Umma Party na Muungano
Muda fulani baada ya Mapinduzi, fununu zilianza kuhusu kuundwa kwa Muungano , kwa wakati huo Memba wengi wa Baraza la Mapinduzi hawakujua hatari ya Muungano, hata Karume alo uunda Muungano pamoja na Nyerere, hakuelewa uzito wa khatuwa kama hiyo. Umma Party mara tu kusikia fununu hizo za Muungano ikaanza kuupinga, na ilikuwa kwa sababu ilitanabahi kwamba Zanzibar ingelipoteza uhuru wake pindi khatua hiyo ingelitekelezwa. Umma Party ilitambua umuhimu wakuwa na umoja baina ya nchi za Kiafrika, lakini umoja huo haukuwa lazima uwe wa Muungano wa nchi mbili huru. Wakati huo kiongozi wa Umma Party, Babu, alikuwa safarini Indonesia, kungojewa amekwisha ondoka na kutoshauriwa kwa makusudi, kuhusu uundaji wa Muungano huo. Huku nyuma makada walivyo kuwa wakipinga Muungano, tarehe 23, mwezi wa marchi 1964, wakaitwa Ikulu, Zanzibar na huko Karume akawaambiya kwamba kama hawakuwacha upinzani wao wa Muungano, basi wangeliletewa Wamakonde kufyeka fyeka na kuwapiga mishare na Wamakonde hao. Karume alisahau Okello na Ingen walivyofirigiswa na makada hao. Makada hao hawakushitushwa na vitisho hivyo vitupu, kwani waliujuwa uwezo wa Wamakonde katika medani ya mapambano, wakitumia mishare kupambana na vyombo vya automatic (Karume hatimae akawafukuza nchi wamakonde hao hao ). Zanzibar wakati huo kukawa na vikundi viwili vikubwa, vya Umma, kimoja kikitaka kuchukuwa " khatuwa za kuhitajika" za kuzuwiya Muungano na wengine wakapendekeza asubiriwe Babu arudi kutoka safarini, na kufanya mazungumzo namashauriano. Wakati akiwa njiani, akirudi nyumbani kutoka Indonesia, Babu, huko Pakistan, akapambanishwa na khabari za waandishi wa magazeti na kuulizwa kama alijuwa kuhusu matayarisho ya kuunda Muungano huo na kutakiwa kutoa msimao wake,kwamba aliunga mkono khatuwa hiyo au la; jawabu lake likawa," ndio, alijuwa nakusema kwamba aliliunga mkono suala hilo". Ukweli ulikuwa ni tafauti kabisa nausemi huo na kwamba Babu alikuwa hajajulishwa kuhusu Muungano, na kwa desturi mtu hawezi kuunga mkono au kupinga kitu asichoki juwa. Huku nyuma,Tanganyika, kumbe kulikuwa kumekwisha tayarishwa cello maaluum katika gerezala Simbawanga la kumtilia Babu ndani pindi angelipinga Muungano. Hatimae ikaonekana kwamba majungu ya Muungano huo yalipikwa na shirika la kijasusi la Kimarekani la CIA; kumtia chuki, hofu na wasi wasi Karume, kumghilibu na kumlazimisha mtu huyo kuunda Muungano. Aliyeshirikiana namajasusi hao katika mipango hiyo ya Muungano, alikuwa ni Nyerere. Wakati huo kulikuwa askari wa Tanganyika walikuja Zanzibar kusaidia kulinda usalama.Nyerere kwa hivyo alitishia kuondosha askari polisi wake Zanzibar, pindi Karume angelikataa kujiunga na Muungano. Habari hizo zinakaririwa kwa urefu katika kitabu cha Amrit Wilson (US Foreing policy and Revolution - The Creation ofTanzania) kuhusu vipi Zanzibar ililazimishwa kushiriki katika Muungano huo. Ingelikuwa Umma Party haikusisita, kuchelea na kujiweka nyuma basi labda Muungano wa Marekani na Nyerere usingeliwezekana. Umma Party kama chama chengine chochote lazima kujiendeleze kwa mujib wa wakati na hali ya kinchi na kilimwengu kwa jumla. Kati ya njia moja wapo ya kujiendeleza ni kujikosoa na kukosowana, na chama chochote cha kisiasa kinachojiheshimu na kutizama, kulinda na kuweka maslahi ya nchi mbele, kinawajib wa kutumia mtindo wa kujikosoa na kukosowana. Ingawaje, kuna umuhimuwa kuhadhari na kuweza kujuwa mpaka baina ya siasa ya kinadharia na yautendaji. Umma Party imetumia muda mwingi sana kwa sera hiyo, yaani kutumia wakati kujadili siasa ya kinadharia. Hatimae, mijadala hiyo haikuchukuwa muda mwingi tu, bali imechelewesha utekelezaji wa yale yaliyojadiliwa na hatimae hata kuleta migongano ile isio yakihasama na ile yakihasama. Babu kiongozi wa Umma Party alikuwa mmoja wapo wa wale ambao wakitumia siasa nyingi sana, pale ambapo wakati mwengine palihitaji vitendo. Hasa kwa vile huko Bara baadae kulizuka mkondo wa vijana wenye fikra za kimaendeleo ambao walikuwa na hamu ya kusaidia urekibishaji wa hali ya mambo Visiwani (Wengine hata kutaka kuundwa upya kwa Umma Party). Hali hii baadae ikaipa Umma Party sifa ya kuwa wanasiasa wakinadharia tu, ambao wanakaa wenyewe kwa wenyewe hata kutokaribisha vijana wengine waliokuwa na hamu ya kujiunga nao, katika mijadala ya kisiasa. Hali kama hiyo iliwafaidisha wale tu waliyoweza kushiriki katika baraza hizo na kuwapa nafasi ya kupata elimu bora ya kisiasa. Hali hii ilisababisha hata kukuweko kwa pengo la kisiasa baina ya mwananchi wa kawaida na Uongozi wa Umma Party. Ingawaje, Umma Party ilitanabahi baadhi ya makosa yake, kujikosoa baadhi ya makosa yake na kuweza kusababisha mengi ya mafanikio ya Zanzibar yanayodhihirika hivi leo, na viongozi na wanachama wake kujiunga na mkondo wa maendeleo wa leo. Siasa ya Umma Party, kwa ujumla haikuwa yenye kupinga Umoja au Muungano wa nchi za kiafrika yaliyoamuliwa na kukubaliwa na wananchi wote kwa kupitia kuraya maoni, mradi Umoja au Muungano wenyewe una maslahi ya umma na kuwafikiwa na umma. Mfumo wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar wa miaka thelathini iliyopita, si mfumo wa halali, bali ni wenye sura za kikoloni wa mkubwa kumtawalia mdogo na wa kuigubika Zanzibar isahaulike na isijulikane, na hatimae kuigeuza jimbo. Wazanzibari wengi zaidi hawaupenedelei Muunagano wa aina huo, kwa hivyo Muungano huo unafaa uvunjwe na kama pana haja ya kuunda Muungano wowote basi kufanywe kura ya maoni ya Muungano au Shirikisho, ikiwa kama Muungano au Shirikisho la Afrika ya Mashariki yote au la Zanzibar na Tanganyika, mradi kila nchi iwe na utawala wake kamili, kuwa na Rais wake ikiwa Seif Sharif Hamad au Salmin Amour, pamoja na Baraza la Mawaziri na Bunge huru. Na serikali ya Muungano huo au Shirikisho hilo liwe na mawaziri na wakuu wa maidara wa Shirikisho au wa Muungano wakishughulikiya mambo ya Muungano/Shirikisho hilo tu na sio kuingilia kati katika serikali huru za Tanganyika na Zanzibar, ambazo ziwe na Mabunge yao huru. Nyota ya Muungano imekuwa ikizidi na kuzidi kufifiana kufika hadi CCM kuuogopa Uzanzibari hasa katika uchaguzi ujao na kutaka kuuondowa Uzanzibari. Nyerere yumo katika kulazimisha serikali moja, lakini ajuwe kwamba hili ndilo suala litakalo iuwa CCM moja kwa moja visiwani Zanzibar, na vyovyote Nyerere atakavyo lazimisha, ikiwa seriakli moja au mbili, hata kufa kabla Zanzibar kuwa huru na kuwa na serikali yake wenyewe.
