ZANZIBAR - USULTANI NA UKOLONI

USULTANI NA UKOLONI

Usultani wa jana na Utawala (Usultani) wa leo

Tabia ya kutawala au ya kunyanganyana utawala au mali, si sifa za Waarabu tu,Waomani au Mabusaidi peke yao. Ulimwenguni kuna tawala tofauti, na tawala hizizinaweza kugawika katika makundi mawili makubwa, moja likiwa na maslahi natabaka la utawala, na kundi la pili likiwa na maslahi halali ya umma mzima nakuwapa watu haki sawa. Sifa ya kuhifadhi maslahi ya takaba la utawala haitegemeiutawala huo una rangi gani, kwani tumeona mifano ya utawala wa Sultan na utawalawa Karume. Utawala usio na maslahi ya umma kwa desturi unakuwa ni wakutumiamabavu na kutowashirikisha wananchi katika uamuzi wa mambo yao wenyewe.Utawala kama huo huchaguwa vibaraka wake kuwatumilia katika kuendelezautawala au mtawala aliyehusika. Serikali nyingi za Kiafrika zilisahau maagizo na ahadi walizozitowa wakati walipokuwa wakipigania uhuru, na kusahau kwamba walichokipigania kilikuwa niserikali ya watu, iliyochaguliwa na watu kwa maslahi ya watu. Karibu serikali zoteza Kiafrika baada ya kupata uhuru zilifuata mtindo wa utawala wa Kidikteta nakusahau ahadi zote walizozitowa kabla ya hapo. Wengine walitumia siasa dhidi yautumwa na kupinga Usultani kama ndio kampeni yao, lakini hatimae, walipopata khatamu za utawala wakaonyesha kuwa ni tawala akhasi za Usultani na ukoloni.Baadhi yao walidai uhuru wa Mwafrika lakini walipopata khatamu za utawala walizidi kumkandamiza Mwafrika, na waliendeleza siasa ya udikteta, utawala wamabavu na kutaka kumtawalia huyo huyo Mwafrika kwa kujigeuza Mabwana/Wakoloni wepya, kama Tanganyika na Zanzibar. Watawala wa Kiafrika wakipata khatamu za utawala wana mtindo wa kutakakuselelea katika utawala milele na hata watakapo kwisha ondoka au kulazimishwa kuondoka bado huwa wanataka kuingilia kati mambo ya utawala, kama vile Nyerere, kupinga aumuzi wa Bunge la Tanganyika la kutaka Bunge na Serikali ya Tanganyika na kuwalazimisha Wazanzibari bila ya khiari zao kubaki katika Muungano kwa kulazimisha serikali moja. Tumemuona Karume, aliyedai siku zanyuma kumpimgania Mwafrika na hatimae tukaona ukatili aliyomfanyia Mwafrika mwenziwe, mtu yule yule ambaye aliyempa yeye nguvu hizo, ndiye hatimaealiyemgeuza adui na kumteketeza. Kwa hivyo suala la kuliangalia kwa makini na kulidurusu kwa kituo ni aina yautawala unohusika, na kama utawala fulani una maslahi na wananchi au la , na siotu kwamba utawala huo una jinsiya gani, ya kutoka Butiama au kwengineko. Kwanihata utawala usio wa kikoloni unaweza kuwa mkatili hata kupitia ukoloni. Suala lakulizingatia ni kama utawala huo ukiwa wa kienyeji unatekeleza maslahi ya umma au maslahi ya watawala na jamaa zao, na hata ukiwa ni utawala wa kienyeji, mradi unakandamiza wananchi lazima up igwe vita mpaka utokomee, na utawala halaliwenye misingi ya kidemokrasia uwekwe badala yake.

Kumiliki Ardhi Zanzibar

Katika historia ya leo kuna madai mawili muhimu kuhusu umilikaji wa ardhi Zanzibar. Dai moja ni la wale wanaodai wamenyangnywa ardhi baada ya Mapinduzi ya 1964, wakidai warejeshewe ardhi zao walizo nyang'anywa, hizo zikiwa ni malizao za kihalali; wanadai . Kwa upande wa pili kuna wale Wazanzibari wanaodaikwamba mababu zao walihamishwa kwa nguvu kutoka zile sehemu zenye ardhi yarutba na kuhamishiwa kwenye sehemu za ardhi duni (Kuna kikundi chengineambacho hakitajwi sana, nacho ni cha wale Wazanzibari ambao ni vitukuu navirembwe wa watumwa waliyotoa jasho lao katika mashamba hayo, bila ya kupatamalipo.) Suala muhimu, katika madai mawili haya, ni jinsi gani kupitisha haki bainaya Wazanzibari bila upendelevu wowote, lakini kabla ya kuweza kufanya hivyo itabidi ijulikane nani MNYANG'ANYA NA NANI MNYANG'NYWA. Hili sio suala rahisi kwa sababu kwa uchache vitendo hivi vya uhodhi wa ardhi vilitokea kamamiaka 160 iliyopita yaani baada ya Seyyid Said kuhamia na kuhamishia mji mkuu wa utawala wake kutoka Oman kuja Zanzibar. Seyyid Said mwenyewe alijigawiya ardhibora kabisa yenye nafaka, na haifikiriki kwamba alimuomba Mhadimu, Mtumbatu,Mshirazi rukhsa ya kuchukuwa ardhi hiyo au kujulikana kwamba ilikuwa ni ardhiisiyotumika kabla ya hapo. Hatujui kwamba Mwiny i Mkuu nae alipochukuwa ardhialiomba au kununua ardhi kwa nani au kwamba ardhi hiyo ilitumika kabla ya hapoau sivyo. Baada ya "Harameli bin Ali" kuleta miche ya karafuu kutoka R'union katika mwakawa 1929 na Seyyid Said kutilia mkazo na kushajiisha upandishaji wa zao hilo muhimu, mfalme huyo aligawa ardhi kwa zile koo za Kiomani zilizotukuzwa na ufalme huo, pamoja na kuwa aila hizo zilikuwa na rasilmali ya kutosha ya kuwezakukuza zao hilo. Ingawaje huko Pemba kati ya makabila muhimu yaliyotia mizizi kabla ya utawala wa Omani kudhibiti Zanzibar, ilikuwa Mazrui na Mauli, namakabila haya yalikuwa yameshajizatit kuoleyan a, kuchanganya damu na kumilikiardhi muda mrefu kabla ya vitendo hivyo kupitika Zanzibar. Itakumbukwa kwambatokea kutolewa kwa Mreno kwa mara ya pili katika 1728 huko Mombasa, mara yakwanza ikiwa mwaka 1660, kabila la Mazrui lilikwisha tia mizizi Momba sa na Pemba pia. Ingawaje hakuna ushahidi unaoonyesha kwamba watu hawa ambao na wao piawaliyokuwa na asili za Kiomani walinunua ardhi hiyo kutoka kwa mtu yeyote katikahizo siku za mwanzo au walizipata kwa sababu za kuingia ndoa. Lakini, vile vile, hakuna ushahidi uliyotolewa unaoonyesha kwamba kulikuwa na watu waliyomiliki ardhi hiyo hapo zamani, waliondoshwa mashambani ama kwa sababu wakiishi sehemu hizi au kuzimiliki. Zanzibar ya kale haikuwa nchi ya ukulima na uchumi wake kutotegemea uuzaji wa mazao ya ukulima na kwa hivyo si suala dhahirikwamba ardhi hiyo ilimilikiwa kwa madhumuni ya ukulima wa biashara. Jambo wazini kwamba ardhi hiyo ilitumika kwa madhumuni ya kujilisha wenyewe, jambo ambalohalikuhitaji sehemu kubwa ya ardhi kutosheleza mahitaji hayo. Zaidi ya hayo idadiya Wazanzibari kwa wakati huo ilikuwa ni ndogo sana hata kutoweza kutumia ardhiyote ama kwa makaazi au kwa ukulima au kwa yote mawili, na ndio maana wakati wautumwa na wa baadae ilibidi kuleta watumwa na vibarua kutoka Bara ku ja kutumikamashambani. Kabla kwa kuja kwa karafuu, uchumi wa Zanzibar ulitegemea zaidibiashara baina ya nchi za Bahari ya Hindi na Afrika ya Mashariki na ya Kati, naZanzibar ndio ikiwa kitovu au kiini cha biashara hiyo, yaani kuwa soko na bandari muhimu, huu ndio uliokuwa msingi wa uchumi wa Zanzibar. Suala muhimu ni, jee ni halali kwa mtu kutoka nchi nyengine na kuja kuikuta ardhi haikaliwi, kuichukwa, kuilimiya na kudai ni yake. Ardhi ya nchi kwa ufupi nirasilmali ya dola kwa jumla na atakayeitumia kwa maslahi ya maisha yake, ya ukoowake na ya nchi kwa jumla atakuwa na haki ya kuitumia akijuwa wazi kwamba hiyoni mali ya umma. Kwa desturi, vizazi vilivyozaliwa katika sehemu fulani kwa karne na karne, ndiwo wanaotambuliwa kuwa wamiliki wa sehemu fulani ya ardhi kwa vilewaliitolea jasho kwa kuifanyi ya kazi sehemu hiyo. Ingawaje kuna wananchi wenginewa Zanzibar ambao hawakuishi sehemu hizo za mashamba, bali waliishi mijini, nakwa desturi huwa hawamiliki ardhi ingawa wana haki sawa ya kumiliki ardhi yanchi yao kwa jumla. Wale wanaosemekana wamenunu wa ardhi, nao siku za mbelehuenda wakawa matatani, ikiwa kutakuwa na up ungufu wa ushahidi kutoka kwawale waliyowauzia ardhi hizo. Watumwa walifanyishwa kazi katika mashamba tofautiZanzibar bila ya kulipwa, ingawa watumwa wengi walirudi makwao mabara baadaya kupata uhuru wao, wale waliyobaki na kuigeuza Zanzibar nchi yao kihalaliwanatakiwa kwa desturi wawe na haki ya kumiliki ardhi katika zile sehemu walizolazimishwa kufanya kazi. Zanzibar ya leo ni Zanzibar yenye raiya (300/Km) kuwa na wakaazi wengi hata ardhi kutotosha kwa wananchi wote kama itagawiwakihalali baina ya wazalendo wote, ikitafsiriwa kwamba ardhi ni rasil mali ya umma. Wabara waliyowasil Zanzibar kwa kazi za vibaruwa mashambani nao wanadai kuwana haki ya kumiliki ardhi kupita wale wazalia wenye asili za Kiomani, wanadai hakihiyo si kwa sababu nyengine zaidi, isipokuwa kuwa wao ni Waafrika na walikuwavibaruwa/maskwatta sehemu hizo. Itaonekana kwamba watu hawa, tofauti nawatumwa, walilipwa kwa jasho lao walilolitowa baada ya kukubaliana kufanya kazi kwa mikataba. Mtumishi karakhanani hamiliki karakhana, ingawa naye hunyonywa.Yupi mwenye haki zaidi ya ardhi ya Zanzibar, yule mwenye uzalia wa Kizanzibaritokea 1660-1728 (kutolewa kwa Mreno) na 1832 au yule jirani aliyekuja kwamkataba wa kibarua makhsusan katika karne ya ishirini. Vijukuu, virembwe navitukuu vya Kizanzibari ambao mabibi na mababu zao walikuwa watumwa waliyofanyishwa kazi katika ardhi fulani ni kati ya watu ambao madai yao ya ardhilazima yatiliwe maanani, suala hili litakapojadiliwa siku za mbele.

