KIKAO CHA DHARURA TANZANIA


Kikao cha dharura
"Mawasiliano", kitaalam wanaita "communication"

"utunzaji wa mazingira" kitaalam wanaita "environmental conservation"

"kiziwi" kwa lugha ya kitaalam wanaita "deaf"

"Kichocho" kwa lugha ya kitaalam wanaita "Bilhazia"

"kukohoa" au kwa lugha ya kitaalam "coughing".
"mmen'genyo wa chakula" au kitaalam "food digestion"

Mifano ni mingi, na watu wengi huwa wanafanya hivi mara kwa mara. Najiuliza ni kwa nini lugha ya kitaalam iwe ni Kiingereza. Binafsi sipati mantiki ya tafsiri hii ya kubadilisha maneno kiswahili, pengine yaliyojitosheleza na kuyapeleka kwenye lugha nyingine( kiingezera) na kisha kulitunuku neno hilo kuwa ni la kitaalam. Likiwa katika lugha ya kiswahili , haliitwi la kitaalam.

Sijui niite ni dharau za wazi kwa lugha yetu adhimu ya Kiswahili, au ni ishara ya wazi ya upungufu wa uzalendo tulio nao?
Binafsi bado sijapata maana halisi ya kwa nini maneno ya kiswahili pindi yageuzwapo pamoja na kuwa na maana ile ile huitwa ya kitaalam. Kwa nini "mawasiliano" lisiwe neno la kitaalam? Au kiziwi? Au kukohoa? Au " mmen'genyo wa chakula?

Lugha ya Taifa yenye kupewa msisitizo mdogo nayo ni changamoto.

Hoja hiyo hapo ndugu wajumbe, kikao kinaendelea.

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Postagem Anterior Próxima Postagem