Makosa ya Mapinduzi
Kutekwa nyara kwa mapinduzi kumeathiri kazi muhimu iliyofanywa na Wazanzibari katika kupigania haki zao halali. Udhalimu katika jamii kwa kawaida ndio sababu inayoleta Mapinduzi, ingawaje mara nyingi jina la Mapinduzi linatumika vibaya, au maana yake kutumika ovyo, kutumika pale ipasapo na isipopasa, kama vile Kuudi-ACtaa, Puuch, Kuu ya Ikulu, Kuu ya Kijeshi, mabadiliko yote hayo hali huitwa Mapinduzi, ingawa sifa zake ni nyengine kabisa na zisizo za Kimapinduzi, mfano mzuri wa Kuu ya Ikulu ni ule wa Jumbe kuondoshwa madarakani. Mara nyingi watu hudhani kupindua serikali kwa mabavu ndio Mapinduzi, ilhali ukweli wenyeweni kinyume kabisa. Kwanza hakuna Mapinduzi bila ya kuwa Mapinduzi ya"kimapinduzi", kuangusha serikali bila ya misingi ya kimapinduzi si Mapinduzi.Ujana mapinduzi au siasa ya kimapinduzi haina lazima kuambata na kupindua serikali. Fikra za kimapinduzi ni yale mawazo yanayokusudia kubadilisha maisha ya wanyonge, yaliyoselelezwa nyuma na ya kudhulumiwa kwa madhumuni ya kuleta maisha bora, ya haki na usawa, yaani kubadilisha hali iliyoselelea nyuma na kuleta iliyoendelea. Fikra hizi zinaweza kukuwepo kabla ya mapinduzi ya serikali; bila ya mapinduzi ya serikali au baada ya mapinduzi ya serikali. Hakuna lazima kuwa baada ya kupinduwa serikali siasa itakayofuatiya lazima itakuwa ya kimapinduzi.Siasa ya kimapinduzi ni ile inayopigania mabadiliko ya mfumo wa jamii bora nakuondosha maovu. Hali hii inawezekana kukuwepo ama kwa kupindua serikali au hata bila ya kutumia mabavu ya kupindua serikali. Serikali ya Hizbu imepinduliwa kwa kutumia njia za kimapinduzi, lakini kitendo cha mapinduzi yenyewe mwanzoni hayakuongozwa na wanamapinduzi au na f- ikra za kimapinduzi. Ni baadae ndipo uongozi na fikra za kimapinduzi zilish- irikishwa.Ingawaje, baada ya kuonekana hatari ya kuleta mapinduzi ya kimapinduzi katika Afrika Mashariki ilibidi watu fulani wayasaliti Mapinduzi hayo. Katika muda mfupiwa Mapinduzi ya kimapinduzi ya Zanzibar, program ya kimapinduzi iliweza kupendekezwa na kutekelezwa kama vile, Matibabu na siha bora bure; kupendekezwa -Elimu bure kuanzishwa, Mpango wa Uchumi wa kihalali kupangwa, Ardhi kugawiwa sawa kwa wote, Haki za kimsingi kuhakikishwa, uhuru wamaandishi na wa fikra kupendekezwa, haki za wafanyakazi kuhakikishwa,kupangwa uondoshaji wa vibanda na kuhakikisha makaazi bora kwa masikini naupangaji wa mengi mengineyo ambayo yalitokana na program ya chama cha Umma Party. Hiyo ilikuwa program ya kimapinduzi iliyokuwa na azma ya kubadilishamfumo wa kijamii kongwe na kuleta mfumo wa halali. Siku za mwanzo za Mapinduzi, program hiyo ilitekelezwa kwa kiwango fulani, lakini hatimae, baada ya viongozi walivyo endelea wengi kuhamishwa kupelekwa Bara na kwengineko, kama itavyokaririwa baadae, program hiyo ilisalitiwa .
Matibabu bora yakawekewa Memba wa Baraza la Mapinduzi, kwa kufunguliwa Mapinduzi Wing, Madaktari, Manasi na Wafanyakazi waliyo kuwa na ujuzi tofauti hospitalini na sehemu mbali mbali serikalini na katika jamii wakapigwa vita na kukimbiya nchi na siha, elimu na huduma zote za jamii kurejeshwa khatuwa nying nyuma. Kukiondowa kituo cha siha cha Umoja wa Mataifa (WHO) na kusababisha utapakaaji upya wa magonjwa na kurejea kwa malaria, ugonjwa uliyokuwa umeshatoweka Zanzibar ni kati ya usaliti wa hisia za kimapinduzi. Thamani ya elimu ikashuka kwa kufukuza walimu na wale waliyokuwa na ujuzi, kuwafanya wakimbie nchi na badala yao kuwaweka watoto wa skuli kusomesha maskulini. Kuwapa wataalamu waliyorudi masomoni ng'ambo mishahara ya chini kabisa ya shillingi mia nne (400/ ) wakiwa na shahada za elimu ya juu na ambao wazazi wao wakiwahitajia wawatizame wakishamaliza kusoma, kuliwafanya wakimbie nchi.Kuleta ubaguzi baina ya wanafunzi, kuzuwiya wanafunzi kupata elimu ya juu na kutoa elimu kwa ubaguzi. Kipato kutoka karafuu (shina la uchumi wa nchi)kuhodhiwa na Karume na shirika la biashara la ZSTC, kutoagizia chakula na watu wakawekwa na njaa. Kutotekelezwa kwa mpango wa uchumi wa miaka mitatu, na badala yake kubuni uchumi usioku- wa na mbele wala nyuma. Kuchukuwa kwa eka tatu tatu za ardhi zenye rutba, na zaidi ya moja, na Memba wa Baraz- a la Mapinduzi. Viongozi wa Baraza la Mapinduzi kujenga majumba mazuri kwa kuiba mali ya serikali, kama vile vitu vya maonyesho vya Makumbusho na kuwaibia watu binafsi milango na madirisha yao na kutia katika majumba yao. Pamoja na kuiba nakunyanganya mali tofauti pamoja na kuozwa kwa watu kwa nguvu na mengi mengineyo yakina Ali Mzee Mbalia na wengineo, hayakuwa mambo ya kimapinduzi,bali ya upinduzi. Haki za kimsingi karibu zote kupigwa marufuku, kama vile kutolewa kauli ya kutofanywa uchaguzi kwa miaka 50, kutoruhusu uandishi na usomaji huru, kuondosha Mahkama za kisheria na haki ya utetezi huru, kuendeleza sheria yakuweka watu kizuizini na kuuwawa kwa watu kwa sababu ya fikra zao za kisiasa. Kufunga Umoja wa vyama vya Wafanyakazi na Wanafunzi (The Federation of Revolutionary Trade Unions na Zanzibar Revolutionary Students Union). Kufuja mipango ya kuwapatia Wazanzibari wote nyumba nzuri zilizoambatana na mazingara ya Zanzibar, kama zile nyumba za Bambi, ilivurugwa vur ugwa na hatimaepakajengwa nyumba za mabogi ya gari la moshi pasipo na ujuzi wowote. Kwenda kinyume huku na program ya kuwatowa Wazanzibari katika mfumo zorota ulitokana na upungufu wa ufahamivu wa fikra za kimapinduzi ndio ulosababisha leo kuifanya Zanzibar iko nyuma, masikini na kuwezesha kutawaliwa na Muungano.