Katika kujaribu kuleta usawa baina ya Wazanzibari, Serikali ya Mapinduzi ilitaifisha ardhi na baadae kugawa "eka" tatu tatu kwa wananchi, ingawa nia yalengo hilo ilikuwa ni nzuri lakini ugawaji wenyewe haukuwa wa kihalali. Kwanzasi Wazanzibari tu waliyo pewa ardhi hiyo, pili ugawaji huo haukuwa wa usawa kwaniwale waliyojiweza walizidishiwa, na kupewa (kuchukuwa) mashamba zaidi ya mojana yale yaliyokuwa na rutba zaidi, mfano mzuri ni wa Memba wa Baraza laMapinduzi wenyewe ambao tayari walikuwa na mishahara miwili, wa Baraza laMapinduzi na Bunge la Tanzania. Uhalali wa kitendo hicho umeingia dowa nakupotosha lengo na madhumuni ya ugawaji ardhi kihalali. Zaidi ya hivyo, ardhihiyo iliyogawiwa umekuwa ikiuzwa ovyo ovyo, hivi karibuni hata serikali ya Zanzibar imekuwa inagawa ardhi kwa madhumuni tofauti kwa njia za ama mapendeleo au kwa kilanguzi, kuzidi kuwapa walonacho na kuwanyima wasonacho. Serikali vile vile inasemekana kuwagawiya au kuwakodisha kwa bei za bure wataliana na wageni wengine ardhi ya Wazanzibari, wakati wageni hao wakifanya kejeli, ufudhuli wa kuwafukuza wenyeji sehemu hizo na kuwazuwiya hata kuvua. Wataliana hao waliosabiliwa ardhi hizo, inasemekana wanatumia sehemu hizo kwa uendelezaji wa biashara za madawa ya kulevya. Chau chau gani wanoipata serikali hiyo haijulikani. Kuna watu wengine wanasemekana wamerejeshewa ardhi zao, mali zao na majumba yao, bila ya kutolewa kielezo chochote, wakati wengine bado hawajarejeshewa mali zao. Kutokana na hayo machache kuhusu ardhi, Zanzibar itakapojipatia uhuru wake, kutoka Bara, pata kuwa na haja ya kuunda Mahkama au Tume maalum ya kisheria kulijadili suala la ardhi ya Zanzibar kihalali na kikamili.

Wahindi kudhibiti uchumi

Baada ya kuja kwa utawala wa Kiingereza Zanzibar, Seyyid Said akaonjeshwa shubiri aliyowapa kina Mwinyi Mkuu. Kwanza kwa kukaliwa juu ya kichwa na Mngereza, pili kwa Mngereza kuondosha njia ya uzalishaji mali ya Utumwa ambaoUfalme huo ukiutegemea katika zao lake la karafuu na tatu kwa kutiliwa mkazo kwanjia nyengine ya uzalishaji mali yaani ya kibwanyenye ambayo hatimae ilishajiishakukuwa kwa mfanya biashara, ambae alikuwa Mhindi, wengi wao kuselelea kuwaraiya wa Kiingereza. Hatimae kugeuzwa karibu Mabwanyenye wote waliyokuwa naasili ya Kiomani kuwa kama ni waangalizi tu wa mashamba ambayo kabla waliyamiliki, kwa vile karibu mashamba yote yalikuwa yamewekwa rahhani, baadaya muflis uliyotokana na uuzaji wa watumwa, baada ya hapo Wahindi wakapata satwa ya kuweza kuudhibiti uchumi wa Zanzibar. Kwa hivyo khatamu za utawala na nguvu za uchumi hazijawa tena katika ukoo wa Kibunsaidi na Wale Wazanzibari waliyokuwa na asili ya Kiomani, bali utawala ulikuwa chini ya Mngereza na uchumiwa ndani ya nchi kuwa mikononi mwa Mhindi, wakipeana wadhifa, Mngerezakukamata serikali na uchumi wa nje na Mhindi kukamata uchumi wa ndani, akiwamjumbe wa ubepari bila ya kuwa na njia za uzalishaji mali za kibepari.

Mngereza na mfumo wa matabaka

Kutawalia Zanzibar rasmi na Mngereza (1890), ambaye alikuwa na mgawanyiko wa matabaka ya bayana zaidi kuliko yaliyokuweko Zanzibar wakati huo, kwa hivy oulizidi kuyapanga matabaka Zanzibar kwa utulivu nabayana zaidi. Kwanza kwakuwapa Waarabu, hasa wenye asili ya kiomani, na Wahindi ubora katika matabakaya jamii. Ingawaje katika tabaka la wenye asili ya kiarabu na kihindi kulikuwa na mgawanyiko wa matabaka mbali mbali, yakiwemo matabaka ya chini kabisa katikajamii. Baina ya tabaka la Mabwanyenye/Wafanya biashara wa juu, na matabaka yachini kabisa kulikuwa na tabaka la kati na kati, ambalo lilikuwa na wafanyabiashara wadogo wadogo, maafisa wa serikalini, mafundi waliyojimudu, wakulimana wavuvi waliyomiliki ardhi na vyombo vya kuvulia, na wengine waliyojimudu kwanjia nyenginezo. Katika tabaka hili kulikuwa na makabila ya mchanganyiko.Tabaka la chini likiwa ni vibarua, maskwata na maproletariati "walolala hoi" wengiwa hawa walikuwa ni walalahoi waliyotoka nchi za jirani ambao walivutiwa na hali bora ya kiuchumi ya Zanzibar au walikuwa wakikimbia ulipaji wa "kodi ya kichwa " makwao. Wale waliyokuwa wakijiweza mabara walibaki huko. Mngereza alipojizatit Zanzibar alihakikisha kwamba ugawaji wa matabaka ulizidi kutia mizizi na katika njama zake za kawaida za "kugawa watu ili aweze kuwatawala" kwa urahisi zaidi,alihakikisha matabaka haya yamejengeka kwa msingi wa elimu, kipato, rangi nakikabila .Tabaka la Mngereza mwenyewe bila ya shaka kuwa ni bora kushindayote, na kuwa tabaka la juu kabisa katika jamii hata kushinda la mfalme, na wakatihuo huo kuwatumilia wale waliyokuwa katika matabaka ya juu kuendeleza utawalawa kikoloni. Sababu zinazotokana na mfumo wa utumwa kwa jumla; sababu za kuondoshwa na kupunguzwa hadhi kwa utawala na ubwanyenye wa kishirazi uliyofanywa na SeyyidSaid, na sababu za ujenzi wa matabaka kwa msingi wa kikabila uliyonufaisha ukoloni ambao ulifumwa na Mngereza na kuzaliwa kwa tabaka la walalahoi lilokuwana sehemu kubwa zaidi kutoka bara; zimeleta sio mfumo maalum tu na chuki zakikabila visiwani, bali muhimu ya yote zimeleta Mapinduzi, Muungano na CCM.

