MFUMO MPYA
6.1 CUF AU ZUF ?
CUF, chama cha wananchi, sehemu ya Zanzibar, ndicho chama kinachotaraji kushinda kwa kiwango kikubwa Zanzibar katika uchaguzi ujao wa vyama vingi Tanzania. Ingawaje, CUF si jina halisi la Kizanzibari linalopendeza sana baina ya Wazanzibari wote. Kukubali kwa CUF na vyama vyengine vya upinzani Zanzibar, kujiunganisha na vyama vya Tanganyika bila ya kuwa na maslahi ya aina moja na misingi ya kisiasa ipatanayo na inayoambatana, kumefanya uamuzi huo uonekane kama kuuza heshima ya Uzanzibari. Kama vyama vya upinzani vya Zanzibar pamoja na wale wanaojiita CCM Zanzibar wangelishikilia uzi ule ule wa kudai Zanzibar ni nchi huru, taifa huru na dola huru linalostahiki kuheshimiwa kama taifa, basi bila ya shaka yoyote wangelishinda kuirejeshea Zanzibar heshima yake . CCM na Nyerere wasingelithubutu kuilazimisha serikali ya Zanzibar kujitoa katika Jumuiya ya Waislaam na wanasiasa wa Tanganyika wasingeli thubutu kupita na kutumia lugha ya matusi dhidi ya Wazanzibari na viongozi wake. Sababu muhimu mojawapo ya kufanya Zanzibar kuzidi kutothaminiwa, ni kwa sababu Viongozi wa Serikali na Viongozi wa Upinzani wa Zanzibar walishindwa kusimama madhubuti na kidete kusisitiza kwamba walidai vyama vya Kizanzibari, na kama madai yao yasingekubaliwa, basi wangelidai kwamba vyama vyote vingelikataa kujiandikisha katika uchaguji huo. Wakosa zaidi, katika suala hili ni CUF, kwani ilikuwa CUF ndiyo iliyotarajiwa kuilazimisha Serikali ya Zanzibar kuchukuwa khatuwa kama hiyo. Ingawa CUF na Serikali ya Zanzibar zina siasa na malengo tofauti, sehemu zote mbili, bila ya kificho zinataka uhuru zaidi kutoka Tanganyika. Pindi makundi haya mawili, pamoja na makundi mengine ya upinzani ya Zanzibar yangelishikilia madai hayo na kutojiandikisha, basi serikali ya CCM ingelilazimika kuyakubali madai hayo, au kujitayarisha na kulaaniwa ulimwenguni kote. Kama serikali ya CCM ingeliendelea na kushikilia na njozi za vyama ati vya "kitaifa" basi ingelikosa misaada ya kiuchumi kutoka kwa wafadhila wao, misaada ambayo Tanzania Bara isingeliweza kuikosa, wakati Zanzibar kwa miaka na miaka ilikuwa haiitaraji misaada hiyo iliyokuwa ikiishiya na kumalizikia Tanganyika. CUF, ikiwa Zanzibar na wafuasi wasiyopunguwa asili mia themanini, iliwajibika nakusisitiza ibaki ZUF, na hata kama wasingelisajiliwa katika uchaguzi basi nguvuzao hatimae zingezidi kuwa kubwa na kuifyeka CCM moja kwa moja. Chini ya mwavuli wa ZUF, fikra tofauti za Kizanzibari zilikuwa zikiwakilishwa, kutetewa, kujadiliwa na kupelekwa mbele. Wazanzibari wengi hata wale wa CCM waliitambuwana kuiheshimu ZUF kwa sababu walijuwa kwamba, ZUF ikiwakilisha na kutetea Uzanzibari na utaifa wake, wakati huo huo ZUF ikitambulika kama ni mchanganyikowa fikra za kimapambano karibu za Wazanzibari wote, wakiwemo na wale wanaojiita CCM. Wengi wa Wazanzibari hao wanaojiita CCM, wanafanya hivyo kwa vile hawanabudi na pindi wangeli kuwa na satwa ya kuchukuwa khatwa zao wenyewe bila yakuomba ruhusa Dodoma, basi angalau wangelijiita CMZ, yaa- ni Chama Cha Mapinduzi cha Zanzibar, baadala ya CCM. ZUF kukubali kujiita CUF ilikuwa nimakosa, kwani sasa CUF inatambulika kama chama cha siasa cha Tanzania wakati,ZUF haikutambulika kama ni chama kimoja tu bali