Vuguvugu la Venceremos
Kwa nini kulikuwa na haja ya kuunda Muungano na nani hasa aliyetaka Muungano huo. Ingawa fununu kuhusu Mapinduzi ya Zanzibar yalikuwa yameshawafikia Wakoloni pamoja na Mashirika ya Kijasusi, kama ilivyokwisha kaririwa huko nyuma. Watu hao walishindwa kuamini habari hizo, hasa kwa vile nyendo za Umma Party zilikuwa hazi kuonyesha harakati zozote zilizokuwa si za kawaida, kwa hivyo habari hizo zikadharauliwa. Walipokuja kutahamaki, serikali ya Hizbu imekwisha pinduliwa na baada ya hapo hali ya hewa na mazinga ra ya Zanzibar yalibadilika kwa ghafla na kujaaa hamasa za kimapinduzi na muamko wa kimaendeleo, kukataa sera kongwe za kijamii na kuleta mfumo mpya wa kujikombowa. Bila ya muda mrefu kupita upepowa kimapinduzi ukaanza kupepea Afrika ya Mashariki nzima na kutikisa mizizi ya tawala za kitimba kwiri za nchi hizo. Wamarekani na Wangereza walipoanza kusikia "Venceremos Patriomuerte "(tutakubali kufa lakini si kushindwa) wakashituka na kudhani Cuba ya pili imekwisha zaliwa na wakaona maslahi yao yako hatarini hasa kama wangeliruhusu upepo wa kimapinduzi uliyojaa jazba za kijananchi na nia ya kujitolea uliyokuwa ukipepea Zanzibar na kutambaa Afrika ya Mashariki na ya Kati. Viongozi wa Afrika ya Mashariki nao, akina Nyerere, Obote na Kenyatta wakaingiwa na wasi wasi wakupinduliwa na kwa pamoja na kwa msaada wa Marekani na Mngereza wakawa wanajitayarisha kuivamia Zanzibar kijeshi. Kenyatta na Obote hatimae wakajitoa katika mipango hiyo na mwishowe akabaki Nyerere peke yake (soma kitabu cha Amrit Wilson kinachokariri jinsi Nyerere na Ujasusi wa Kimarekani walivyo shirikiana kuulazimisha Muungano wa Tanzania). Nyerere akamshawishi naku- mtia uoga Karume na kila mmoja kati yao akiwa na sababu zake, wakashirikiana kuunda Muungano huo bila ya kuwashauri watu wao. Sababu mojawapo iliyomfanya Nyerere ashituke na kuogopa mapinduzi ilitokana na hatuwa ya jeshi lake kutaka kumpinduwa na sababu yake ya pili ilimbidi awatumikie wafadhili na mabwana zake Marekani na Mngereza (ambaye alimuokoa kijeshi siku za ghasia za Colito Barrackswiki tu baada ya Mapinduzi ya Zanzibar). Wamarekani na Wangereza walitishwa na mfumo mpya uliokuwa na program ya ki mapinduzi na kuhatarisha maslahi yao ya kiuchumi na kisiasa. Karume, kwa upande wake, alikuwa na matatizo yake mbalimbali na yale ya mstari wa mbele yalikuwa kwa uroho, kujaribu kuhifadhi uongozi wake usichukuliwe na Othman Sharif na Abdalla Kassim Hanga, watu hawa wakishirikiana na viongozi wengine waliyosoma na waloendelea katika ASP. Kwa upande wa pili Karume alihisi kwamba siasa yake ya zamani haikuweza kuwaletea wana Afro tija yoyote, wakati siasa mpya iliyokuwa na program ya kimapinduzi, ghafla iliibadilisha sura ya Zanzibar na kungwa mkono na Wazanzibari wengi. Kwa hivyo Nyerere hakuwa na haja ya kutumia ustadi mwingi wa kumfanya Karume kukubali pendekezo la Muungano, wote wawili walitaka kuhifadhi khatamu zao za utawala na maslahi yao wenyewe. Kwa kisiri siri na haraka haraka, na kwa msaada wa wataalam wa sheria wa kikoloni, ikaundwa Katiba ya muda ya Muungano bila yakushirikishwa Wanasheria wa Zanzibar au maoni ya wananchi kuulizwa. Katiba hiyo ilifuata mfano wa katiba ya Uingereza na Ireland ya Kaskazini, yaani baina ya mtawala na mtawaliwa, Tanganyika ya Nyerere ikiwa mtawala. Maandishi mengi yakisheria yamejadili upungufu wa Uhalali wa Katiba hiyo na Muungano wenyewe kwa jumla. Serikali ya Tanzania bado haija jibu hoja hizo, isipokuwa kila usiku uchao kuleta mapendekezo mepya ya kuidhibiti Zanzibar. Utangazaji wa makubaliano hayo baina ya Nyerere na Karume yalifanywa makusudiwakati A. M. Babu kiongozi wa Umma Party alipokuwa hayupo nchini. Baada yahapo, karibu viongozi wote waliyokuwa na fikra za kimaendeleo au waliyokuwa na haki ya kuongoza ASP wa kaondoshwa nchini, ama kupelekwa Bara au katika Mabalozi mbali mbali. Kati ya waliyoondoshwa nchini kwa sababu ya Muungano na upingaji wa udikteta na ukoloni mambo leo walikuwa A. M. Babu, A. K. Hanga,Othman Sharif, Salim Ahmed Salim, Salim Rashid, Mohammed Ali Foum, Hasnu Makame, Idris Abdulwakil, Ali Mwinyi Gogo, Adam Mwakanjuki, Ali Khamis nawengi wengineo. Wale viongozi wa ASP waliyobaki Zanzibar na kupinga udikteta na Muungano na kuwa na fikra za kimaendeleo, karibu wote waliuwawa; hawa ni akina Sa leh Sadalla, Abdulaziz Twala, Mdungi Usi, Khamis Masoud, Jimmy Ringo,Idrisa Majuya, Jaha Ubwa, Ngwali Usi n.k. Viongozi wachache wa Wafanyakazi walibaki Zanzibar na hata hao baada ya muda kupita na wao wakaombolea gerezani na kuteswa. Karibu makada wote wa Umma waliyo somea mapambano ya kigorilla huko Cuba pamoja na makada wengine wakasafirishwa kwenda ama Urusi au Indonesia. Wengi kabisa wa Wazanzibari waliyosoma walilamika kuhama au kuhamishwa nchi, wengi wao kuifaidisha Bara kwa elimu na ujuzi wao na kuwacha pengo kubwa la ujuzi Zanzibar. Baada ya vikosi vyote hivyo vya kijananchi kuondoshwa Zanzibar, Muungano ukazidi kutia mizizi, hatimae kuletewa wataalam wa mabibo kuja kutibu mikarafuu. Ingawaje Wazanzibari hawaku kubali kukaa kimya bali mapambano na vuguvugu la chini kwa chini yaliendelea. Katika mwaka 1972,mwezi wa Aprili tarehe saba Karume akapigwa risasi na kuuwawa, na mandhara mpaya ya kisiasa ikachipuka. Kufuatia tukio hilo maelfu ya watu wakatiwa ndani,kati yao wakiwa wengi wa Viongozi wa Umma Party pamoja na baadhi ya makada. Baadae pakafanywa kesi, na kesi hiyo ikaendeshwa katika Mahkama iliyokuwa siya kisheria kwa vile Mahakimu hao walikuwa hawana ujuzi wa kisheria, waliyokuwa ni watu wenye sura za kimapendeleo kwa vile walikuwa wafuasi wa chama tawala tuna washtakiwa kutoruhusiwa mawakili wa kisheria wa kuwatetea. Mkuu wamashtaka hayo ndie wakati huo huo akiwashtaki na wakati huo huo kupewa wadhifa wa kuwatetea washtakiwa hao hao. Baadhi yao walishtakiwa wakiwa hawapo, yaani wakiwa Bara na mmoja Salim Ahmed Salim akiwa nchi za nje kama Balozi waTanzania, mashtaka yake hatimae yakafifirishwa. Wafuatao ndio waliyoshtakiwa: 1. A. M. Babu 2. Khamis A. Ameir 3. A. B. Qullatein 4. Amar Salim Saad 5. Nurbhai Issa 6. Ali Sultan Issa 7. Abdulrazak M. Simai 8. Mussa Shaaban 9. Moh'd A. Baramia 10. Kadiria Mnyeji 11. Miraji Mpatani 12. Ali Mshangama 13. Haroub M. Salim 14. Hussein Mbaruk 15. Moh'd S. Mtendeni 16. Cpt.Abdulla Khamis 17. Said Moh'd Said 18. Ali Seif Karkoboi 19. Cpt. Abdull Moh'd 20. R. Moh'd Rashid 21. Lt. M. A. Chululu 22. Lt. Salim A.Rashid 23. Sgt. Humud Ali 24. Yusuf Ramadhan 25. Col. Ali Mahfoudh 26. Cpt. Hassan Makame 27. Moh'd Ali Seif 28. Said Salim Said 29. Naaman Marshed 30. Ali Hemed Humud 31. Ishaq Juma Harakati 32. Rashid M. Ahmed 33. Juma Mussa Juma 34. Ibrahim M. Hussein 35. Khamis Masoud 36. Moh'd A. Ladha 37. Moh'd A. Sahir 38. Moh'd Khalef Moh'd 39. Salim Abdalla Saleh 40. Saleh Ali Saleh 41. Moh'd Said Moh'd 42. Khamis Abeid Omar 43. Ibrahim Omar Soud 44. Abdulla Mussa Moh'd 45. Alawi Tahir Moh'd 46. Moh'd Khalfan Salim 47. Ahmada Shafi 48. Hassan Said 49. Tahir Adnan 50. Ali Mzee Mbalia 51. R. M. Rashid 52. Lt.Salum A. Rashid 53. Seif Said Hamadi 54. Lt.Mikidadi Abdulla 55. Lt. Ali Othman 56. Abas Mohammed 57. Lt. Abdulla Juma 58. Lt. Ahmed M. Habib 59. Cpt. Suleiman Moh'd 60. Lt.Hashil S. Hashil 61. Cpt. Hemed Hilal 62. Lt. Shaaban Salim 63. Lt. Amour Dg'hesh 64. Maj. Salim S. Salim 65. Lt. Haji Othman 66. Tahir Ali 67. Badru Said Badru 68. Abdulaziz Abdkadir 69. Ali Salim Hafidh 70. Ali M. Ali Nabwa 71. Moh'd A. Ameir 72. Ali Y. Baalawy 73. Saleh Abdulla Waliyoshtakiwa wote walikuwa 81, wengine waliwachiliwa mapema.