Vyama vya kisiasa kabla ya Mapinduzi

Chanzo cha Mapinduzi kinatokana na misingi ya kisiasa na ya kijamii ya Zanzibar.Ili kuweza kufahamu kwa urahisi zaidi matatanisho ya siku za nyuma kwa vijana waleo wa Kizanzibari na baadhi ya Wabara; pana haja yakunakili uundaji, misingi,mifumo na uendeshaji wa vyama vya kisiasa vya zamani hasa Afro Shirazi Party(ASP) na Zanzibar Nationalist Party (ZNP) au Hizbu. Chama cha ASP kiliundwa katika mwaka 1957 kutokana na muunganisho wa chama kile kilichojulikana kama African Association (AA) (ambacho asili yake ilikuwa nikama tawi la TANU na kuwa na uongozi na wafuasi wa Bara) na Shirazi Association(SA) chama chenye uasili wa Kizanzibari. Vyama hivi viwili vilikuwa na sura zakikabila kutokana na misingi iliyowekwa na Mngereza kama ilivyokaririwa hapo juu. Chini ya Uingereza watu waligawiwa kwa makundi ya kikabila na kwa kupitia njiakama hizo ndipo makundi hayo yalipoweza kuwakilisha maslahi ya makundi yaoyaliyohusika. Vikundi viwili hivi, yaani AA na SA, ni vikundi vilivyokuwa namaslahi tofauti yaliyokuwa yakigongana. Shirazi Association ilikuwa ikiwakilishaWaafrika wenye asili ya Kishirazi, waliyokuwa wazalia wa Kizanzibari kwa mababu na mababu. Wakati African Association iliwakilisha Waafrika waliyozaliwa sehemembali mbali za Afrika ya Mashariki na Kati, hasa bara la Nyika/Mrima, kati yaowalikuwemo waliyoishi Zanzibar kwa muda mfupi ilhali wengine walikulia Zanzibarama bado wakiwa na uzi wao wa kitovu Bara au wengine waliyokwisha kuukata uzihuo na kundi jengine likiwa wazalia wa Zanzibar wenye asili ya Bara au kuwa naujamaa na Bara. Suala muhimu la pili liloyagawa makundi hayo lilikuwa ni suala laki tabaka, Washirazi wengi walikuwa Mamwinyi wenye uwezo bora wa kiuchumi, hatawafuasi wao wa chini ni waliyojiweza zaidi. African Association iliwakilisha zaidi watu wa tabaka la chini zaidi, yaani wale waliyokuja Zanzibar kwa kutafuta kaziza muda mfupi kama vile za vibarua, wachukuzi, makuli na wafanya kazi wamashambani (maskwata). Uongozi wa SA vile vile ulikuwa umeelimika zaidi na kwahivyo kuwa tabaka la juu zaidi. Kwa hivyo kulikuwa na mambo mawili muhimuambayo yalivitenganisha vikundi viwili hivi. Vikundi hivi, mwanzoni vilipoundwa,havikuwa na misingi ya kisiasa kama vyama vya kisiasa vya kawaida vinavyojulikana, bali kila kimoja kikijaribu kutetetea uongozi wa kuwakilisha-0Bmaslahi ya jamii yake. Chanzo cha uundaji wa AA, kwa kweli, haikuwa siasa au maslahi ya jamii yote kwa jumla, bali kilianza kama ni chama cha riadha (mpira,ndondi) na hatimae kuanza kujishughulisha na masuala ya kijamii, wakati baadaekikawa tawi la TANU. Ndani ya kila kikundi, kulikuwa na mvutano, na baina yavikundi viwili hivyo kulikuwa na mchuano mkubwa wa kuweza kuingia katika Majlis'ltashrih (LEGCO Legislative council). Muundo wa Legco siku hizo ulikuwa nawawakilishi kwa misingi ya kikabila, kipato na kisomo. Hali hii ilipangwa na Mngereza ili inufaisha mataba fulani na kunyima haki matabaka ya chini. Yalematabaka yaliyonufaishwa kwa kuambatana na uteteaji wa maslahi yao walilindamaslahi yao kwa kuzidi kumt-etea Mngereza na utawala wake. Siasa za kupigania uhuru zilipoanza, Nyerere alijaribu sana kuunganisha AA na SA, hasa kwa vile AA ilikuwa kama ni tawi la Tanganyika African Association,historia hatimae imetushuhudushia lengo la Nyerere la kusisitiza hivyo. Historiaimedhihirisha kwamba Nyerere kwa siku zote alikuwa na lengo la kuimeza Zanzibar na hatimae kuigeuza jimbo. Baada ya jitihada kubwa ya Nyerere AA na SA zikaungana- katika mwaka wa 1957 na kuwa Afro Shirazi Union, yaani umoja wa Waafrika na Washirazi. Ingawaje sio SA yote iliyojiunga na kuwa Afro Shirazi kwani viongozi wa SA wa Pemba waliamua kubaki huru na katika uchaguzi wa mwanzo wa Zanzibar wa 1957, Washirazi wa Pemba, Mohammed Shamte na Ali Sharif Mussa,waligombea uchaguzi huo kama watetezi huru na kushinda kwa kiwango kikubwasana na kuonyesha kwamba tokea siku hizo chama mama cha ASP, ambacho kwawakati huo kikijulikana kama Afro Shirazi Union (ASU), hakikuungwa mkono Pemba. Ndio maana leo serikali ya CCM inawalipizia kisasi Wapemba kwa kuwanyimangazi zote za maendeleo na kuyafanya maisha ya Pemba kuwa ya ufukara wa mwisho. Afro Shirazi Union ikashinda Unguja na kupata viti vitatu kati ya vinnekimoja kuchukuliwa na mjumbe wa Muslim Association na Shirazi Association kushinda viti vyote viwili vya Pemba, Hizbu kutopata hata kiti kimoja. Kina Shamte hatimae wakajiunga na ASP iliyoongozwa na Abeid Amani Karume lakini migongano mikali ilitokea kati ya uwongozi wa chama hicho.

