Asili ya Kua
Walikuwa Waarabu wawili walipofika kwa wenye mji wa Kua. Waliokuwa wenyeji ilikuwa ni Washirazi ambao walifika zamani kutoka Ajemi. [Waarabu] wakataka pahali [pa] kujenga wakapewa wakajenga. Waarabu walipewa kaskazini ya mji huo na kwamba ulioikuwa Mkokotoni – Washirazi waliwambia Waarabu ‘tulingane pamoja’ (yaani [ninyi] mjenge huko na sisi tuko huko tuwe jirani pamoja). Waarabu walijibu wakasema ‘hatujui kama itakua’.
Baasi Waarabu walianza kujenga upande wa kaskazini ya mji wa Mkokotoni. Baada ya kwisha mji wao, waliwaita wenyeji wao (yaani Washirazi) na wakambia ya kama ‘mji wetu sasa jina lake Kua’. Wenyeji Washirazi walikubali nao pia wakataka mji wauite Urangayu (yaani ‘muungano’). Asili yake maneno haya ilikuwa ni desturi ya watu wa zamani kutumia maneno ya fumbo.
Baasi ingawa walisema Kua ile kwa ujenzi – bali wakinuia baada ya kukaa watawala na wawatumie wenyeji wao. Hivyo Washirazi hawakulifahamu siri yake neno hilo. Wao [Washirazi] waliwakaribisha kwa wema na wakaa wote kama watu wa moja kwa kueleana hata kwa muda ilikuwa. Waarabu wamekuwa wenye sehemu kubwa na nguvu, na wakataka ndio waliotawala sehemu yote. Baada ya muda mchache Waarabu walipokwisha kuwa mahwana, walianza kuwa wabaya, na kwanza walimkata mkono mkubwa wa mfundi ili asiendelee mahali pengine. Fundi aliona ungonye yunjefikilia na machungu mengi kwa ajili ya kazi hiyo. Waarabu walijenga tena chumba kidogo cha uhalifu chini ya Jumba la Mfalme na wakatia misumari. Hapo wenyeji waliona taabu sana. Mfalme wa Kisimani [Mafia] akapata habari ya kama Washirazi wamo katika taabu.
Mfalme wa Kisimani akaunda jahazi. Ilipokwisha alipeleka habari kwa Mfalme wa Kua na akamtaka ampelekee vijana ili waje wakamshulie jahazi lake. Mfalme wa Kua aliwataka raia zake wote akawaambia ya kuwa kila lake. Mfalme wa Kua aliwataka raia zake wote akawaambia ya kuwa kila mtu atoe mtoto wake mmoja ili wanaenda wakamsaidia Mfalme wa Kisimani Mafia anashua jahazi yake [Alisema] na si kwa kuwa site tu ndugu moja tufanya shime (heshima?) mtumpe msaada huo. Watu waliokwenda walikuwa kidogo sana. Ilikuwa kiasi cha watu sita au saba tu, sababu kilikuwa muda mtihani fulani fulani. Mfalme wa Kisimani aliwauliza mmoja katika watoto wa watu wa Kiarabu na alipofahamu alikamata akamlaza na biroti na akamlaza chini ili iwe ni sadaka kwa kushulia jahazi hiyo. Waliobaki walirudi nao walipewa barua iliyosema kuwa ahsante kwa msaada wako. Na katika jumla ya watoto waliokuwa kunisaidia nimechukua mmoja nimefanya sadaka ya jahazi yangu.
Katika upande wa Kua [watu] walikatazwa wasiende kupigana wala kufanya maneno yoyote juu ya matokeo hayo. Baadaye, [watu wa] Kua walifanya shauri wakijenga nyumba moja ya chini. Walipokwisha tengeneza nyumba yao nayo, ilikuwa ni muda mrefu sana tangu kutokea tendo lile la kushua jahazi. Mfalme wa Kua alifanya arusi bali karamu kubwa kilifanya na watu wengu walialikwa. Aliwaita watu wa Kisimani kuja katika arusi, nao walikuja vijana. Siku waliofika vijana, walikaribishwa nyumba hiyo ya chini ilivyojengwa na kustareheshwa pamoja na vijana wa Kua wote wa jumla. Mazumgumzo wa raha zote jumla ilikuwa sika saba hata wakawa wamezoea, hata wakawa wanakwenda peke yao kula na kutembea. Siku ya nane, ambayo ndio siku ya ilikuwa mwisho, walikwenda kuzumgumza ndani ya nyumba ile pamoja [na] kizee mmoja alikuwa mkongwe sana naye alikuwa anawauliza wale vijana wa Kua ‘Je, namna gani mbona mnatoa na mnaua wenzenu?’ Lakini wakati huo, milango ya nyumba hiyo ilikuwa imefungwa na hakuwa na pa kupita tena, mara watu wakajatia chokaa uma wa mlango ile ikiwa na ndio kaburi yao tena.