Awamu tafauti
Baada ya kuuwawa Karume hali ya mambo ikaanza kubadilika Zanzibar. Kwanza kulikuwa na mchuano mkubwa wa kugombania khatamu za utawala baina ya Aboud Jumbe na Seif Bakari, ambaye ndie aliyekuwa chini ya Karume. Nyerere akaamua kumuunga mkono Aboud Jumbe. Jumbe alileta mabadiliko tofauti visiwani, kama vile kuruhusu watu kutoa maoni yao, kukosoa bila ya kuogopa kutiwa ndani. Aliruhusu waliyoshutumia katika kesi ya uhaini kupandishwa Mahkamani, ingawa Mahkama yenyewe ilikuwa haijatoa ruhusa ya utetezi huru au kuwa na Mahakimu waliyosomea sheria. Katika utawala wake Jumbe aliweza kuondosha khofu, kuheshimu wasomi, kupunguza nguvu za Memba wa Baraza la Mapinduzi, na kuleta nafuu kwa kadri fulani. Alianzisha Baraza la Wawakilishi. Ingawaje kwa sababu yamigongano yake na Baraza la Mapinduzi likiongozwa na Seif Bakari akazidi kuitia Zanzibar katika kabari ya Muungano. Baadae Jumbe nae akaanza kuwa muamuzi wapekee. Baada ya muda fulani kupita Jumbe nae kama Karume, akaanza kutan- abahi uovu wa Muungano na akaanzisha mbinu za kuitoa Zanzibar katika Muungano. Lakini kwa bahati mbaya makosa aliyokwisha yafanya ya kuizamisha Zanzibar katika matope ya Muungano yalikuwa ni mengi na kumzamisha mwenyewe kila alipojaribu kujitowa. Kosa kubwa kabisa alilolifanya Jumbe dhidi ya maslahi ya Zanzibar ilikuwa ni kukifufua chama cha ASP (viongozi wake halisi kwisha kuteketezwa) na baadae kukiunganisha na TANU na hatimae ku- zaliwa CCM, MAMA WA BALAA LOTE. Baadae chama hicho hicho cha CCM alichokuwa mmoja wawakunga wake kikamfukuza kwenye uongozi kama kitakataka. Baada ya kuondoshwa na kuuzuliwa Jumbe kwa muadhara mkubwa, akawekwa Ali Mwinyi, ambaye siku za mwanzo alipendeza sana Zanzibar lakini baadae akababaishwa na Urais wa Muungano na kuusahau Uzanzibari wake. Idris Abdul-wakil (mmoja kati ya wale viongozi waliyojitowa ASP 1964) baada yakuchukuwa pahala pa Ali Mwinyi akagonganishwa na Wazanzibari wenzake.Kufuatia tukio hilo kundi la watu Saba likiongozwa na Seif Sharif Hamadi likafukuzwa Chama na kutolewa madarakani. Idris Abdulwakil nae nyota yake mwishowe ikafifia katika CCM ya Nyerere, na wakati CCM inapanga kumuuzulu, Idris akawawahi na kujiuzulu mwenyewe na kujikosha na balaa la Muungano. Salmin Amour akashika ukanda lakini kabla hajawahi kukaa vizuri katika Kiti chake Salmin akajiona kwamba alikuwa "Chui wa Karatasi" asiyekuwa na meno walamakucha. Hali hiyo ilidhihirika wakati alipoiunganisha Zanzibar na Jumuiya wa Nchi za Kiislaam. Bila ya mapenzi yake akaambiwa aitowe Zanzibar katika Jumuiya hiyo. Hapo akatanabahi kwamba Urais wake wa Zanzibar ulikuwa ni wa jina tupu, usiyokuwa na nguvu sawa hata za Waziri mdogo wa Bara. Wakati huo alitakiwa Rais Amour aonyeshe "Ushupavu" wake kama Kiongozi mwenye uzito na ama kuitoa ASP katika CCM au kuitoa Zanzibar katika Muungano. Wapiiii, kipindi cha kihistoria kimempita Rais Amour na Wazanzibari itabidi wangojee ushupavu wa Rais mpya atakayekuwa na ukakamavu na ushupavu wa kutosha unostahiki Rais wa nchi. Amour nyota yake nae imekwishafifia katika CCM na Nyerere yumo kumtayarisha Dr. Omar au mwengine kama huyo kuchukuwa madaraka.
Migogoro ya Nyerere na Karume
Nyerere kwa mara nyingi katika historia ya Zanzibar amekuwa akijaribu kuwaamulia Wazanzibari nini la kufanya kama vile wao wenyewe hawajajiweza. Kwa ujanja na ulaghai wake aliweza kufanikiwa kutia fitina baina ya Wazanzibari wenyewe kwa wenyewe kama vile Mngereza alivyofanya siku za nyuma. Wakati wa mwanzoni watu wengi hawakuelewa nini azma ya Nyerere, na kumdhani kama ni mtu mwema, lakini hatimae ilidhihirika kwamba alikuwa akitaka kuitawala Zanzibar. Kwa upande mmoja, kati ya baadhi ya njama zake, baada ya kuundwa Muungano, alisaidia na kuhakikisha kwamba wale Wazanzibari waliyokuwa wamesoma walihamishwa Zanzibar. Kwa njia kama hiyo sehemu kubwa ya uongozi uliyobaki Zanzibar ulikuwa ni wa wale wasiosoma, ambao aliweza kuwaendesha na kuwadanganya kama alivyotaka. Kwa upande wa pili, ingawa suala la usalama lilikuwa chini ya Muungano na Nyerere ndiye aliyekuwa mkuu wa Muungano, ili kuhifadhi maisha ya Muungano huo alikataa kuhami maisha ya viongozi wa Kizanzibari waliyouwawa kwa sababu ya kuwa na fikra tofauti za kisiasa. Kwaupande wa tatu Nyerere aliwatumilia wale waliyoitwa Wabunge wa Zanzibar, Bungeni Dar es salaam, kuwazuwia Wabunge wa Tanganyika kumshambulia Nyerere na serikali yake. Wabunge hao wa Zanzibar waliogopa kuwasaidia Wabunge wa Tanganyika kwa vile waliporudi Zanzibar walim'haha Karume ambaye asingelisita kuwapeleka chuoni kwa Mandera, kwenda kudurusu. Kwa njia hii Nyerere aliweza kudhibiti utawala wa Tanganyika na wa Zanzibar kwa wakati mmoja. Ingawaje, kulifika wakati fulani ambapo, maingiliano baina ya Karume na Nyerere hayakuwa mazuri na Karume alifanya njama na mbinu za kum adhiri Nyerere kila alipopata nafasi. Katika mwaka wa 1971 Karume alifanya mbinu i li ahakikishe kwamba, ikiwa kwa sababu yoyote Nyerere atasita kuwa Rais, basi yeye Karume ndiye ahakikishiwe Urais wa Tanzania. Mipango hiyo aliwahi kuipendekeza hatambele ya mkutano wa Baraza la Mawaziri. Nyerere akamshitukiya Karume, na akamsail Karume mbele ya mawaziri, na kumuuliza kama Karume alitarajia kuchukuwa Urais akifa Nyerere. Kama kawaida ya mgogoro kama huo, Jumbe aliingilia kati na kumhakikishia Nyerere kwamba" Karume hakuwa na azma mbaya na yeye, bali Karume alieleweka vibaya". Nyerere bi- la ya kufikiri na kutanabahi sana, kwa haraka haraka, kama desturi yake akatunga sheria mpya ya Tanzania Bara, na kuipa serikali uwezo wa kuwa na Waziri Mkuu, ili kama yeye Nyerere kwa sababu hii au ile angelikutwa na ajali ya kifo cha ghafla, basi Waziri Mkuu huyo ndiye aliyekuwa achukuwe ukanda wa Urais wa Muungano na sio Makamu wa Kwanza wa Rais, yaani Karume .Uamuzi huu ulimkasirisha sana Karume kwa vile aliona kwamba uwezekano wake wa kuwa