SEKRETARIETI YA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA MFUKO WA UADILIFU, UWAJIBIKAJI NA UWAZI UTARATIBU WA KUOMBA RUZUKU KUTOKA MFUKO WA UADILIFU, UWAJIBIKAJI NA UWAZI.
Utangulizi: Mfuko huu umezinduliwa tarehe 29 Septemba, 2007 kwa lengo la kutoa Ruzuku kwa Taasisi na Asasi zote nchini zinazojishughulisha na kukuza Uadilifu, Uwajibikaji na Uwazi ili kuzijengea uwezo wa kutekeleza majukumu yao. Miradi inayoweza kupata ruzuku: o Miradi inayoweza kupata ruzuku ni ile iliyobuniwa na taasisi inayoomba Ruzuku. o Mradi uliobuniwa uonyeshe ushahidi kuwa ni kipaumbele cha taasisi hiyo na majukumu yake. o Kuwe na ushahidi kuwa mradi hauna pengo katika gharama, na ruzuku ya Mfuko pamoja na Mchango wa Asasi wa 10% zitagharamia shughuli zote. Mchango wa taasisi yenyewe uonyeshe mchanganuo wa bajeti yake jinsi utakavyotumika ili kukamilisha Utekelezaji wa mradi husika. o Mradi huo usiwe unafadhiliwa na mfadhili mwingine. o Uwe ni mradi unaoshirikisha walengwa na jamii kwa jumla. o Kipindi cha kutekeleza mradi kisizidi miezi 12. o Uwe ni mradi wa kujenga uwezo wa Taasisi. o Mradi uwe na ushahidi kuwa Taasisi iko tayari kuuendeleza hata baada ya Ruzuku kukoma. o Usiwe ni mradi unaorudiwa na Taasisi ila tu kama uko katika hatua ya kukamilika vizuri na umekubaliwa kwa matokeo yake na kutimiza masharti ya Mfuko. Miradi ambayo haitakubaliwa kupewa Ruzuku: o Shughuli ambazo zinahusiana na Polisi, kuendesha mashtaka, Magereza au vyama vya Siasa. o Ununuzi, Ujenzi au upangaji wa nyumba: ununuzi au upangaji wa Ardhi na ununuzi wa magari. o Gharama za utawala na malipo ya mishahara na marupurupu mengine ya watumishi wa Asasi au shirika husika. o Mafunzo nje ya Afrika. o Shughuli za kuchangia fedha, kuomba hisani, zawadi au bakshishi. o Ununuzi wa vifaa ambavyo ni zaidi ya asilimia 15 ya ruzuku iliyoombwa. o Miradi ambayo sehemu kubwa imetayarishwa na washauri wanaofanya kazi kwa niaba ya Asasi na ambao siyo wanachama wa Asasi iliyoomba ruzuku. Utaratibu wa kuwasilisha maombi ya Ruzuku: Asasi iwe na sifa zifuatazo:o Imesajiliwa na msajili wa Asasi za Kiraia na iwe na Hati ya kusajiliwa. o Iwe na Katiba na uwezo wa kujiendesha, wadhamini na angalau wafanyakazi watatu wa kudumu. o Iwe na uwezo wa kuchangia asilimia 10 ya gharama za mradi na uwezo wa kutoa mizania yake ya mapato na taarifa ya Ukaguzi kwa mwaka uliopita. Kamati ya Uendeshaji wa Mfuko inakaribisha maombi Awamu ya pili Uwajibikaji na Uwazi na Utawala Bora ambazo ni:o Taasisi za Serikali o Mashirika yasiyo ya Kiserikali (NGO'S) o Vyama vya Kitaaluma (Professional Associations) o Vyama vya Kiraia (CBO'S) ya Ruzuku
kutoka Asasi na Taasisi mbalimbali zinazojishughulisha na masuala ya Uadilifu,
Fomu za maombi zinapatikana katika Ofisi ya Meneja Mradi, Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Dar es Salaam, na Ofisi za kanda za Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kama ifuatavyo:-
1. Kanda ya Kaskazini, Jengo la Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Arusha, Mtaa wa Makongoro, S.L.P. 3174, Simu 027 2544534, ARUSHA. 2. Kanda ya nyanda za juu kusini, Jengo la Wakala wa Majengo, Mtaa wa Sabasaba Mbeya, S.L.P. 6311, Simu 025 2502714 MBEYA. 3. Kanda ya Kati, Jengo la Mfuko wa Hifadhi ya Jamii,(N.S.SF) Dododma,Mtaa wa Askari, S.L.P. 1887, Sim:026-2321059 DODOMA.
4. Kanda ya Ziwa, Jengo la NSSF S.L.P 1473, MWANZA. 5. Kanda ya Kusini, Jengo la Mkuu wa Mkoa Mtwara, S.L.P 218, Simu: 023 2333962, Fax: 023 2333963, MTWARA. 6. Kanda ya Magharibi, Jengo la Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (N.S.SF) Tabora, Mtaa wa Jamhuri, S.L.P. 1126, Simu: 026 2605323, TABORA.
Muda wa kutuma/kuwasilisha MAOMBI YA RUZUKU ni kuanzia tarehe 1512-2008 hadi tarehe 31 January, 2009. Kwa maelezo zaidi wasiliana na:Meneja Mradi, Mfuko wa Uadilifu,Uwajibikaji na Uwazi, Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya viongozi wa Umma, S.L.P. 13341, Dar es Salaam. Simu: 022 2111810/11 Fax: 022 -2119217 Barua pepe: secretariat@ethics.go.tz
Mwisho wa kupokea maombi kwa Awamu ya pili ni tarehe 31 January, 2009. Ni vyema kuwasilisha fomu yako mapema ili iweze kufanyiwa mapitio kabla ya tarehe ya mwisho ya kupokea maombi ya Ruzuku.