Muamko wa kudai uhuru

Kumalizika kwa vita vya pili vya ulimwengu, kulileta muamko mpya katika makoloni mbali mbali, kwanza kwa kushindwa kwa Mafashisti wa Kijerumani, Kijapani naKitaliana, pili makoloni yaliyokuwa chini ya Wakoloni kama vile wa Kiingereza walianza kuwa na muamko mpya. Nchi kama za India na Uchina kujinyakulia Uhuruwao katika miaka ya 1947 na 1949. Baadae hamasa za upiganiaji uhuru na zakimapinduzi za nchi za Arabuni ambazo zilikuwa za kiislaam, pamoja na kwamba Mngereza (1949) aliwapa Majahudi nchi ya Mapalastina ambao wengi wao walikuwani waislaam, zilifanya muamko wa Wazanzibari dhidi ya Mngereza kuzidi kutia fora.Mapinduzi ya Jamal Abdil Nasser (1952) na vita vya Mchirizi wa Suez vya Misri (1954) dhidi ya Mngereza, Mfaransa na Jahudi vilifanya jazba na damu yaWazanzibari kuzidi kuchemka na kuleta muamko wa kupigania uhuru na kujitegemea. Mapambano ya Nkurumah, ya Ben Bella, ya Mau Mau na wengineo yalizidi kurekibisha gurudumu la mapambano ya Wazanzibari. Mchemko wavuguvugu la Misri uliwafanya wale wanafunzi wa Kizanzibari waliyokuwa wakisomahuko na wataalam wengine wa Kizanzibari kuchukuwa msimamo madhubuti dhidi yaUtawala wa Kiingereza. Kati ya wale waliyokumbwa na muamko huo ilikuwa ni Arab Association ya Zanzibar na kufika hadi katika mwaka wa 1954 kugomea kwendamajlisi 'l tasrih, mmoja kati ya viongozi wake washupavu alikuwa Ali Muhsin. Jinsihamasa za uhuru na azma ya ku-jitawala zilivyokuwa ziko hali ya juu na hamu yakutaka kumuondoa Mngereza ilivyokuwa kubwa, mmoja wa wanachama wa ZA, Inspector Sultan Ahmed Mugheri, alipovunja mgomo huo na kuhudhuria kikao cha Legco, alipigwa visu na kuuwawa. Mtu aliyejitolea kumuuwa Sultan Ahmed alikuwasi mwengine, bali ni baba yake Lt. Humud Mohammed, yaani Mohammed Humud. Katika mwaka 1951 Wangereza walitaka kuanzisha kuchanjwa n'gombe Zanzibar,lakini jinsi ya hamasa zilivyokuwa ziko juu dhidi ya Mngereza kati ya wazalia wa Zanzibar, jambo lolote lile alilolitaka Mngereza kulifanya lilitiliwa shaka, hasa kwavile tokea 1940 Mngereza alianza kuchukuwa ardhi ya wakulima wa Kiembe Samakikujengea uwanja wa ndege. Hali hii ilizidi kutia fora baina 1949 na 1951 wakatiWangereza walipochukuwa ardhi iliyokuwa na Msikiti kwa madhumuni ya ujenzi.Kwa hivyo watu walivyoambiwa n'gombe wao wachanjwe, waligoma na kuonakwamba Wangereza walitaka kuwaulia n'gombe wao, kama ng'ombe wao walivyokufakufa Zanzibar baada ya kukogeshwa katika madawa siku za kabla ya hapo, kwahivyo wakakataa. Badala ya kutumia siasa, Mngereza akatumia kibri chake chakikoloni na kutumia nguvu na mabavu kwa kuanza kutia viongozi wa wafugajin'gombe hao ndani na kuwapandisha Mahkamani. Jambo hilo liliwakasirisha sanawazalia na kusababisha mgomo na mhadhara uliyoelekea gerezani "kiinuwa miguu"na kuwatowa viongozi wao kwa nguvu. Mngereza kwa mara nyengine tenaakaonyesha kibri chake cha kutumia nguvu na kupiga watu risasi, hapo ndipovi kazuka "Vita vya N'gombe". Tukio hilo ni tukio muhimu sana katika sera za kisiasa za Zanzibar, kwani hapo ndipo gurudumu la kihistoria la kuleta mabadiliko na vuguvugu la kuleta uhuru lilipozidi kupata nguvu. Vita hivyo vya N'gombeviliwaunganisha Wazanzibari wa matabaka mbali mbali na kuondosha yale mabomaya Mngereza ya kubaguwa watu kwa makabila. Chanzo cha mgomo wa kupingauchanjwaji wa n'gombe ulianza Kiembe Samaki, na watu wa huko wakiungwa mkonona mashamba mbali mbali wakaunda chama na kukiita Hizbu 'l Watan Raiyat Sultani,na baadhi ya viongozi wao walikuwa ni Vuai kiteweo, Miraaj Shaalab, Maalim Zaid,Haji Hussein n.k. Mngereza kwa kutumia nguvu za kisilaha, nguvu za gereza nanguvu za mahkama zao waliukandamiza mdhahara huo na viongozi hao. Hatimae Mngereza alishinda kijeshi lakini hakutanabahi kwamba alijichimbia kaburi lakisiasa na kupigwa pigo lisotibika. Kumbukumbu hilo likawafanya viongozi waHizbu, ambao chanzo chao kilikuwa Kiembe Samaki, na waliyokuwa hawana asili yakiarabu, kuchukuwa khatuwa muhimu katika historia ya Zanzibar. Kwa vileviongozi hawa walikuwa hawana elimu ya kizungu waliuendea uongozi wa ArabAssociation uwasaidie katika mapambano yao na Mngereza. Matekeo yake yakawavyama hivyo viwili kuungana na kufanya chama kimoja kilichojulikana kama Hizbu'l Watan au kilojulikana kwa jina la kiingereza Zanzibar Nationalist Party (ZNP).Wakati vuguvugu la kusonga mbele na kudai uhuru katika bara la Afrika lilikuwakatika kiwango cha hali ya juu kabisa. Majina na mifano ya viongozi kama kinaKwame Nkurumah, Patrice Lumumba, Sokou Toure, Jamal Abdel Nasser, ModiboKeita, Ben Bella, Didan Kimathi, Jomo Kenyatta n.k. yalikuwa ni majina yakusisimua, ya kimapinduzi na ya kujivunia kwa kila Mzanzibari na kwa Bara zimala Afrika. Viongo zi hawa waliichemuwa Afrika nzima na kuwaamsha Waafrika wotekupigania Uhuru wao.