Rais, pindi Nyerere akifa ulififirishwa na kuondoshwa, na kwamba Waziri Mkuu huyo atakuwa wa Zanzibar vile vile. Ingawaje, Karume hakukubali kushindwa, kwani alidai kwamba kitendo hicho cha Nyerere cha kujiamuliya hivyo ilikuwa ni, kuiruka na kuikuuka Katiba ya Muungano na kujiamulia kuteuwa na kuanzisha Wadhifa wa Waziri Mkuu kulikuwani kinyume na Katiba ya Tanzania. Kwa hivyo Karume akaamuwa kumpeleka Nyerere Mahkamani kwa kuikiuka Katiba. (Tutakumbuka baadae hata Jumbe nae alitaka kumpeleka Nyerere katika Mahkama kwa kukiuka makubaliano ya maandhishi ya Muungano.) Karume tokea mwaka 1970 alikuwa ameanza kampeni kali sana ya kwenda sehemu mbali mbali kama vile Kariakoo na kwenda kuwahutubia makabwela na kutia fitna dhidi ya Nyerere na kuwaahidi makabwera kazi na nyumba bure Zanzibar kama Nyerere angelishindwa kuwapatia vitu hivyo Bara. Karume vile vile alikuwa akitowa mapesa kuwapa vilabu vya mipira vya Bara ili kuwavutia na siasa yake, wakati huo huo Wazanzibari wakikaa na njaa. Karume alijaribu kuwashawishi wanajeshi wa Kizanzibari waliyokuwa Bara, kumpelekea khabari za kijasusi dhidi ya utawala wa Nyerere. Isitoshe katika sherehe za miaka kumi ya uhuru wa Tanganyika, Karume alipeleka Dar es salaam majeshi ya Zanzibar na silaha kubwa kubwa, ikiwemo mizinga tofauti. Majeshi hayo yanasemekana yalikuwa yajiandae sehemu mbili tofauti za Uwanja wa Taifa ambako sherehe hizo zilikuwa zifanyike. Uwanja huo uliwekwa katikati na makombora na mafashi fashi yalikuwa yakutanie katika ya anga ya Uwanja huo. Makombora hayo yalikuwa yatupwe kutoka hizo sehemu mbili tofauti, moja sehemu ya Mgulani na nyengine sehemu za Mjini. Hapo watu wangelikuwa wakishughulika na kutizama mafashi fashi angani, na wale askari wa jeshi la Zanzibar waliyoshiriki katika paredi hiyo wangelimtwanga risasi Nyerere na Karume angelishika ukanda kufuatia kifo cha Nyerere. Kiongozi mmoja wa jeshi la Zanzibar aliyekuwa aongoze majambo hayo, bahati mbaya amekwishakufa, nae alikuwa Col. Mussa Maisara, lakini wakuu wengine wengi wa kitendo hicho bado wahai. Kwa bahati wanajeshi wa Bara walishituka, kutokana na hemkahemka na kwa sababu ya idadi ya askari wa kushiriki katika sherehe hizo kutoka Zanzibar iliwashitua Jeshi la Bara na vile vile kushitushwa na wingi wa silaha hasa zikiwa silaha kubwa kubwa. Vile vile kile kitendo cha wanajeshi wa Zanzibar waliyo omba kutumia nafasi ya zile sehemu zilizokuwa na ulinzi mkali ili kutekelezea matayarisho ya tafrija zao, zilitia wasi wasi. Baada ya kuchekechwa kwa makini Wanajeshi wa Bara wakanusia harufu ya hatari na kwa hivyo hizo sherehe zikaaghirishwa na Nyerere kujificha. Baada ya tukio hilo Col. Ali Mahfoudh akarejeshwa Zanzibar. Karume hakumuwahi Nyerere bali akawahiwa yeye. Baada ya kuuwawa kwa Karume, Nyerere akaanza kutamba. Katika maziko ya Karume, Nyerere akatokwa na machozi ya mamba, huku akichekelea ndani kwa ndani na kuukaribisha wakati mpya. Ingawa wakati Karume alipokuwa hai Nyerere alidai kwamba Wazanzibari walivyokuwa wakiteswa na kuuliwa yeye hakuwa na uwezo wa kuingilia kati mambo ya ndani ya serikali ya Zanzibar, lakini mara tu baada ya kuuwawa Karume, Nyerere mwenyewe hakusita kuchukuwa fursa ya kuwatiya ndani maelfu ya Wazanzibari waliyokuwa Tanganyika. Wengi ya Wazanzibari hao hawakuwa hata wanasiasa, wangine walikamatwa kwa kusingiziwa ati wamesherehekea kifo cha Karume kwa kupika pilau ya kuku, huko Bara; au mtu mmoja, Mzee Salim, alitiwa ndani kutoka kijiji cha Ujamaa, ati kwa sababu aliweka dhamiri kwamba, ikiwa Karume atak- ufa basi atakula ugari chini, mchanga ukiwa sahani yake, na mtu huyo akatiwa ndani atikwa sababu alionekana akila huo ugari chini. Ingawaje kutiwa ndani kwa watu wengine baada ya kufa Karume kulikuwa na madhumuni maalum ya kuunufaisha utawala wa Nyerere. Shabaha moja muhimu ya kwa nini mfano Babu alitiwa ndani, ilikuwa na madhumuni maalum kama yale ya 1964 ya kumuondosha Babu, Hanga n.k. wasije kuchafuwa mambo ya Muungano, kwani kwa mujib wa ngazi za utawala wa Zanzibar Kinara alikuwa Karume, chini yake akawa Hanga na baada ya Hanga alikuwa Babu. Kwa hivyo maadhali Hanga, kwa wakati huo alikuwa amekwisha uwawa, kwa hivyo kufuatilia kifo cha Karume aliyekuwa ashike ukanda wa madaraka ya Utawala wa Zanzibar alikuwa awe Babu (tazama orodha ya Baraza la - Mapinduzi, 1964) na sio Jumbe ambae alikuwa kiongozi wa tano katika orodha hiyo. Muungano uliundwa kuizuwiya Zanzibar isifuate mwenendo wa kimaendeleo ambao hatimae ungeli wafanya Watanganyika kudai maendeleo kama hayo na hatimae kumuondosha Nyerere. Babu na Umma Party, pamoja na mamilitanti wa ASP walionekana kama ni watu waliyoitakia Zanzibar msimamo madhubuti, uliyokuwa huru na wakimaendeleo, na kuwa dhidi ya azma na njama za Muungano wa Nyerere.Kwa hivyo kuuwawa kwa viongozi tofauti Zanzibar na kutiwa ndani kwa Babu kufuatia kifo cha Karume kulikuwa na madhumuni yale yale kama ya kuunda Muungano, yaani kuimarisha Muungano usiyoamuliwa na watu. Babu na Umma Party kwa jumla waliwekwa ndani kwa miaka sita, bila ya kufunguliwa kesi yoyote huko Tanganyika ya wale aliyokuwa wametiwa ndani Tanganyika, na wale waliyokuwa gerezani Zanzibar kuteswa kikatili, wengine kuuwawa na halafu kufanyiwa kesi isiyokuwa na Mahakimu wa Kitaalam, wasiopendelea upande wowote, wala kuwa na uwezo wa kupata mawakili wakuwatetea ambao waliwachaguwa na kuwataka wenyewe. Kama Nyerere angelikuwa ametaka kesi halali ifanyike, asingelishindwa kufanya hivyo, kwani kwa wakati huo ule aliyekuwa akimuogopa alikuwa hayuko tena na alikuwa na nguvu za kutoshaza kuweza kufanya atakacho Zanzibar, kama tulivyoona baadae, alivyo wasambaza kina Seif Bakari. Nyerere aliogopa kesi kufanyika Tanganyika kwa sababu aliogopa ufichuliwaji wa mizoga aliyoificha katika makasha na makabati yake na kuogopa, kama Babu angelimuacha nje Wazanzibari wangelimtaka awaongoze.