vyama tofauti vya Kizanzibari vilivyokuwa vikipigania maslahi ya Zanzibar. Pindi ZUF ingeliendelea kuwa kamaZUF, basi bado ungelikuweko uwezekano wa vyama vyote na fikra zote za Kizanzibari kuwa chini ya mwavuli mmoja. Hali hii ingeliiwezesha Zanzibar hatakuweza kuwa na serikali moja ya Taifa ikiwakilisha vyama, fikra na misingi tofautikwa maslahi ya Zanzibar yote kwa jumla na kuepusha mgogoro wa leo wa kupiganiana kung'ang'ania Kiti cha Urais, kwani katika serikali hiyo wangelikuwemo Afro-shirazi na CCM Zanzibar vile vile. Viongozi wa ZUF walidhani kwamba njia pekee na ya urahisi ya kuipatia Zanzibar utaifa wake ni kukamata khatamu za serikali na kutarajia kwamba mambo yatakaa sawa wenyewe baadae. Kwa bahati mbaya, hali hii haionekani kuwa inamkinika. ZUF ilikuwa sio chama kimoja tu cha kisiasa, bali ni muungano wa mikondo ya fikra mbali mbali; fikra ambazo zilitiliwa mkazo na dai la "Kura ya maoni" . Leo kura ya maoni hatuisikii tena. Mbele kuna khatari fulani inakuja na hatuna tena ZUF yakutulinda na khatari hiyo; na kama hatujatahadhari mapema, itapita miaka thelathini mengine bila ya kupata uhuru wetu. Lengo la baadhi ya Viongozi wa CUF leo ni kukamata khatamu za serikali, na- kwamba wao pekee ndio wenye haki ya kuiongoza Zanzibar. Baadhi ya viongozi hao wanasahau vipi wao wameweza kupata nafasi ya kuwa viongozi, wamesahau kwamba roho mbichi za watu zime toka, wamesahau kwamba watu wameteseka na kuteswa kadri kiasi hata leo tukafika tulipo fika. Kuna baadhi ya viongozi wa CUF wanahitaji wajisomeshe kisiasa kabla hawajaanza kutaka kuwafundisha wengine siasa, hasa wanachohitaji ni kukariri historia ya kisiasa ya Zanzibar ya tokea 1964.Kati ya Viongozi hao wachache katika uongozi wa CUF wasiote kwamba, CUF ikishashika serikali, wao watakuwa mabwana au kwamba CUF pekee au viongozi wa CUF pekee ndio watakaokuwa na haki ya uamuzi wa mwisho wa mambo ya visiwa vyetu. CUF lazima iwaelimishe baadhi ya viongozi wake tokea hivi sasa kwamba,Wazanzibari hawataki siasa ya chama kimoja kwa sababu wanapinga CCM tu. Hata sivyo hivyo, kile wanachokipinga Wazanzibari ni mfumo wa ki- dikteta na wa chama kimoja, na kupinga huko ni kwa kimsingi, yaani hata itapokuwa CUF ina khatamuza serikali Zanzibar, patatakiwa lazima pawepo vyama vya upinzani na kidemokrasia- kwa jumla. Wadhifa wa kuijenga Zanzibar mpya umo katika viganja vya mikono vya Wazanzibari wote kwa jumla. Uongozi wa nchi vile vile ni wadhifawa Wazanzibari wote wenye uwezo na waliyokuwa tayari kuitumikia nchi kwamaslahi ya nchi na sio maslahi ya ubinafsi. CUF inawajib wa kuhakikisha kwamba wale viongozi wenye sifa za kudhani ni wao tu wenye haki ya kuongoza Zanzibar,wanachujwa tokea leo na wasipewe nafasi za hatimae kuleta tena rushwa, ulanguzi,wizi, unyanganyi ubinafsi na udikteta. CUF inatarajiwa isome kutoka na makosa ya Hizbu ya kusahau kwamba ASP na- Umma Party vilikuwa ni vyama vya upinzani ambavyo ililazim vitambuliwe navihishimiwe. Vile vile iepuke makosa ya Hizbu ya kukana kujitayarisha ku- unda serikali ya Kitaifa na kutokubali kujiandaa kwa siku za mbele pindi chama hicho kingelishindwa katika uchaguzi na hatimae kuwa chama cha upinzani. CUF vile vile inawajibika kuepuka makosa ya ASP ya kuufyeka upinzani wa ndani