BAADA YA KICHAA KUPEWA RUNGU.
Leo katika pitapita zangu katika mji wa Moshi nilikutana na kisanga kimoja ambacho kilinifanya niwe na hisia za aina yake kuhusiana na hawa waliopewa jukumu la kuangalia ama kusimamia usalama wetu.Kabla ya kushuhudia kisanga hicho, katika pitapita nilifanikiwa kuwaona makuruta(recruits) vijana wanaopata mafunzo ya upolisi katika chuo cha polisi(ccp)tawi la Moshi.Nafikiri vijana hawa wanakaribia kutunukiwa vyeti vyao vya upolisi na wako kwenye mafunzo kwa vitendo.
Nikiwa nimeweka pozi sehemu fulani,mara niliona kundi kubwa la wanausalama hawa watarajiwa takribani ishirini hivi wakiwa wanawakokota vijana wanne huku wakiwa wamefungwa na kuunganishwa pamoja kwa kutumia mashati yao(kimsururu,yani kwa kufuatana),huku mkong'oto wa hapa na pale ukiendelea,
Nilijiuliza,hata kama mtu kakosea ndio achukuliwe kinamna ile kweli,? Kwani pale waliuondoa utu wa mtu kabisa kabisa!!
Nikajiuliza tena,au ni namna ya kupunguza hasira za mazoezi makali wayapatayo chuoni? Kama vijana walikuwa wanaleta ukorofi,mimi naamini katika mafunzo ya huko chuoni ,kuna mbinu ambazo hufundishwa ktk kukabiliana na hali kama hizo na si kupiga na kumdhalilisha mtu.
Naomba msinielewe vibaya,hapa siwatetei wahalifu ,bali najaribu kuongelea namna ambavyo binadamu wanavyowatreat binadamu wengine bila kujali utu.
Au pengine hali hii ni kwa sababu hata wahalifu wenyewe pia huwa hawajali utu? Je hiki chaweza kuwa kigezo cha wanausalama hawa kuwatreat vibaya wahalifu?
Hali hizi za kuwatreat watu vibaya si tu katika nyanja hii ya usalama bali hata ktk nyanja nyingine kama za uongozi .nk.
Ufisadi,rushwa na mambo mengine ya hujuma ni baadhi ya mambo ambayo huashiria kupotea kwa haki za watu.Kwa vile mtu ni kiongozi basi anatumia kila mbinu katika kujinufaisha yeye mwenyewe.Hii imetawala sana kwa viongozi wengi duniani.Wanawekwa na wananchi madarakani lkn huwa wanajali maslahi yao zaidi na hata ikiwezekana kuwakandamiza wananchi kwa manufaa yao huku wananchi wakibaki na ahadi.