UKOSEFU WA UZALENDO, SUMU YA MAFANIKIO TANZANIA


Ukosefu wa UZALENDO, sumu ya Mafanikio Tanzania.
Tanzania ni nchi ambayo imebarikiwa kwa kuwa na rasilimali za kutosha kabisa ambazo zikitumika vizuri zinaweza kubadilisha hali mbaya ya uchumi na umasikini tulionao watanzania tulio wengi.

Hali ya "umimi" kwa viongozi wengi wa serikali inakithiri kila kukicha, hili lajidhihirisha kwa namna watu wanavyotumia kila mbinu kupata uongozi kuliko kutafakari hali halisi ya watanzania.Watu wanazitafuta nafasi za uongozi kwa manufaa yao binafsi na kulisahau taifa. Tujiulize viongozi wastaafu mathalani maraisi,wana mchango gani baada wao kuachia ngazi? Wengine wanasahaulika kabisa kama walishakuwa maraisi!Hivi baada ya Nyerere kung'atuka alipotelea mitini kabisa? Umimi, ukosefu wa "uzalendo" kwa viongozi wetu ni tatizo kubwa na ni sumu ya maendeleo.

Wananchi nasi twahitaji kuwa wazalendo pia.Yashangaza sana,tena sana kwa baadhi ya wananchi kushabikia chama kuliko uwezo wa mgombea ktk uongozi. Utamsikia mtu anasema mimi ni CCM damdam kwani kila mwaka inashinda tu,hawashindwi hawa,hata kama ni kwa kuiba kura ilimradi wanashinda! Yasikitisha ushabiki wa mchezo wa mpira wa miguu ndio watumika hata kwenye siasa,yani ni sawa na mtu aseme kuwa ametokea tu kuipenda Simba sport club kwa sababu mpaka sasa ktk msimu huu wa ligi inashinda tu. Utaratibu huu kwenye michezo ni sawa kabisa lakini si kwenye siasa.Utaratibu huu wa ushabiki wa michezo unapoingizwa kwenye siasa, ni hatari na ndio unachangia sana kuchagua viongozi wasio na uzalendo na walio na umimi uliokithiri na ambapo ni matokeo ya wananchi wasio na uzalendo.


Misingi ya uzalendo miongoni mwetu sisi kama wananchi na miongoni mwa viongozi wetu ni muhimu sana kwa maendeleo chanya ya Taifa letu.

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Postagem Anterior Próxima Postagem