na wa nje ya chama, na kuwauwa wanasiasa wapinzani, wakisahau kwamba na wao wakati fulani walikuwa wapinzani. CUF lazima iepuke makosa ya UMMA PARTI yakulinyamazia Baraza la Mapinduzi na kutochukuwa hatuwa mpaka maji yalipomwagika na kujikusanya wao wenyewe tu. CUF lazima ilaani uuwaji wa Wazanzibari wote na sio Wazanzibari fulani tu. CUF inatakiwa iepuke siasa ya Baraza la Mapinduzi la kuwafukuza wazalia wa nchi kwa sababu wa likuwa na fikra tofauti za kisiasa, kuwageuza Wazanzibari hao wakimbizi ilhali nchi yao ikiwahitaji,na wakati huo huo kuwafukuza kazi na kuwanyanganya mali zao. Hivi ni vitendo vilivyo dhidi ya haki za kibinaadam na ambavyo lazima vipigwe vita, kwani kila mwananchi ana haki ya kuwa na fikra huru na kufuata mkondo atakao. CUF ikipata khatamu za serikali inafaa ipendekeze uanzishaji wa kuruhusu Uraiya wa nchi mbili kwa wale Wazanzibari waliyolazimika kuchukuwa uraiya wa nchi nyengine. Vile vile CUF inalazimika iepuke siasa ya CCM ya kukaa Dodoma na kuugubika Umma wa Kizanzibari na Wakitanganyika utawala wao bila ya kuwashauri au kuwashirikisha katika kutawala nchi zao na kuwanyima kila haki ya kushiriki katika ujenzi wa nchi zao. CUF lazima tokea mapema iwaelimishe wazi wale viongozi dhaifu kwamba madai ya demokrasia na ya kuheshimu haki za kibinaadam hayatasita baada ya serikali yachama kimoja cha CUF kupatikana, bali kwamba CUF itahakikisha kutekelezwa kwamfumo wa vyama vingi, kutekelezwa kwa malengo ya demokrasia na kuheshimiwakwa haki za kibinaadam, na sio kwamba CUF ikipata serikali basi haya mambo yatasahaulika. Ikiwa CUF itashindwa kuyatekeleza malengo hayo basi kuna haja muhimu na ya haraka ya kuifufuwa na kuiimarisha ZUF.
Vyama vya Upinzani vya Tanganyika
Vile vyama vya upinzani vya huko Tanganyika vinatakiwa vipewe haki za kidemokrasia za kikamilifu bila ya kuwekewa vikwazo vyovyote, vya siri au vya kidhahiri. Kwa vile misingi ya kisiasa, ya kitamaduni, ya kiuchumi na ya kijamii ya Tanganyika na ya Zanzibar inatafautiana, lazima mazingara ya vyama vya nchi mbili hizo vitafautiane. Ni kinyume na muelekeo wowote wa kisiasa kuwatarajia Watanganyika waweze kuanzisha chama cha kisiasa Zanzibar, kuweza kujuwa shida za Wazanzibari na kuweza kuzitetea shida hizo vilivyo. Kwa minttaraf ya mantiki za kisiasa ya kinadharia na ya kitendaji, ni kinyume kabisa na uzoefu wa kisiasa wa kidemokrasia ambayo ina msingi wa kihalali, kulazimisha vyama vyenye misingi yao huko Tanganyika kutafuta wafuasi Zanzibar katika dakika za mwisho za kampeni ya uchaguzi. Ikiwa CCM (pamoja na vyama mama vilivyoizaa) kwa muda wa miaka thelathini imeshindwa kupata zaidi ya asilimia kumi na tano ya wapigaji kura wa Zanzibar wa leo, na asilimia kumi ya wa Bara, vipi itatarajia chama kipya cha Tanganyika kuwa na uwezo huo kwa muda mfupi sana. Vyama vya Tanganyika vinatakiwa vidai kwamba, kama CCM itashikilia msimamo huo, basi Zanzibar iwe na majimbo na wagombaniaji uchaguzi sawa na wale wa Tanganyika, yaani kama Tanganyika kuna watetezi 100 na Zanzibar kuwe na watetezi 100, katika Bunge lawajumbe 200 na chama chochote ambacho kitashinda kwa asili mia kubwa zaidi katika nchi moja wapo ama pekee au kikiungana na vyama nyengine, kiwe na hakiya kuendesha serikali ya Tanzania