Tanganyika imepiga kamba
Tanganyika kwa kuunganishwa na Zanzibar imeathirika kama Zanzibar ilivyoathirika, na kugeuzwa kama watu wawili waliyopeyana migongo, kufungwa kamba pamoja na kuambiwa washindane mbio kila mmoja akielekea kwake, halafu atafutwe mshindi. Sababu mojawapo ya kuunganishwa kwa nchi mbili hizi ilikuwa nikupunguza kasi za maendeleo ya Zanzibar na kwa njia hiyo kuepusha hamasa kama hizo zisije zikatambaa Tanganyika na kuwafanya wananchi wa huko kuanza kuzidi kudai haki zao zilizotokana na majasho yao. Hali hii hatimae ingelileta mgogoro kwa Wakoloni mambo leo, mabeberu na wanyonyaji kwa jumla. Kuambatana na vuguvugu hilo wananchi wa Tanganyika wangelidai maendeleo zaidi ambayo hatimae yangeliwafanya kuweza kujitegemea zaidi na kuwa huru zaidi. Wapata hasara wangelikuwa ni watawala wa Kibeberu waliyomiliki njia na funguo zote za uzalishaji mali na ambao wanaamua thamani ya jasho la mfanya kazi na bei za bidhaa ulimwenguni, bidhaa ambazo kwa daima zikimdhalilisha, kunmyonya na kumkandamiza mnyonge ambae ni Mtanganyika na Mzanzibari wa chini. Wakati huo huo kumlazimisha alime chai, kahawa na pili pili hoho na asilime chakula chake chakujishibisha yeye na ukoo wake na kuhakikisha kwamba uchumi umedhibitiwa na wale wale watawala wetu wa zamani. Kutokana na utawala wa kikatili wa kijerumani Watanganyika hata alipokwisha ondoka Mjerumani huko Tnaganyika, walibaki kuwa wananchi watiifu sana, waliyopenda usalama na waliyokuwa hawapendi vurugu. Suala jengine muhimu- lilo wasononesha Watanganyika ni lile la mwaka 1964 wakati walipojaribu kuchukuwa silaha dhidi ya Nyerere, hatimae walimuona Mngereza kaleta majeshi yake kumtetea Nyerere na kuwakandamiza Watanganyika, kwa hivyo Watanganyika walihisi kwamba kama wangelimu ondosha Nyerere basi Mngereza angeli rudisha tena kwa kutumia mabavu na ndio maana baadae walisita sita kumuondowa Nyerere, hasakwa vile wale waliyokuwa na fikra kama hizo waliambulia kuwekwa vizuizini hadi kuota ukungu. Hii ni sababu mojawapo ambayo ilimuwezesha Nyerere kuweza kuwatala Watanganyika bila vuguvugu au mapambano makali. Kwa vile Tanganyika kulikuwa na makabila mbali mbali, Watanganyika vile vile walishindwa kuunganana kuweza kumpa Nyerere upinzani wa kutosha ambao hatimae ungeli waletea maendeleo. Waliyoathirika na kuteseka zaidi katika Muungano huu, walikuwa bila ya shaka yoyote, ni Wazanzibari, kwani wao walitawaliwa mara mbili, yaani walitawaliwa na Muungano na wakati huo huo kutawaliwa na utawala wa kikatili, wautesaji na wa kiuwaji. Watanganyika walitawaliwa na Muungano (ambao kwa kweli ukiendeshwa na serikali ya Tanganyika) wa Nyerere tu, in- gawa baadhi ya Watanganyika walipowekwa vizuizini walivushwa kwenda Unguja kushuhudia nakuonja mateso ya gerezani kwa Mandera. Chini ya jina la Muungano, Watanganyika walinyimwa me ngi, hata mambo yale ya kawaida ya nchi huru, kama vile kuwa na Bunge lao wenyewe, ambamo wangeliweza kukaa kwa siri au kwa dhahiri na kuamuwa mambo ya maslahi yao wenyewe. Kunyimwa kwa Watangayika kwa kikao huru kama hiki hakijawanyima Watanganyika tu ku jitambua kama Taifa na Nchi huru, bali papo kulileta athara kubwa mno kwa- Wazanzibari. Watanganyika walikuwa wakijuwa wazi mateso ya kikatili yaliyokuwa yakiwapata Wazanzibari wakati wa Karume; kinyimwa chakula, kunyimwa masomo, kuozwa kwa nguvu,kufukuzwa nchi walizozaliwa, kutokuwa na usalama, kunyanganywa wake zao kwa nguvu, kutishwa saa zote, kupewa mishahara ya chini, kutokuwa na haki za kifanyakazi na kikulima, wanawake kutoheshimiwa na kutowakilishwa, vijana kulazimishwa kufanya kazi makambi ya kazi bila manufaa yoyote, kuzuiliwa kusafirikwa wanafunzi, kupigwa risasi watu msikitini, kutiwa vizuizini kwa mashekhe, kukimbizwa kwa wataalam na kufukuzwa kwa shirika la siha la Umoja wa Mataifa(WHO), kuhamisha Wazanzibari waliyosoma na waliyokuwa na fikra za kimaendeleo,kunyang'anywa ovyo kwa mali za watu, kutiwa nd ani kwa ovyo kwa watu wenye fikra tofauti vizuizini, kuteswa kwa vipigo vya kinyama mbali mbali kwa waliyotiwa vizuizini, kuuwawa kwa Viongozi wa Kisiasa waliyokuwa na fikra tofauti na Karume na mengi mengine maovu; ingawa yote haya wakiyajuwa, Watanganyika waliyanyamazia kimya, maonevu yote haya ya kikatili, kutotetea haki za kibinaadam za Wazanzibari na badala yake walinong'ona pembeni pembeni tu.Pindi Watanganyika wan gelikuwa na Bunge lao huru wakati huo, basi Wazanzibari wanaamini kwamba mateso hayo ya Wazanzibari wasingeliyanyamaziya na waasingeliruhusu jeshi la Tanz- ania kumhami Karume. Kwa hivyo Watanganyika hawana haki tu ya kuwa na Bunge lao huru kama Taifa na Nchi yeyote huru ulimwenguni, bali wana lazima na wajib wa kupiganiwa haki hiyo. Kuwepo kwa Bunge huru la Tanganyika kunatarajiwa kuleta haki za kidemokrasia halali zitazopigania hata haki za Wazanzibari. Na Mzanzibari yeyote yule ambaye atapinga haki za Watanganyika kuwa na Bunge huru basi si mpinga mandeleo ya Tanganyika peke yake, bali wakati huo huo mtaka kuwaona Wazanzibari wanateseka milele.