Upiganiaji Uhuru

Kama ilivyotajwa hapo juu ZNP ilishindwa na ASU (ASP) katika uchaguzi wa 1957, lakini baadae mabadiliko makubwa ya kisiasa yalitokea. Viongozi vijana waKizanzibari waliyokuwa Uingereza walishauriwa na uongozi wa ZNP kurudi nyumbani kwa madhu-muni ya kushiriki katika kuanzisha upangaji wa mikakati wakuongoza mapambano ya kisiasa na vuguvugu la uhuru. Viongozi hawa walikuwana umoja wao huko Uingereza na kati yao walikuwa A. M. Babu, Khamis AbdullaAmeir, Ali Sultan Issa n.k. Viongozi hawa waliamuwa kumpeleka Babu Zanzibar kutoka Uingereza kwa madhumuni ya kuchunguza hali ya mambo na alitakiwaaepuke kujiunga na kundi lolote baina ya ASP na ZNP. Ingawaje, Babu alipofika Zanzibar hatimae akajiunga na ZNP. Wenzake walipomsaili kuhusu kisa cha kuamuakujiunga na upande mmoja, akawajibu kwamba kwa wakati huo ZNP ndio iliyokuwa ikifuata siasa ya kimaendeleo na kwamba ASP ilikuwa bado inapinga uhuru na kudai kwamba Mngereza asiondoke mpaka Waafrika wa Zanzibar wasome ("It is quite true that the African Association of Zanzibar and Pemba does not favourthe proposed Round Table Conference. As we are the backward community in theseislands, we shall ever beg our needs and claim our rights for the benefit of Africans in this Protectorate for it is the adopted policy of AfricanAssociation to achieve advancement and endeavour to win rights for our selvesso long as we are sons and dauhgters of the soil. So our immigrant friendsshould not forget that our aim is African self government,....not Zanzibari self-government - May 5, 1955 - Rankie Constitutional proposals). Hicho ndichokilikuwa kiini cha msingi wa chama hicho baadae. Sumu hiyo ya kutodai uhuru kwa ASP ilitiwa na vibaraka wakiingereza waliyopenyeza katika uongozi wa ASP. Inagawa ASP ilidai kuchelewesha uhuru hadi Waafrika wasome, baada ya Mapinduzi kati ya watu wa mwanzo kuuliwa na serikali ya Mapinduzi walikuwa wale wale viongozi wa Kiafrika waliosoma na serikali kuendeshwa na wale wasiosoma. Hatimae viongozi wengine wa Kizanzibari wakawasili Zanzibar kutoka Uingereza na shamra shamra na muamko wa kuendesha kampeni ukazidi kutia fora na kabla ya miaka mitatu kupita vizuri, ZNP ikaweza kuchuwana na ASP katika uchaguzi nakuweza kwenda karibu sare na ASP katika chaguzi za 1961. Kwa wakati huo ZNP ndio iliyokuwa chem chem ya hamasa za upiganiaji uhuru wakati ASP ilitumia siasa ya "Ugozi na Zuwiya", yaani Ugozi wa rangi nyeusi nazuwiya Uhuru mpaka gozi asome. Kwa upande mmoja chama cha ASP kiliaibisha Zanzibar, hasa wakati kulipokuwa na mikutano mikubwa ya nchi za Kiafrika, kama vile PAFMEC kwani msimamo wa ASP katika mikutano hiyo ulikuwa ule ule waUgozi na Zuwiya uhuru hadi Waafrika wasome na ndio maana walikataa kuwaungamkono Hizbu katika kudai Uhuru. Suala hili lilileta aibu hata kufanya viongozikama kina Nkurumah na Kanyama Chiume kuingilia kati na kuwalazimisha ASPkujiunga katika mapambano ya kudai uhuru, na hatimae kusababishwa kuundwa "kamati ya uhuru" ya ASP na Hizbu katika mwaka 1958. Katika mikutanoiliofanyika PAFMECA, Mwanza 1958 na All African People's Conference, 1959 Accra na Zanzibar, ujumbe wa ASP, ulikuwa na wahka kwa sababu katika uongozi wake tokea hapo nyuma kulikuwa na mgawanyiko baina ya Wa shirazi na Waafro, na katiya Wa Afro kulikuwa wale wazalia hasa wa mashamba na "malumpa" "walala hoi" na ambao wengi wao walikuwa si wenye asili ya Kizanzibari, na kulikuwa na kikundicha wasomi. ASP mwanzoni walikataa kubadilisha siasa yao ya kuchelewesha uhuruna kukataa kutotumia ubaguzi wa rangi kama ni msingi wa siasa yake, ingawajebaada ya kulazimishwa na PAFMECA walikubali kufanya hivyo. ASP waliogopakusimama katika jukwaa la kudai uhuru pamoja na ZNP kwa sababu waliogopakwamba suala hili lingeliondosha msingi wa siasa na kampeni yao ya kudai kwamba Hizbu ni chama cha Waraabu, ingawa Hizbu walikuwa wote ni Wakizanzibari kwa auzalia. Nyerere kwa kisiri siri akazidi kupalilia moto kwa kutia sumu ya kusema kwamba maingiliano ya Wazanzibari bado yalikuwa kama baina ya " Mabwana nawengine Watumwa". Ingawaje ASP ikadai katika PAFMECA kwamba, iko tayari kuiunga mkono Hizbu katika kupigania uhuru na kuwacha ukabila mradi Hizbu nayo ingeli ahidi kwamba pindi likitoka pande na kujigawa katoka ASP, hawataliunga mkono wala kuungana nalo. Hizbu nao wakakubali masharti hayo kwamba hakuna upande wowote ule utaounga mkono kundi lolote litalojitenga kutoka katika chama kimoja wapo. Kwa kipindi fulani vyama vyote hivyo viwili vikawa vianapigania uhuru bega kwa bega kwa hamasa za pamoja na kitaifa, hata kupanda majukwaa ya mikutano kwapamoja. Kutokana na mvutano ambao kwa kimsingi ni wakitabaka na vile vile wenyemuelekeo wa uasilia katika mwisho wa mwaka wa 1959, mvutano huo ulisababishakugawika kwa ASP na kundi lenye mrengo wa kibwanyenye na kujitambua kamaWashirazi walitoka chama cha ASP na kuunda chama cha Zanzibar and PembaPeople's Party (ZPPP). Kwa upande wa Hibzu nako kulikuwa na mirengo mitatu,mrengo wa kushoto ambao ulikuwa kina A. M. Babu, Ahmed Badawi Qullatein, Ali Sultani, Abdulrazak Mussa Sima, Miraji Mpatani, Abdulaziz Ali, Mzee wa Tarekh Muhsin Abeid, Amar Salim Kuku, Salim Ahnmed Salim n.k.; mrengo wa kulia wa kina Juma Alley na wafadhila wa Wangereza waliyowacha kazi za serikali dakika zamwisho na kuingia katika siasa, uhuru ulipokuwa unakaribia, kama vile MohammedSalum Jinja, wengine wa mrengo wa kulia ambao ndio waliyopalilia siasa ya chuki katika ZNP na kufuata mrengo wa kulia na kuzidi kuleta mifarakano ya kisiasa baadala ya majadiliano na hatimae kutoka kwa Umma Party, ni Ahmed Lemky,Amani Thani na Suleiman Malik. Kundi la kati na kati la ZNP lilikuwa ni akina Dk. Baalawi, Maulidi Mshangama, Amour Zahor, Haji Hussein, Rashid Hamadi, Miraaj Shaalab, Vuai Kiteweo, maalim Zaid na maalim Mandoa. Itaonekana kwamba hatakatika Kamati Kuu ya Hizbu nako kulikuwa na mvutano mkubwa sana lakinimvutano huu ulikuwa zaidi baina ya waliyoendelea wa mrengo wa kushoto na waselelea wa mrengo wa kulia. Kiongozi wa Hizbu alikuwa Ali Muhsin na kwa sikuza mwanzo alikuwa ni kiongozi mshupavu wa kujitolea kupigania uhuru wa Zanzibar. Vuai Kitoweo alikuwa Rais wa Hizbu na Katibu Mkuu kuwa A. M. Babu. Kiongozi wa ASP alikuwa ni Abeid Amani Karume, ambae alikulia Zanzibar, lak- ini Othman Sharif, msomi mmoja wapo katika ASP pamoja na Abdulla Kassim Hanga, Hasnu Makame, Aboud Jumbe, Abdulaziz Twala walitarajiwa hatimae kuchukwa uongozi kutoka kwa Karume, na Karume aliwaona hawa kama ni wasaliti waliyojitayarisha kumpokonya n ofu lake la uongozi. Fungu lililomuunga mkono Karume dhidi ya wasomi wa ASP walikuwa ni Afro Shirazi Youth League. ZPPP ilipoundwa mrengo wa kulia wa Hizbu haukusita kunyakuwa nafasi yakuwaunga mkono na kutarajia kupunguwa nguvu kwa ASP kinyume na ahadi walizozitowa katika PAFMECA, Accra, ya kutoliunga mkono pande lolote litakalojigawa. Wakati huo, Hizbu ilipoungana na ZPPP, Babu alikuwa safarini na aliporudi akakabiliwa na Karume na kusutwa kwa maneno kama haya, "jee unaona tulisemaje sisi, unaona si wamewaunga mkono?" Babu anadai kwamba alijaribu kusema na uongozi wa Hizbu, kwamba wamevunja ahadi za Mkutano wa Accra bila ya kusikilizwa. Zaidi ya hayo kwa upande wa Hizbu wa mrengo wa kulia walipata turufu mpya ya kuwapiga vita kina Babu kwa kupata msaada wa mrengo wa kulia wa ZPPP. Kuundwa kwa ZPPP na kuongezwa katika uongozi wa Hizbu kwa baadhiya vibaraka kama kina Amani Thani kwa bahati mbaya kulimbadilisha msimamo na muelekeo wa Ali Muhsin na kumfanya kuelemea zaidi mrengo wa kulia hata hatimae akishirikiana na Mngereza kumtia Katibu Mkuu wa ZNP A. M. Babu ndani, akiwa kiongozi pekee chini ya ukoloni wakati wa serikali ya ndani, kuhukumiwa na kufungwa kwa sababu za kisiasa. Njama za makusudi za kumfunga Babu zilipunguza kasi ya mrengo wa kushoto na wakati katika uongozi wa Hizbu, namara tu alipofunguliwa Babu mrengo wa kushoto ukadai watoke katika chamahicho. Babu akajaribu kuwazuia wenzake kudai kwamba lazima wapambane navibaraka hao wakiwa ndani ya chama, na hapo tu ndipo wangeliweza kuleta makubaliano ya kitaifa kwa maslahi ya Wazanzibari wote bila ya kujali ufuasi wa chama. Upinzani ulikuwa mkubwa na katika mkutano wa kupendekeza na kupanga watetezi wa uchaguzi wa 1963 kundi la mrengo wa kushoto la ZNP likadai kwamba chama cha ZNP lazima kichukuwe msimamo wa kitaifa na kuwacha mtindo zorota wakusimamisha watetezi wa uchaguzi kwa mujib wa rangi au kabila. Yaani Babu alidai, Ali Muhsin si lazima asimamishwe jimbo la Malindi na Abdulrasul Alarakiya jimbo la Shangani. Babu alipendekeza Abdulrazak Mussa Simai asimamishwe jimbola Malindi (Forodhani) na Ali Muhsin asimamishwe jimbo jengine lolote la uhakika, ili kuwathibitishia Wazanzibari kwamba msingi wa siasa ya Hizbu haukuwa wa kikabila. Na kuweka wazi kwamba kile ilichotaka Hizbu ni kuleta usawa kwa Wazanzibari wote kwa jumla. Wale waliyokuwa na kasumba za mrengo wa kulia wakapinga mapendekezo hayo na hatimae mrengo wa kushoto ukaamuwa kutokubali kufuata siasa hiyo ya kibaguzi na kujitowa katika Hizbu na Julai, mwaka 1963, kikaundwa chama cha Umma Party na Babu akawa ni Rais wake. Kufuatilia uchaguzi wa 1957 palifanyika uchaguzi mara ya tatu, katika mwaka 1961,mwezi wa Januari, matokeo yalikuwa ASP ilipata viti 10, ZNP viti 9 na ZPPP viti 3. Katika mwaka 1961, mwezi wa Juni ASP ilipata viti 10 na ZNP kupata viti 10 na ZPPP viti 3. Katika uchaguzi huu kulitokea ghasiya na maisha ya watu kupotezwa bure na wengi katika hao waliyoshiriki katika ghasia hizi walikuwa ni watu waliyokuwa na asili ya Bara. Katika uchaguzi huo mbinu mbali mbali za kuwezesha kushinda zilitumika sehemu zote mbili. Njia mojawapo ZNP iliyotumia ilikuwa ni kutumia kura za ZPPP pale ambapo wasingelishinda, kuhamisha wapigaji kura kutoka zile sehemu waliyokuwa na uhakika watashinda na kupeleka zile sehemu waliyokuwa na wasi wasi wa kushinda. Utafiti na uchunguzi wa makini na wautulivu ulifanywa na ZNP na kuweza kujua hesabu ya kila mpigaji kura hadikuweza kujua tofauti ya kura moja. Katika uchaguzi wa mwaka 1963, mwezi wa Julai ASP ilipata viti 13, ZNP viti 12 na ZPPP viti 6 na kwa hivyo ZNP na ZPPP wakaunda serikali. ASP nao walitumia mbinu zao katika kujitayarisha na uchaguzi lakini mipango na njama zao zilikuwa koroma kwa vile wao walipigania wingi waidadi ya kura na sio wingi wa ustadi wa upigaji kura. Ahmed Hassan Diria (mmoja kati ya waliyowauza na kina Hanga na kuwanyanganya mali Wapemba) na Ali Mwinyi Tambwe, huyu akiwa wa Tanganyika, walishughulika sana katika siku za uchaguzi kuleta Watanganyika kutoka Bara na kuja kupiga kura Zanzibar. Tatizo lao katika njama zao ilikuwa kwanza wametumia wageni na kwa vile hawa ilikuwa ni wageni walipelekwa zile sehemu ambazo zikiunga mkono ASP na kwa hivyo watu wa sehemu hizo hawakulalamika kwa vile hawa wageni walikuja kuwasaidia wao. Kwa njia hiyo ASP ilizidisha idadi ya watu katika zile sehemu ambazo walikuwa tokea hapo lazima washinde. Vile vile ghasia za Juni (ati leo tunaambiwa zilikuwa majaribio ya mapinduzi, yaani kumpindua mgereza kwa magongo) zilikuwa na madhumuni yakuleta vurugu ili watu wasishughulishwe na kuangalia wageni waliyokuja kupiga kura na vile vile kutisha watu wasiende kupiga kura hasa zile sehemu ambazo ASP ilikuwa na wafuasi wengi. Kitu kilicho wafaidisha ASP ni baada ya kuhisabiwa kura hizo kudai kwamba wao ingawa walikuwa na kura nyingi zaidi na hata hivyo walishindwa. Dai hili halikuwa na tija yoyote, kwani mbinu walizozitumia zilikuwa mbaya. Ushindi ulitegemea idadi ya viti na sio idadi ya voti; pindi ASP ingelitumia maarifa mengine labda ingelifanikiwa zaidi, na leo tungelikuwa tunasoma historia nyengine kabisa.