nzima, yaani kama CUF itapata asili mia 80 au zaidi Zanzibar na CCM asili mia 60 Tanganyika, basi CUF ndio itakiwe kuendesha serikali ya Tanzania nzima. Kwa vile CUF inatarajiwa kushinda Zanzibar zaidi ya asilimia themanini, kwa urahisi inaweza kuongoza serikali hasa ikiunganisha viti vyake na vile vyama vingine vya Tanganyika. Kwa njia kama hiyo Bunge na serikali itayofuatia inaweza kubadilisha sheria na kuweza kuanzisha usajili mpya wa vyama wa kihalali na uondoshaji wa sheria na kanuni potofu za hivi sasa ambazo zimebuniwa na Nyerere peke yake. Vyama vya kitaifa vya Kitanganyika na vya kitaifa la Kizanzibari vinatakiwa kuwa na uwezo wa kujiamualiya wenyewe na kuwa na uhuru wa kusimamisha watetezi wauchaguzi sehemu zile wazitakazo. Kama vyama vya Tanganyika vitaamua kusimamisha watetezi wa uchaguzi sehemu ya Tanganyika pekee waweze kufanya hivyo, na kama watapendelea kusimamisha mjumbe au wajumbe Zanzibar, iwe wenyewe ndio watakao amuwa na sio kulazimishwa. Vyama vya Zanzibar navyo viwe na haki kama hiyo. Katika nchi za kidemokrasia vyama vya kisiasa vina haki yakusimamisha au kutosimamisha watetezi katika jimbo lolote bila ya kulazimishwa na mtu yeyote. Watanganyika kama walivyo Wazanzibari wana haki kamili za kujiamulimambo yao wenyewe.
Matarajio ya Mzanzibari
Matarajio ya Mzanzibari ni kupata ulinzi kamili wa uhuru wake kamili, kupata kuheshimiwa kwa haki za kibinaadam kama zilivyodaiwa katika Tangazo la Haki za Kibinaadam la Umoja wa Mataifa la 1949, ambalo linatetea: uhuru, heshima na haki sawa kupinga ubaguzi wa kikabila, rangi, uume au uke, lugha, dini, wa fikra tofauti, asili, kitaifa, kijamii, mali, wa jinsi ya mtu au msimamo mwengine wa kijamii. linatetea haki ya maisha, uhuru na usalama wa nafsi ya mtu kupinga utumwa wa aina yoyote kupinga kuadhibiwa au kufanyiwa mtu ukatili inatetea kutambuliwa mtu kisheria ulimwenguni kote watu wote kuwa sawa mbele ya sheria kutetewa kwa mtu na sheria kwa mujib wa katiba/sheria mtu asikamatwe bure, kuwekwa kizuizini au kufukuzwa kazi au nchi kila mtu ana haki kwa kupitia mahkama huru kushughulikiwa kihalali na hadharani kuhusu shtaka lolote dhidi yake - mshtakiwa hana makosa mpaka kosa lake lithibitishwe na mahkama halali na ya hadhara akiwa amepewa haki za utetezi kamili mtu hana kosa kisheria ikiwa kitendo hicho alikifanya kabla ya sheria hiyo kutungwa mtu alindiwe haki zake za kibinafsi pamoja na maandishi ya barua zake , heshma, staha na haki zake zilindwe kisheria mtu ni huru kwenda na kuishi atakako mtu ana haki ya kuhama na kurejea nchi yoyote mtu ana haki ya kuomba ukumbizi haki hiyo asiweze kunyang'anywa kwa makosa ambayo si ya kisiasa watu wote wana haki ya kuwa na uraiya mtu asinyang'anywe uraiya kwa maonevu au kukataliwa haki ya kubadilisha uraiya watu wenye umri wa kujitegemea wana haki za ndoa na ya kuanzisha ukoo na kuwa na haki ya kuingia harusi jamii inawajibika kulinda ukoo kila mtu ana haki ya kumiliki rasilmali mtu asinyang'anywe mali bila ya sababu mtu ana haki ya kuwa na fikra huru, muamko, dini au imani huru kila mtu ana haki ya kuwa na uhuru wa fikra na wa kujieleza, kuwa na uhuru wa haki hizo bila ya kuingiliwa kati, kadhalika kuwa na haki ya kutafuta, kupokea na kutoa habari/fikra kupitia chombo