Fundi aliyokuwa amekatwa kono alikimbia akaenda katika nchi ya Madagascar katika mji wa Wibu, akawakuta watu wa taifa la Wasakalava akawambia ‘Iko nchi ya watu lakini wanawake yani hawana zana za kupigana, twendeni makwateke’. Walikubalia nao wakafunga safari kwa mitumbi yao. Ilikuwa kiasi cha paka 100, au 200, na kila moja ilikuwa na kiasi cha watu 2 au 3 .Walipofika Kua hawakupiga, walishuka, wala hawakupigwa wao – ila mmoja tu mzee aliyekuwa na ng’ombe zake na wale Wasakalava waliopoona ng’ombe walitaka wachukue. Yule mzee alipiga mtu mmoja jiwe la kibewe. Haya palepale wakimuwa. Basi hapo watu walipopata habari za watu hao walikimbia wote na watu wengi walikamatwa na Wasakalava, wakachuliwa mateke.
Baada ya kua amani kidogo, mtu mmoja, jina lake Muhamed Raasi, aliyekuwa ndie mume wa Malkia Mwanzuani, alikwenda kuomba msaada sehemu za kwao katika ufalme wa Siu (Lamu). Huko walitolewa watu kuja kupingana Kua. Na walikuwa na Waarabu na Wagunya karo (kama?) Waarabu walikuwa Wahabarani. Watu hao walipotolewa kula Lamu walisema ‘Kwanza tupitia Unguja nao’. Walipofika Unguja hawakuja kabisa huku, walibaki palepale kila mtu. Mkubwa mmoja alijenga mahali pake wakakaa huko huko. Ushahidi wa kwamba mji ule unaitwa Mkokotoni Unguja ni dalili ya kuwa mmoja aliyekuwa amefutana na Muhammed Raasi na akabaki Unguja akapenda kuita sehemu ila jina la maji wao wa Mkokotoni ambao leo ndio kusini ya Kua.
Pia kuna kijiji cha Uzini huko Unguja na Manda hivi pia na majina ya miji iliyokuwa huko katika kisiwa cha Chole na inaonyesha ni wale waliokwenda kutaka himaya na ambao hawakurudi tena Chole bali waliobaki Unguja na kuona kuwa panawatosha wakaanzisha vijiji kwa majina hayo walioyajua.
Kisimani haikupigwa bali ilivunjika tu kwa ajili ya maji yaliojaa. Ilikuwa Kisimani na mji mkubwa na ufalme wake mpaka Bwejuu. Lakini kwa maji hayo hakua anayejua ilikuwa nini.
Baada ya kuona kuwa hakuna msaada uliotoka katika nchi ya Siu au Lamu, mfalme Mwanzuani alihamisha na jamaa wake, wakaja katika kisiwa cha Chole. Naye alikaa kwa muda mrefu na alijengewa majumba na mawe pia. Lakini yalivunjika alipokufa. Na wakati huo kuna mingiliano ya Wareno na Waarabu wengineo. Asili ya Chole ilikuwa na kisiwa cha wavuvi na wakivua samaki wa changu nao walikulikana kwa uzuri wao na kuita Changu wa Chole. Hili ni jina lao wa wavuvi wote katika pwani za Afrika ya Mashariki kwa kuwa hapatikana kwa wingi huku tangu zamani sana na watu wakipelekea zawadi katika sehemu nyingi kila kabila. Na kabla ya kuhamia watu wa Chole sehemu yote ilikuwa ni kama mashamba ya watu wa Kua na hufa (?) wakapata mavuno tu, hata wapotake kuhama au ukimbiza Mfalme wao ndipo walipoona bora kwenda na kukaa huko.
(document obtained by Pat Caplan in Kilindoni 1966. A version of this story appears in the booklet by Chris Walley: ‘Historia ya Chole kama inavyosimuliwa na wenyeji wake’, 1997)