Umma Party haikushiriki katika uchaguzi wa 1963, na mara tu baada ya kujitoa katika ZNP ilianzisha maingiliano ya kitaifa ya waandishi wa magazeti mbali mbali, vyama vya wafanya kazi na kuungana na wale viongozi waliyoendelea wa ASP. Wakati huo Hizbu ilishajiisha chuki kubwa sana dhidi ya Umma Party na hata kuwalazimisha viongozi hao kuzihama zile sehemu walizoishi Mahizbu wengi, kwakuwafanyia kila kashfa na chuki za kipuuzi viongozi hao wakalazimishwa kuhamia Miti Ulaya. Hii ilikuwa si siasa bali ni upuuzi wa kisiasa. Kushirikiana kwa Umma Party na vikundi tofauti vya kipinzani kuliwafanya viongozi washupavu, waliyoendelea na wa mrengo wa kushoto wa ASP kama vile Hanga, Khamis Masoud, Twala, Saleh Sadalla n.k. kupata nguvu zaidi ndani ya ASP. Kuundwa na kushiriki kwa ZPPP katika makubaliano ya mbinu za uchaguzi katika uchaguzi wa 1963 kulirahisisha kushinda uchaguzi huo kwa urahisi zaidi, na hatimae ZNP na ZPPP kuunda serikali. Serikali hiyo ambayo ilikuwa na Waziri Mkuu Mohammed Shamte na Kiongozi wa serikali Ali Muhsin mara ilisahau wapi ilitoka nakuanza kutumia mbinu mbaya za kisiasa za kutumia mabavu ambayo hata Mngereza hakuyatumia. Kitendo chao cha mwanzo cha kidikteta kilikuwa ni kupitisha sheria ya kufungia chama cha Umma Party, khatua iliyo kwenda kinyume na misingi ya demokrasia. Umma Party, kwa wakati huo, kilikuwa kikijaribu kuunganisha Wazanzibari wote kwa jumla. Kwa bahati mbaya Serikali ya Hizbu iliingiwa na wasiwasi mkubwa na vuguvugu la kitaifa lililokuwa likizidi kupata nguvu, na serikali hiyo ikafikiria zaidi maslahi ya serikali yake kuliko ya nchi nzima. Kama ilivyofichuliwa baadae serikali hiyo ilikwisha tayarisha nyaraka za kutiwa ndani kwa viongozi mbali mbali wa Umma Party na ASP, lakini kwa bahati watu hao walipata fununu na kukimbia nchi, Babu kukimbilia Dar es salaam. Serikali hiyo, ikapitisha sheria nyengine kinyume na demokrasia, nayo ilikuwa kulifungia ruhu- sa yauchapishaji gazeti mashuhuri la ZANEWS ambalo ndilo lililokuwa gazeti la maendeleo la kifani lisilo kuwa na upuuzi wa chuki za kikabila na siasa ya kupendelea matabaka ya kikandamizaji. Vitabu vingi vilikamatwa na kuchukuliwa na serikali, kuzuilia watu haki ya kidemokrasia ya kuwa na uhuru wa kusoma. Mambo yote hayo yalikuwa yakiruhusiwa hata chini ya utawala wa Ukoloni wa Kiingereza. ZNP ilikiogopa chama cha Umma Party kwa sababu, chama hicho kilikuwa kikiungwa mkono zaidi na vijana wengi sana na wale waliyokuwa na siasa ya kishupavu.

Umma Party

Chama cha Umma Party kama ilivyonakiliwa hapo juu kiliundwa kutokana na mchuano wa kujaribu kuhifadhi misingi ya kijananchi ya usawa na umoja baina yaWazanzibari, kupigania uhuru wa kweli na sio kivuli cha uhuru kilichomficha mwenye khatamu za kweli za utawala, yaani uhuru wa bandia. Mwanzoni suala lakupigania uhuru wa kweli lilikuwa ni lengo halisi la kuundwa kwa Hizbu, chama ambacho kilizalika na vuguvugu la kihamasa la Ujananchi wa kugomea Majlis `ltashrih na "vita vya n'gombe" vilivyo ongozwa na akina Vuai Kiteweo. Historia ya Hizbu inadhihirisha wazi kwamba chanzo cha mapambano ya chama hicho kilikuwani ya kimaendeleo, kama "vita vya n'gombe" vilivyothibitisha, msimamo wa chama hicho ukaendelea kuwa na nidhamu ya kupigiwa mfano wa kupinga kutawaliwa,kudai uhuru bila masharti yoyote, kupigania utawala uliyowekwa na watu wenyewe, kuendeshwa na watu wenyewe na kwa maslahi ya watu wenyewe, na kuunga mkono upiganiaji uhuru na ukombozi wa nchi zote zilizokandamizwa nakuwa dhidi ya ukoloni na ubeberu. Kutokana na siasa shupavu chama hicho kikaweza kwa muda mfupi tu kugeuza kushindwa kabisa katika uchaguzi wa 1957na kuwa na nguvu za kupata viti karibu sawa na chama cha ASP katika uchaguziwa Januari na Juni 1961. Siku hizo Hizbu ililitukuzisha jina la Zanzibar katika vikao na mikutano mbali mbali ya kupigania haki za waliyoonewa ulimwenguni kote. Kuunga mkono vuguvugu la kugombania uhuru wa bara la Afrika na kupinga vikali udhalimu waliyofanyiwa Waafrika mbali mbali kama vile kukamatwa, kuteswa nahatimae kuuwawa kwa mpiganiaji uhuru mashuhuri na mshupavu Patrice Lumumba. Baadhi ya viongozi wa Hizbu walipoanza kuona uwezekano wa kupata khatamu ukokaribu wakaanza kubadilika na wengine nyuso zao za kikweli zikaanza kudhihiri.Wale viongozi washupavu waliyompinga Mngereza kinaga ubaga na kupinga siasaya kibaguzi wakaanza kupikiwa majungu na kuwekewa vikwazo vya aina mbalimbali. Kutokana na mbinu kama hizo ndipo Katibu Mkuu wa ZNP, Babu, akabuniwa kesi na kufungwa na serikali ya ndani ya chama ambacho alikuwa ni katibu wake. Hii ilikuwa ni mbinu ya kumuondosha njiani ili kurahisisha kupitishwa kwa mamboambayo yeye angeliyapinga. Wakati huo ndipo vitimba kwiri waliyokuwa hawana ujuzi au uwezo wa kisiasa navibaraka wa kiiengereza walipozidi kupenyezwa katika uongozi wa ZNP hasa wale waliyokuwa wakifanya kazi serikalini chini ya Mngereza. Walipoingiya katikauongozi vitimba kwiri na vibaraka hivyo vikapewa nyadhifa za juu na kutapakaza kasumba zao na kutia sumu na ubaguzi katika chama ambacho sifa zake zilikuwa ni za kifani kabla ya hapo. Wakati bahari ilipokuwa chafu na mawimbi kuwa makali, waungwana hao walificha kucha zao na kungoja ufukweni, lakini kazi ngumu ilipomalizika na bahari kuwashuwari wakaanza kujipenyeza katika uongozi, wengine kupewa nyadhifa wasizozimudu na kumtumikia Mkoloni ama kwa kujua au kwa kutotambua. Hali hii iliaibisha sana kwa kuitia ZNP doa na baka pale ambapo nuru ikin'gara. Nguvu za mrengo wa kushoto na wa kati wa ZNP zikazidi kupunguwa na kufifia na vitimbakwiri na vibaraka wakazidi kukaza kamba huku wakiiangamiza Zanzibar. Wakati A. M. Babu alipomaliza kifungo chake na kutoka gerezani dosari lilikuwa ni kubwa mno bila ya kuweza kutengezeka. Ingawa walijaribu kuirejesha ZNP katika mkondo wake wa kijananchi, wa kimaendeleo na wakimapinduzi, haikuwezekana tena kwa vile athari iliyofanywa na kina Amani Thani ilikwisha tendeka na kupitia mpaka.Waliyotoka serikalini kwa Mngereza walitoka pamoja na kasumba zao bila ya kuweza kujirekibisha na kuwa na fikra zile zile za kitabaka na kibaguzi kama walivyotiwasumu, vipi wafikiri. Ingawa hawa walikuwa ni Wazanzibari wa kizalia, lakini kwa vile walikuwa karne za nyuma na asili ya kiarabu na kuwa wasomi, wakatafsiriwa na wale waliyokuwa na upungufu na upeo wa kisiasa, wakafanywa kama ni kisingizio cha kuwadanganya makabwela kuwa ni watu waliyotaka kuleta utawala wa kiarabu na wa wasomi. Wanasiasa waliyokuwa wenye fikra za kikasumba walikuwa ndani ya vyama vyote, hata na wale waliyojiita Waafrika. Ubovu wao ulitokana na fikra zao na sio namna ya sura, rangi au makabila yao au kwamba walikuwa wasomi au pangu pakavu. Kwa wakati huo Bara la Afrika zima pamoja naZanzibar lilikuwa na wataalam wa hali ya juu bila ya kuwa na asili ya Uarabu, naingawa Waafrika wa asili na jadi walikuwa na elimu ya juu kabisa haikuwafanya wote kuwa na fikra za kisiasa madhubuti na za kimaendeleo, kwani kati yao kulikuwa na waliyokuwa na kasumba ya hali ya juu kabisa. Ujuzi wa kisiasa una miko yake nasio kila mtu anaweza kuwanayo. ZNP kuegemea viongozi waliyokuwa na upungufuwa sifa za kisiasa na kuwa na sifa nyengine tofauti za kibwanyenye ilikuwa nimakosa ambayo yaliirejesha Zanzibar nyuma sana. Wale waliyotumia siasa yaukabila walifanya hivyo kwa sababu ya ukosefu wa mfumo wa siasa maalum yaku tatua matatizo ya nchi kisiasa. Wakati wa kabla ya uhuru kupatikana, ulikuwa ni wakati muhimu sana katika historia ya Zanzibar, kwani ilikuwa ni wakati huo ambapo hali ya juu kabisa yakisiasa ilikuwa itumike kwa manufaa ya watu wote. Huo ulikuwa sio wakati ambapovyama vya kisiasa vili kuwa vipapatikie ullwa na khatam za serikali. Huo ulikuwani wakati wa vyama tofauti vya kisiasa kuungana na kuyalinda na kuyachungamaslahi ya Zanzibar na sio vuta n'kuvute. Wale wenye akili za mchwa za kuila nyumba wakayo walitumilia hali hiyo ya ubina fsi na kuzidi kutia chuki baina yaWazanzibari, chuki ambazo kwa desturi ni fikra za wale watu ambao hawana kinaau upeo wa ufahamivu wa kisiasa, watu wa aina hii walikuwako katika vyama vyoteviwili vikubwa vya kisiasa . Mwenye ujuzi wa kisiasa hutumia ho ja za kisiasa na sioza kikabila, kwani siku zote kiini bora cha kisiasa huwa kinaambatana na sababuza kimsingi nazo ni kukomesha sababu ambazo hujengeka kwa ubaguzi wakitabaka.