chochote cha habari bila ya kujali mipaka ya nchi kila mtu kwa usalama ana haki huru ya kufanya mikutano na kuunda chama mtu yeyote asilazimishwe kujiunga na chama fulani mtu ana haki ya kuweza kushiriki katika Serikali ya nchi yake au kwa kupitia njia ya mtetezi wake aliyechaguliwa katika uchaguzi halali kila mtu ana haki sawa katika huduma za kiserikali za nchi yake Matakwa ya umma ndio yawe msingi wa uongozi wa serikali, kwa kupitia uchaguzi wa halali wa majira, wenye kanuni za kidesturi, pakiwa na haki sawa za kupiga kura; uchaguzi wenyewe uwe wa siri na huru. kila mtu ana haki ya kiuchumi, kijamii na kitamaduni kila mtu ana haki ya kufanya kazi, kuchagua kazi, kuwa na haki halali za kufanya kazi na kulindwa na ukosefu wa kazi kila mtu ana haki ya kupata mshahara sawa kwa kazi sawa mfanya kazi ana haki ya kupata mshahara halali na wakutosha, kuhakiki sha maisha yake na ya ukoo wake, kwa mujib wa thamani na heshima ya kibinaadam, kupandishiwa mshahara inapomkinika kila mtu ana haki ya kuunda na kujiunga na umoja wa wafanya kazi kuhifadhi maslahi ya kazi yake kila mtu ana haki ya mapumziko, kujistarehesha, kuwa na kiwango maalum cha saa za kazi na kupata malipo katika likizo kila mtu ana haki za lazima kama vile chakula, mavazi, nyumba, matibabu na huduma nyengine za jamii, kama vile akiwa mgonjwa, kizuka, mzee au kutoweza kujitazama nafsi yake Mzazi na mtoto mchanga wachungwe na watizamwe kila mtu ana haki ya elimu huru tofauti elimu irekibishwe kuendeleza utu kila mtu ana haki huru ya kushiriki katika utamaduni wa jamii, kunufaika na sanaa na sayansi kila mtu ana haki ya himaya kutokana na maandishi yake yote yakiwemo ya kisayansi au kisanifu kila mtu ana haki ya kufaidika na Tangazo hili kila mtu anawajibika kwa jamii ambayo hatimae itamhakikishiya utu wake kila mtu ana wajib wa kutekeleza sheria halali yenye msingi wa kidemokrasia uhuru na haki hizi uepukwe kutumiwa dhidi ya maazimio na msingi wa Umoja wa Mataifa ni kharamu kwa nchi, kikundi au mtu yoyote kutumilia kifungu chochote katika Tangazo hili kuvunja haki au uhuru kama ilivyotajwa Katika mkutano wa haki za Kibinaadam wa Umoja wa Mataifa huko Viena, Austria,katika mwaka 1993 mambo yafuatayo yalisititizwa: Usawa, heshima na kustahamiliana kulaani ukabila, ubaguzi wa kikabila, chuki ya wageni na tabia nyengine ya kutostahamiliana Kuheshimu haki za watu wa mataifa madogo, wenyeji asilia (indegenous - people) makabila madogo madogo, dini au lugha tofauti kulinda haki za wafanya kazi wa kigeni haki za sawa sawa na haki sawa za kibinaadam kwa wanawake kuhifadhiwa kwa haki za watoto (kutumiliwa kisiasa na kuharibiwa mais- ha yao kwa sababu ya matumizi ya madawa (unga) ya kulevya) kuepusha mateso ya utesaji na kuwashitaki wale wanaoshiriki katika uo- vu huo kukomesha sheria ya kuweka watu vizuizini kukomesha kupotezwa/kutoweshwa kwa watu (wanasiasa/wapinzani) Upungufu wa utekelezaji misingi hiyo uchunguzwe na kujulishwa Center ya Haki za Binaadam, New York, Umoja wa Mataifa. Ulinzi wa haki za kibinaadam ni jambo la lazima na inatarajiwa wakati CUF itapopata khatamu za utawala itaanzisha usomeshaji wa haki za kibinaadam hizi maskulini na sehemu zote zinazotowa huduma ya jamii pamoja na katika Redio na Televisheni.