CCM hazina ya baa na balaa
Kama ilivyokwisha kaririwa huko nyuma Mapinduzi ya 1964 hayakupangwa wala kutekelezwa na ASP, bali na sehemu ya ASYL na hatimae Umoja huo wa Vijana ukahakikisha kutoweka kwa karibu viongozi wote wa juu wa ASP, wakiwemo kina Hanga, Othman Sharif, Saleh Sadalla, Mdungi Usi, Ngwali Usi, Khamis Masoud, Abdulaziz Twala n.k. Chama hasa kilichokuwa kiki tawala Zanzibar baada ya Mapinduzi, kwa hivyo hakikuwa ASP bali ilikuwa ASYL ambayo ilishirikiana na Karume kuuwa, kutawala kwa mabavu, na nguvu za mwisho zikiwa katika Kamati ya Watu 14 wa Baraza la Mapinduzi ambao wote walikuwa ni ASYL, Karume aliingizwa baada ya Okello kufukuzwa nchi. Aboud Jumbe, hakuwa- mwana ASYL, wala kuwa mwana kamati wa Kamati ya watu 14, kwa hivyo Jumbe alipopata khatamu za utawala akiungwa mkono na Nyerere ikambidi ajenge Boma lake mwenyewe. Kwahivyo akajaribu kuifufua ASP, lakini hichi hakikuwa kile chama cha ASP kilichotambulika kabla, kwani viongozi wake wote halisia walikwisha toweshwa, kwa hivyo viongozi wa juu wa chama hicho kipya hatimae wakabaki wale wale wana ASYL. Itakumbukwa, mara tu baada ya kuuwawa Karume jinsi Aboud Jumbe alivyokuwa akitatanishwa na Seif Bakari, ambae alijihisi kuwa na haki ya Urais wa Zanzibar, baada ya kufa Karume. Wakati Seif Bakari alipotishia kutumia nguvu za kijeshi, kwa vile jeshi la Zanzibar lilikuwa chini yake, Nyerere akaingilia kati na kumkanya Seif Bakari awache njama za kutaka kumpinduwa Jumbe na kama angelijaribu kufanya hivyo basi angelikiona cha mtema kuni Nyerere; Seif Bakari akaufyata. Kufuatia shida na matatizo ya kila aina ya Zanzibar wanachama wa zamani wa ASP ndio waliyoteseka zaidi kuliko hata wafuasi wa vyama vyengine, kwa hivyo wanachama hao wakaamuwa kutokiunga mkono chama hicho kipya, kwani walijuwa kwamba balaa litakuwa ndilo lile au akhasi ya hivyo. Kwa vile nguvu za utawala wachama hicho bado zilikuwa chini ya ASYL, Jumbe akaharakiza kuungana na TANU ili kuvunja nguvu za ASYL. Kile alichokifanya Jumbe ilikuwa sio kuunganisha TANU na ASP, chama ambacho kilikuwa hakipo tena. Kwa hivyo, bila ya kutanabahi, kile Jumbe alichokiunganisha ilikuwa ni ASYL na TANU, kwani mwishowe viongozi hao hao, yaani wa ASYL, ndio waliyowakilisha Zanzibar katika Kamati Kuu ya CCM, kiini na kinara cha Utawala wa Tanzania. ASYL wakiwa nusuya viongozi katika Kamati hiyo. Wakiwa pamoja na Nyerere na baadhi ya vibaraka wa Bara, ASYL waliweza kuhakikisha kwamba siku zote walikuwa wengi katika kuunga mkono baa na balaa la CCM. Kwa njia hiyo hata waliweza kuibadilisha siasa ya TANU na ya Tanganyika kwa jumla na kuzidi kuzirejesha nyuma Zanzibar na Tanganyika kwa pamoja. Kabla ya hapo, TANU haikuonyesha ishara yoyote ya dhahiri ya kuwa na msingi wa siasa ya kikabila, tofauti na ile siasa iliyofatwa na ASYL. ASLY kwa vile walikuwa hawana sera au siasa yoyote maalum ya kufuata iliwabidi waung'an'ganiye ukabila. Baada ya hapo uongozi wa juu, katika Kamati Kuu ya CCM, ukawa unawakilishwa na siasa mbovu ya ukabila ya ASYL na hatimae CCM ikafilisika na kuanza kutumia siasa dufu ya kudai kwamba Mzanzibari yoyote aliyedai haki za Kizanzibari, haki za kibinaadam na za kidemokrasia alibuniwa kwamba anataka kurejesha utawala wa Sultani na kutaka utawala wa Waarabu urudi. Siasa hii ilionyesha wazi jinsi CCM ilivyokwisha filisika kisiasa na kutaka kung'an'gania katika utawala kwa kutumia kila mbinu, nzuri au ovu. ASYL iliimba wimbo h uo kwa sababu ilikuwa haina mfumo wa kisiasa maalum wa kutatua matatizo ya kisiasa, kiuchumi, kijamii na kitamaduni ya Zanzibar. Kwa hivyo siasa za chuki zilikuwa na madhumuni ya kuwanusisha Wazanzibari kasumba ili walale milele nawasishughulike na ukweli wa mambo ya leo, na kuacha kutafuta sababu zakuwajulisha kwa nini maisha yao yako chini na vipi watayabadilisha. CCM ikaingia katika shangwe la kuitikia wimbo huo na kusahau, kwa makusudi, mambo muhimu sana kuhusu historia ya TANU na historia ya Tanganyika, makhsusan. CCM ilisahau kwamba katika mapambano ya Watanganyika, palipiganiwa haki sawa katika midani tofauti baina ya Watanganyika wa kawaida, ukifananisha na yale matabaka yaliyopendelewa na utawala wa Kiingereza, huko Tanganyika. CCM, mtoto wa TANU, vile vile inasahau kwamba wakati Zanzibar kulikuwa na tabaka la juu la Ukoo wa Kisultan, (watu hawa wakiwa wazalia na raia wa Zanzibar), Tanganyika nako kulikuwa na Koo zilizotukuzwa na kupata manufaa zaidi kupita raia wengine, Koo hizi zilikuwa za Kifalme wa Bara, yaani za Kichifu. Kila mtu anaweza mwenyewe kukisia kwa nini Koo za Kichifu hizo hazijatajwa kama ni Koo za tabakali lomuunga mkono, kumtukuza, kumtumikia na kupendelewa na Mngereza. CCM imesahau vile vile ule ubaguzi uliyofanyika dhidi ya Waislaam wa Kitanganyika katika kila fani na hata kulazimishwa waislaam kubadilisha utu wao "identity" yao, na kubadilisha majina yao ili kuweza kupata elimu ya kwenda maskuli. CCM haijashughulishwa na kubaguliwa kwa Wazanzibari Tanganyika wala kushughulishwa na ubaguzi wa Baraza la Mapinduzi wa wale Wazanzibari ambao ama wanafikra tofauti au asili tofauti, wakati wengi wa hao hao Baraza la Mapinduzi wakiwa na asili za kutoka nje ya Zanzibar. CCM imesahau kwamba kwa mujib wa tafsiri ya kilimwengu ya haki za bidaadam, hata wale walio wengi kuwabaguwa walio wachache ni haramu. CCM inapoleta ubaguzi wa asili visiwani Zanzibar kwa kutarajia kuungwa mkono na wananchi, inafaa ikumbuke kwamba wengi wa wake wa viongozi wa Zanzibar, ni wenye asili za Kiarabu hiyo kuwafanya hata watotowao kuwa wenye asili ya kubaguliwa. Viongozi hao wa ASYL/ASP walipopata vyeo hawakwenda kumuowa Mwanakheri wa Ng'ambo, Chwaka, Mkokotoni au Kizimkazi. Kwa kasumba zao za kubabaishwa na singa na rangi, waliwaona ndugu zao kinyaa na kutafuta masinga, halafu wakitubabaisha sisi kuhusu Waarabu. Viongozi hao wa leo wanaishi kwa anasa, utukufu na kuwa na nguvu zaidi ya huo Usultani wa Kibunsaid wanaotubabaishia.
Mwanzoni Wazanzibari wengi walivyosikiya kwamba ASP (yaani ASYL Zanzibar) itaondoshwa na kuunganishwa na TANU, walipata tamaa na kudhania kwamba hali ya kisiasa Zanzibar itabadilika na kuona bora chama hicho kikorofi cha ASYL kikiondoshwa. Haukupita muda mrefu Wazanzibari wakavunjika moyo kuona kwamba CCM badala ya kufuata siasa njema ya kidemokrasia na iliyoheshimu haki za kibinaadam, ilianza kuongozwa kwa vitisho na utawala wa mabavu ule ule uliyotumika na ASYL, na wengi wa viongozi wake wa Kamati Kuu walikuwa ni walewale waliyoiangamiza Zanzibar.