Zanzibar kama tausi

Kabla kuundwa kwa Umma Party, wale viongozi wa ZNP waliyokuwa na mrengo wa kimaendeleo walijaribu kuunganisha Wazanzibari wa vyama mbali mbali, kuondosha ubaguzi wa aina mbali mbali katika ZNP. Mapambano ndani ya ZNP yalikuwa nimagumu na kama ilivyoelezwa huko nyuma wengi wa mrengo wa kushoto walitakakujitoa katika chama hicho lakini A.M.Babu alisisitiza wapambane wakiwa ndani yachama na kwa njia kama hiyo ndio wangeliweza kuubadilisha mfumo wa chama hichokuwa bora zaidi. Ingawaje hatimae hata yeye nae, yaani Babu, alipungukiwa nasubra wakati Kamati Kuu ya ZNP alipokuwa akiteuwa wagombeaji uchaguzi wamwaka 1963. Katika kikao hicho Babu alisisitiza kwamba ili ZNP ionekane kwambani chama cha Kizanzibari kisichokuwa na ubaguzi wa aina yoyote ile na kwa vile ZNP ilikuwa ni chama chenye mchanganyiko wa watu wenye asili mbali mbali basi,ilibidi uwekwe mfano dhahiri kwa kila mtu kuona kwa macho yake mwenyewe. Kwahivyo katika mkutano huo Babu, kama ilivyotajwa hapo juu, akapendekezaAbdulrazak Mussa Simai, msemaji mashuhuri katika mikutano ya hadhara ya Hizbuambae alikuwa hana asili ya kiarabu, awe mtetezi wa jimbo la uchaguzi la Malindi.Hili lingekuwa pigo kubwa kwa siasa ya Mngereza ya kutaka kugawa watu kwamafungu ya kikabila na ingelikuwa ushindi mkubwa kwa siasa ya ZNP ya kukomesha ukabila na kuweka Wazanzibari w-ote sawa. Mrengo wa kulia waHalmashauri Kuu ya ZNP ikapinga pendekezo hilo na hapo ndipo maji yalipomwagika na kina Babu, Abdulrazak Mussa Simai, Muhsin Abeid, AbdulazizAli, Miraji Mpatani, Ali Sultani, Amar Salim Kuku, Ahmed Badawi Qulllatein, Salim Ahmed Salim, Dr. Ahmed Rashid, Tahir Adnan na wengineo kutoka chama nakuunda Umma Party iliyokuwa na siasa ya Wazanzibari wote kuwa sawa. Dr. Idarus Baalawi na Maulid Mshangama walikuwa ni viongozi wawili wa ZNP waliyokuwawakitia na kutoa kujiunga na Umma Party na kwa kweli mkutano wa mwanzo wawaandishi wa magazeti wa Umma Party ulifanywa katika nyumba ya MaulidiMshangama, huko Mbuyuni. ZNP ilisahau kusisitiza uendelezaji wa sura ya Zanzibar yakuwa nchi iliyokuwa na mchanganyiko wa damu, makabila, mila, jamiina utamaduni tofauti, nchi yenye rangi kama za tausi, tofauti ya rangi zake zikiwandio sifa na pambo lake.

