Vile vile, ninafarijika kufahamu kuwa miradi itakayofikiriwa kuapta ufadhili wa Mfuko huu ni lazima iwe na maelezo ya kitaalamu katika uwasilishaji wake, na ambayo yataonyesha:- 1. Jinsi miradi inavyofuata mipango mingine ya marekebisho Serikalini, yaani Programu za Marekebisho ya utumishi wa Umma, Sekta ya Sheria, na Usimamizi wa Fedha za Umma 2. Jinsi mradi utakavyoirisha ufanisi wa utoaji huduma wa taasisi inayoombewa ufadhili 3. Manufaa ya moja kwa moja ya mradi na manufaa yasiyo ya moja kwa moja, pamoja na kuonyesha kikundi kinacholengwa 4. Mpango wa kazi, na ratiba ya kuonyesha shughuli za mradi zitakazotekelezwa 5. Programu ya ufuatiliaji na kufanya tathmini (Monitoring and Evaluation). 6. Shughuli za mradi zitakavyokuwa endelevu na kudumisha uwezo wa taasisi 7. Mchanganuo wa bajeti ya mradi unaombewa ufadhili na jinsi makadirio ya bajeti hiyo yalivyofikiwa 8. Taarifa mbali mbali za taasisi inayoomba ufadhili, ikiwemo taarifa ya mwaka, taarifa ya fedha iliyokaguliwa, mpango na mkakati wa taasisi na taarifa nyingine.