nyingine waandaji wa hafla hii kwa heshima waliyonipa ya kuwa Mgeni Rasmi hapa leo. Kwa hakika nina furaha kubwa kupata fursa ya kushiriki katika shughuli hii yenye umuhimu wa pekee kwa nchi yetu. Baada ya kutoa shukrani hizo napenda kutamka kuwa Mfuko wa Uadilifu, Uwajibikaji na Uwazi sasa nimuzindua rasmi.

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Postagem Anterior Próxima Postagem