Kuzalishwa kwa CCM katika mwaka 1977 hakumaanishi kwamba TANU imeungana na chama cha kisiasa Zanzibar, wala kumaanisha kwamba hiyo TANU iliunganishwa na lile tawi lake la Zanzibar la African Association. Kwa hivyo CCM haitokani na muunganisho wa chama cha kisiasa cha Tanganyika na chama cha kisiasa cha Zanzibar, maana Zanzibar kulikuwa hakuna chama cha kisiasa tena. Chama cha ASYL kilikuwa ni chama cha vijana na sio chama cha kisiasa kilichotambulika kuwana sifa na ufuasi wa chama cha kisiasa kilichobainika Zanzibar, kwani hata kabla ya uhuru chama hicho cha vijana kilikuwa na wafuasi wachache sana. Ingawaje kila Mzanzibari anakumbuka namna Makao yao Makuu ya Darajani yalivyokuwayakitisha. Kwa hivyo TANU kwa kweli imejibadilisha jina tu na kujiita CCM bilaya kuwa na sehemu ya chama cha kisiasa kilichowawakilisha Wazanzibari. Kwa hali hii CCM haina uhalali wowote wa kuwakilisha siasa ya Zanzibar. CCM kwa hivyo ni chama cha Bara ambacho hakija tekeleza masharti waliyoyaweka wenyewe, yakwamba "chama lazima kuwakilishwa kote Tanganyika na Zanzibar", na kwa mujibwa mantiki za uchaguzi, chama hicho hakina haki ya kuweka mtetezi yoyote wauchaguzi Zanzibar, na wale wanaojitamba kuwa wana CCM Zanzibar itawabidi amawaende wakasimamie uchaguzi Tanganyika, au waunde chama chao kipya kabisa, kisicho ASP, kwani viongozi wa chama hicho wote ni mahtuti, labda ingelikuwa jambo la maana kama wangeliunda chama kimpya cha ASYL ZANZIBAR. Kutokana na wimbi jipya ulimwenguni la kutokomeza udikteta na kuleta hishma kwa binaadam na kuthamini maisha ya kawaida ya binaadam kwa kuondosha uvunjaji wahaki za kibinaadam na kuanzisha demokrasia; serikali nyingi ulimwenguni zililazimishwa na wafadhila wao kuanzisha siasa ya vyama vingi. Mojawapo katikahizo ilikuwa Tanzania, ambayo ilikuwa na utawala wa chama kimoja. Chama hicho hatimae kilikuwa baadala ya kutizama maslahi ya wananchi, kuyatukuza maisha yabinaadam na kupigania haki sawa za wananchi , kikazidi na kuzidi kufuata siasa yaufidhuli na utumiaji mabavu. Chama hicho kilisahau msingi wake na kusahaukwamba kuna tofauti baina ya "Serikali na Chama", na kwamba chama kwa kawaida kinashughulikia siasa maalum ya chama hicho na jinsi inavyotumia siasa yake kuifaidisha nchi nzima na sio viongozi wake tu, bali wananchi wote hata wale ambao si wanachama wake. Baadala ya kwamba chama hicho kilikuwa kiipe serikali muongozo wa kisiasa, kikaanza kuingilia kati katika kila medani, na chama kujifanya serikali yenyewe, na mara nyingi viongozi wa chama kuingilia mambo wasiyoyaelewa. Hali hiyo ikawafanya na wale watumishi wa serikali wajifanye/ au wafanywe wanasiasa, bila hata ya kuwa na ujuzi au sifa za kisiasa. Kwa njia kama hiyo, ndani ya nchi iliyo filisiwa bila ya kiasi, ama walipata maslahi bora yaki binafsi katika makazi yao, kupata vyeo pasi na kustahiki au kuwafanya wale waliyokuwa na vyeo na madaraka serikalini hatimae kugeuzwa kuwa viongozi wa Chama. Hali hii ilivu- ruga mambo na kuufanya mkono wa kushoto kutojuwa nini mkono wa kulia unafanya na kinyume cha hivyo. Hapo maamuzi ya kiajabu ajabu kupitishwa, na mtu kutojuwa nini siasa ya Chama na nini wadhifa wa serikali na wamtumishi serikalini. Ili mtu aweze kupata- ulwa, hata bila ya kustahiki ilitosha kwa mfano kujipendekeza na kumtukuza Mwenyekiti wa Chama. Yule aliyepiga makelele mengi zaidi, ya kumsifu na kumuenzi Mwenyekiti, ndiye aliyezidi kupewa cheo kikubwa zaidi. Mwenyekiti akalevywa na kutukuzwa huko, na hata kutojali nakutotia maanani uwezo na ujuzi wa mtu akipewa wadhifa fulani, mradi akimtukuza Mwenyekiti. Kwa hali hiyo ikawa Mwenyekiti anazungukwa na watu wa "hewallabwana" bila- ya kuthubutu kumkosoa au kumrekibisha Mwenyekiti. Siasa ya chama chote ikafuata msingi huo huo wa kutoruhusu wala kustahamili urekibishaji wamawazo au utoaji fikra au makosa. Kasumba hiyo ikatambaa serikalini hasa kwa vile wakuu wa maidara/jeshi/polisi wote walikuwa wameshageuzwa wanasiasa. Wakuu hao walijuwa kwamba mradi Chama kilikuwa nyuma yao, wangeliweza kufanya jambo lolote lililowapendeza bila ya kutarajia kurudiwa au kuadhibiwa. Hali ya ulanguzi, wizi na unyang'anyi ikawa inapaliliwa serikalini, na kila kitu kikawa kinahitaji chau chau. Wale waliyoiba na kufanya ulanguzi wakipewa uhamisho au kupewa vyeo vikubwa zaidi sehemu nyengine. Yule aliyekuwa nacho kuzidi kupewa na masikini ya Mungu kuzidi kunyang'anywa. Wanachama wa CCM walikadiriwa kama millioni mbili, wengi wa hawa kutojiunga na chama hicho kwa hiari zao, bali kwa kutizama maslahi yao ya kibinafsi , au kwa kulazimishwa, na hakuna mtu anayeweza kuwalaumu, kwa vile nchi ilikuwa na njaa. Hali kama hii iliwalazimu wanajeshi, polisi na jeshi la usalama wa siri, pamojana wafanya kazi wengi wa serikali na wale wote waliyotegemea ama huduma zachama au za serikali. CCM ilikuwa na maofisi na maafisa mbali mbali bila ya kiasi, wakiwa na vyeo tofauti bila kujulikana hasa kazi na wadhifa wao ni nini. Hali hii pamoja na utumizi wa vifaa na matumizi tofauti kama vile kusafiri ng'ambo kwa sababu za "maji kup- wa na maji kujaa" kumekifanya Chama hicho cha CCM, kiwe na matumizi makubwa mno. Kwa vile CCM ilikuwa haina fedha zake wenyewe, ilibidi fedha hizo izichote kwenye hazina serikalini, fedha ambazo ni za wananchi wote,yaani hata za wale millioni ishirini na tano waliyokuwa si wananchama wa CCM. CCM haikuweza wala kutaka kutafautisha madaraka ya Chama na ya Serikali, kwa hivyo walikuwa wakijitumilia huduma zote za serikali jinsi walivyotaka wenyewe na kwa vile kulikuwa hakuna chama cha upinzani, hakuna aliyeweza kulisaili suala hilo. Yule aliyethubutu kuulizia au kuyakemea mambo kama hayo, ambayo ni hakina halali yake, alijikuta amepumzishwa pahala maalum, kwa usalama wakemwenyewe. CCM hadi leo, kukiwa na mfumo wa vyama vingi, imezoweya mtindo huowa kufanya na kujidhani kuwa wao ni Serikali na Dola, na kufikiri kwamba nchi ni mali ya CCM na hata leo kutoruhusu vyama vya upinzani kutumia huduma za nchisawa na CCM, mfano kufanya mikutano na matayarisho mengine katika heka heka za kampeni na kujitayarisha katika uchaguzi ujao. Kuzuwiya uundaji wa NGO mbalimbali zenye madhumuni ya kukuza maisha ya wananchi wote kwa jumla. Hali hii ni bayana zaidi Zanzibar hasa kwa vile serikali imeshatambua kwamba haina uwezo wa kushinda katika uchaguzi ujao, Zanzibar. CCM Zanzibar, bado ina uzoefu wa kudhani kwamba CCM ndio serikali na ndio yenye uamuzi wa mwisho. Kutoweza kujirek ibisha na kutambua kwamba sasa kuna mfumo wa vyama vingi, na maana yake ni kwamba serikali si mali ya chama fulani bali ya vyama vyote na ya nchi nzima. Kwa desturi kile chama chenye khatamu za utawala kwa muda fulani ni chama chenye dhamana tu ya kuendesha serikali kwa muda na sio kumiliki serikali kwa milele. Hali ya kuvizuiliya vyama vya upinzani ruhusa ya kufanya mikutano au kuwachelewechea haki hizo, kuwanyima kutumia huduma za nchi kama TV na Redio, magazeti huru, ufunguwaji wa matawi n.k. sio khatuwa zitakazowavunja moyo wananchi bali kuzidi kulipamba moto vugu vugu la upinzani. Kwani kama vile kila usiku ukizidi giza, asubuhi hupambazuka, ni sawa na kila ukandamizaji ukizidi, ukombozi kukaribia. Hali ya kukandamiza upinzani hatimae, kwa desturi, inaleta mapambano makali na kuwapa wananchi muamko wa hali ya juu kabisa. Viongozi wa CCM wa Zanzibar inafaa waamke na kutambuwa kwamba hakuna njia yoyote watakayoitumia itakayowafanya washinde katika uchaguzi ujao. Kwa hivyo itakuwa ni jambo la maana kama wakitafuta njia ya kuungana na Wazanzibari wenzao. Vitisho, sabotaji, kuvunja haki za kibinaadam, kupinga wimbila demokrasia, kutumia mabavu, kuufumbi a macho ukweli na kudhani kama haupo, hautawasaidia kitu, bali kuharibu maslahi ya nchi kwa jumla. Wakati umefika kwa Wazanzibari kwa jumla kukaa pamoja na kutafuta maslahi ya nchi na sio ya kibinafsi au ya ubinafsi. Zanzibar ina haja kubwa ya kupiga khatuwa mbele na kuendeleza maisha ya wananchi wake, na haina haja ya NONGWA NA UBINAFSI. Wakati umefika wa Wazanzibari kuunda Baraza jipya la kutunga Sheria mpya na Katiba mpya ya Zanzibar kwa maslahi ya Wazanzibari wote. Mirengo yote ya kisiasa inafaa iwakilishwe katika Baraza hilo la muda litakalokuwa namadhumuni ya kuheshimu haki za kibinaadam na kuje nga misingi mipya ya Kidemokrasia.