Demokrasia
Kukubaliwa kwa uanzishaji wa vyama vingi nchini ni moja tu katika misingi yakutekeleza demokrasia. Kwa mujib wa hali ilivyo Tanzania, hasa Zanzibar , hata suala hili hali-jatekelezwa kikamilifu, kwani vyama vya upinzani ha- vipewi haki sawana Chama cha CCM, na CCM bado ina uzoefu wa kujifanya kama ni serikali badalaya kuwa ni chama. Kwa hivyo vyama vya upinzani si vyama vyenye uhuru wakuendesha kazi zao huru, wala kuwa na uhuru wa kuamua jina la chama chao auchama hicho kiwakilishe taifa gani. Mfumo wa vyama vingi wa Tanzania hauheshimu misingi ya Haki za kibinaadam na Kidemokrasia. Zanzibar panahitajika utekelezaji wa misingi wa vyama huru vya kisiasa vyen- yemisingi halali ya kidemikrasia. Upinzani unatakiwa upewe haki zote za kidemokrasia za kuweza kufanya kazi hurbila ya kuingiliwa kati na wafuasi wake kutopatishwa taabu na kufukuzwa kazi kwa sababu ya fikra zao. Zanzibar kunatakiwa kuwe na uwezekano wa kufanya mikutano huru nchini kote , kaskazini, kusini, mashariki na magharibi. Utoaji waruhusa hizo uwe chini ya mikono ya idara isiyo pendelea na sio vyama hivyo kucheleweshwa cheleweshwa wanapodai haki zao. Upinzani uwe na uandishi na utangazaji wa habari huru kwa kutumia vyombo vyao wenyewe pamoja na vyombo vya dola. Upinzani uhakikishiwe kuweko kwa uchaguzi huru utakaoangaliwa na wachunguzi kutoka Umoja wa Mataifa na upinzani ushirikishwe katika tume ya kupanga nakutekeleza uchaguzi. Upinzani lazima kushirikishwa katika Baraza la utungaji wa katiba na utungaji washeria mpya za Zanzibar. Upinzani upewe haki katika huduma mbali mbali za kitaifa . Upinzani ushirikishwe katika madaraka tofauti serikalini. Upinzani ushirikishwe katika kuanzisha mipango ya Mahkama huru. Upinzani uwe na uhuru wa kuunda vyama vyenye utaifa au jina walitakalo. Upinzani ishirikishwe katika mazungumzo ya kuirejeshea Zanzibar kiti chake katika Umoja wa Mataifa. Upinzani uruhusiwe kufanya maandamano na kugoma . Upinzani uruhusiwe kuunda vyama vya wafanyakazi. Upinzani uwe na haki ya kuunda vyama vya wanawake. Upinzani uwe na haki ya kuunda vyama vya vijana. Upinzani na wananchi wa kawaida wawe na haki ya kuunda NGO tofauti. Ili kuhakikisha maisha bora ya Mzanzibari, kuishi kwa usalama na amani,kuheshimu maisha na haki za binaadam za kila Mzanzibari, kumhakikishia kila Mzanzibari haki zote za kihalali za kidemokrasia, pana wajib mkubwa sana kwa wanasiasa wote wa Kizanzibari kutizama na kulinda maslahi ya Wazanzibari wote kwa jumla bila ya kujali chama wakifuatacho. Kwa hivyo viongozi wote wa kisiasa lazima wasahau tofauti zao na kuungana na kutizama maslahi ya nchi nzima. ASP,CCM(ZNZ), Um- ma Parti, ZNP na ZPPP lazima watambuwe kwamba wanawajib mkubwa sana kwa nchi yao na vizazi vyao, na bila ya kuungana watu wataendeleakuangamizana na nchi kuselelea nyuma milele. CUF ni chama pekee kinachowakilisha mirengo yote hiyo tofauti Zanzibar. Kwa hivyo itakuwa jambo lamaana ikiwa viongozi wa ASP, CCM (ZNZ), Umma Party, ZNP na ZPPP wote wataingia katika CUF kuendeleza maslahi ya Zanzibar na CUF wenyewe kabla hawajaungwa mkono na vyama hivyo lazima wakubali kujibadilisha jina na kujiita ZUF na wakati huo huo kuwahakikishia uongozi wa juu wakuu wa vyama vyote hivyo vitakavyojiunga nao.