Vugu vugu jipya la Upinzani

Chama cha Umma Party kilikuwa hakina kasumba za ugozi au ukabila, lengo lake lilikuwa kuwakombowa Wazanzibari kisiasa, kiuchumi, kijamii na kitamaduni. Lengola Umma Party halikuwa kuimba wimbo wa kupigania uhuru tu bali ilileta mfumo mpya wa kisiasa ambao uliwavutia Wazanzibari tofauti kutoka matabaka tofauti.Umma Party ilipendeza kwa Wazanzibari kwa sababu haikuwa tu inadai uhuru bali ilikuwa imeshatayarisha program/sera iliyohitajika ya kufanya maisha ya Mzanzibari bora. Ilikwisha tayarisha jinsi ya haki za mfanyakazi zilindwe, kuhakikisha kwamba mtuanapata kipato kwa mujib wa mahitaji yake, yaani yule mwenye ukoo mkubwaalikuwa apatiwe kipato cha kutosheleza ukoo wake wote. Kuwahakikishia wafanyakazi kazi bora, sheria za kuwalinda na kuwaepusha na ukosaji kazi.Kuwahakikishia wafanya kazi mapumziko ya likizo marefu na malipo yake yakutosha. Kuwahakikishia malipo ya kujitizama wakikosa kazi. Kuwajengea makaazibora na ya siha njema ili wawe watu wenye siha nzuri za kuweza kuitumikia jamii yao vyema. Wakulima walikuwa wahakikishiwe uuzaji wa bidhaa zao kwa bei muwafaka na kupatiwa misaada wanayohitaji katika jukumu lao la uzalishaji mali bora. Walikuwa wapewe vifaa vya lazima vilivyoendelea, kupewa mikopo ya kuendeleza kilimo bora,kusaidiwa kwa ujuzi wa kisasa na kujengwa kwa sehemu za mashamba ili kuwezakujitegemea na kuwekewa Benki ya maendelo ya ukulima na uvuvi. Mashambakuweza kuwa na huduma zote zilizopatikana mjini bila ya haja ya kusafiri safiri.Kuwahaki kishia watu wa mashamba umeme, maji safi ya mfereji, makaro, usafi namaskuli ya madarasa ya juu yaliyokuwa na sifa sawa na mijini. Kuwajengea watuwa mashamba vituo vya siha vilivyoweza kuhudumia magonjwa yote ya kawaida namagonjwa makubwa sana tu kupelekwa Spitali Kuu. Ujenzi wa mashamba ulikuwauwe na vituo mbali mbali ambavyo vitu vyote vilikuwa viweze kupatikana katika"centa" maalumm bila ya kulazimika kwenda mijini. Kulipangwa ujenzi wa viwandambali mbali katika sehemu hizo za mashamba. Wavuvi walipangiwa uvuvi bora wakutumia vifaa, mitambo na vyombo bora. Kuhakikishiwa usalama wao wakiwabaharini kwa kuweza kuwasiliana na vyombo vya dola kama wangelipata matatizo.Walikuwa wahakikishiwe vyumba vya barafu vya samaki wao na kuhakikishiwaviwanda vidogo vidogo vya kutia samaki katika vibati. Wavuvi kwa vile wengi waoni watu wa mashamba wangelipata huduma kama zile wakulima waliyozipata kwa vilewote wakiishi katika mazingara ya aina moja. Maisha ya Wanawake yalikuwa yaendelezwe kwa kila fani, sehemu za wazazi maspitalini zilikuwa ziendelezwe ili kumtukuza mzazi na kumfanya ajivunie kuzaana kutambuwa kwamba kuzaa kwake kulikuwa ni kutekeleza wajib mtukufu katikajamii. Wazazi walikuwa wapewe mapumziko maalum baada ya uzazi, wale waliyofanyakazi kuhakikishiwa mishahara yao kamili kwa muda wa kutosha na wale waliyokuwawakifanya kazi za kutunza ukoo kuhakikishiwa kipato sawa na mahitaji yao. Siha za watoto wao zilikuwa zitunzwe, kuangaliwa na kufuatilizwa tokea wakiwa wachanga. Kuhakikishiwa kupata chakula bora, kuchanjwa, kupimwa kwa majira kuhakikishiwa malezi bora ikiwa kwa kusaidiwa mabibi zao waliyowaleya au kuwajengea sehemu maalum za kutunzwa wakati wazazi wao wakiwa wameshughulikana kazi. Ilipangwa kuwahakikishia mabibi kazi na majira bora ya kazi na kuwahakikishia kipato bora na haki sawa katika jamii. Elimu ya mabibi ilikuwaitiliwe mkazo mkubwa zaidi. Wazee wote waliyokuwa na jamaa au bila ya jamaa walikuwa wahakikishiwe maisha bora bila ya kupata taabu zozote. Walikuwa watizamwe katika vituo maalum vyawazee, pale ambapo pangelihitajika. Wagonjwa, wasiyojiweza na vilema walikuwa wapewe haki saha na wananchi wengine na walikuwa watizamwe na kutunzwa bila ya ubaguzi au dharau yoyote.Ilipangwa wapewe huduma zote za lazima bila malipo au mapendeleo yoyote,kuhakikishiwa elimu na siha bora wakiwa chini ya uangalizi wa watu waliyojifunzakazi hizo. Vijana walikuwa wahakikishiwe maisha bora majumbani mwao ambako wazee wao walikuwa wahakikishiwe maisha bora na jamii kwa jumla ilikuwa iwahakikishie kipato cha kutosha na kwa hivyo jamii kuweza kuwatizama vijana na kuwahakikisha maisha bora. Kama vijana wangelihakikishiwa maisha bora majumbani mwao wangeliweza kushiriki kikamilifu katika masomo tofauti ya kujiendeleza. Masomo ya aina mbali mbali ya kutosheleza matakwa ya kijana wa Kizanzibari yalikwishapangwa ambayo yalisisitiza umuhimu wa masomo mbali mbali kuambatanana mazingara yetu. Skuli za kawaida zilikuwa ziende sambamba na maskuli mbalimbali ya ufundi kwa madhumuni ya kutajirisha siasa+ na uchumi wa Zanzibar.Maskulini elimu ya kilimo ilikuwa itiliwe mkazo kuambatana na mazao tuliyokuwanayo na yale ambayo yangewezekana kupan dishwa baada ya uchunguzi nautaratibu makini na maaluum. Mfano mwengine maskuli hayo yangelifundisha zaidikuhusu bahari ya Zanzibar na hazina yake na kujuwa jinsi ya kuitumia, kuitunza na kuihifadhi bahari hiyo. Masomo kama haya na mengi mengineyo kama ya siha,uchumi, n.k. yalikuwa yaendelezwe tokea skuli za msingi na hatimae vijana kuwana uzoefu bora wa kuchaguwa na kujua walichotaka kufanya baadae katika maishayao yakiambatana na majingara ya nchi. Vijana walikuwa walindwe na uhuni nakuzurura ovyo na baadala yake walikuwa wapewe nafasi tofauti za kuwawezesha kutumikia jamii na kujifurahisha wenyewe kama vile katika riadha na michezo mbalimbali. Vijana ndio walitizamiwa hatimae kulijenga taifa la Kizanzibari na kwa hivyo mipaka ya kujiendeleza walikuwa wawe nayo wenyewe. Wazanzibari wote walipangiwa wawe na haki sawa sawa na haki hizo kulindwa nakuhifadhiwa na Mahkama huru, zenye msingi wa Katiba na Sheria halali. Wafanyakazi serikalini walikuwa na haki ya kufuata siasa yoyote waliyoitaka,lakini walipokuwa makazini mwao walikuwa wawe na wajib wa kuutumikia umma wa Kizanzibari bila ya kujali imani na vyama vyao. Na serikali yoyote ambayoingelitawala isingelitakiwa iwabadilishe wale wafanyakazi wa serikali ambao imanizao zisingeliambatana na siasa ya serikali. Wafanya kazi hao walikuwa wahakikishiwe ulinzi wa haki zao zote za kifanya kazi, kupewa haki zote zilizostahiki. Wale ambao wangelikosa kazi wangelifanyi wa mipango ya kulipwa hadi kupata kazi upya. Wazanzibari walikuwa wahakikishiwe kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa dolalao na kupewa uhuru wa kuchaguwa viongozi ambao wangeli wawakilisha katika Bunge halali na kuhifadhiwa haki zao zote za Kidemokrasia, kama vile uhuru wakusema, wa kusoma na kuandika, wa kujikusanya na wa kufanya mikutano,kugoma na kuuandamana, haki za kibinaadam kwa jumla n.k. Mipango iliwekwa kuhakikisha kwamba hakutakuwa na tofauti yoyote baina ya Pemba na Unguja.

Umma Party ilikataa kujishughulisha na siasa za kipuuzi za Ugozi na Ukabila kwa sababu ilikuwa na program maalum ya kuihifadhi na kuinusuru Zanzibar. Umma Party ilikuwa na mpango maalum wa Uchumi wa kuinusuru Zanzibar. Mpango wa uchumi huo ulikuwa ni usambazaji wa vituo tafauti katika sehemu maalum mbalimbali za Unguja na Pemba. Vituo hivyo vilikuwa viwe kama chem chem, kiini chahuduma tafauti, zenye michirizi ya kiuchumi, michirizi hiyo ilikuwa iizunguka chemchem hizo kutoka kila pembe. Michirizi hiyo ilikuwa iwe kama mishipa ya damu,ikiwa na sifa zote za kijamii zikinufaisha maisha ya mwananchi, kwa mfano mchirizi mmoja ungelikuwa unawakilisha tu seme ukulima au uvuvi. Kwanza mchirizi huu ungelijengwa kwa mujib ya uwezo na mazingara maalum ya sehemu inayohusika naungelipangiwa mipango ya hali ya juu kabisa kuambatana na uchunguzi wakisayansi ili kuwezesha kuzalisha mazao bora kabisa. Mchirizi huo ungelihakikishiwa usafiri bora kabisa na sio mabarabara mabovu yenye mashimo matupu, bara bara zilikuwa ziwe za kuweza kusafirishia bidhaa kwa haraka na kwa usalama. Bara bara hizo wakati huo huo zingelifaidisha maendeleo ya jumla yasehemu inayohusika na nchi nzima kwa jumla na kuwezesha uuzaji na usambazajiwa vifaa na bidhaa tofauti. Michirizi mingine ungelihusika na vitu kama vile ujenzi wa viwanda vidogo vidogo mbali mbali, ujenzi wa majumba bora, ujenzi wa maspitalina maskuli, usambazaji wa umeme, soko na vituo vya biashara, siha bora: vituobora vya siha, maji safi , makaro n.k. Upangaji makini wa mambo hayo ungelizaamakazi mbali mbali katika sehemu hizo na kukuza hali bora ya maisha ya wananchi sehemu zote. Vituo kama hivyo vingelisambazwa sehemu tafauti, kila kimojakujishughulisha na mambo maalum yaliyohitajika nchini na yaliyoambatana namazingara yao na vingeliingiliana kwa madhumuni ya kusaidiana na kushirikiana.Fedha za ujenzi huo zingelitokana na uchumi wa nchi kwa jumla, uchumi ambao hatimae ungelinufaika kutokana na maendeleo hayo. Kwa wakati huo uchumi wa Zanzibar ulikuwa umenona. Wananchi wa sehemu hizo mbali mbali wenyewe walitarajiwa kupatiwa ujuzi uliyohusika na hatimae wenyewe kuendesha miradi hiyotofauti ikipewa muongozo na marekibisho tu na Serikali Kuu. Siasa ya miaka ya mwanzo ya 1960 na kuendelea ilikuwa ni siasa iliyonuka mizoga ya kikabila na ugozi, tofauti kabisa na siasa ya leo, wakati ambapo Wazanzibari karibu wote wanapigania Uzanzibari na kukataa kumezwa na Bara. Ingawa leo wanaotumia siasa ya ukabila ni wachache na wasiyokuwa na maana, juu ya hivyo bado pana haja kubwa sana ya kukariri ubaguzi wa kikabila ili kufaham historia nasababu za kutumia njama hizo. Suala hili litakaririwa zaidi wakati tukio la Mapinduzi na siasa ya CCM zitakapochambuliwa. Umma Party ilibahatika kuwa na viongozi na wafuasi wengi waliyosoma, kushir- ikikatika kuijenga ZNP na kwa kupitia njia hiyo kuweza kukielewa chama h- icho vizurizaidi jambo lililokuwa na umuhimu mkubwa mno baadae. Baadae U- mma Party kwakupitia "United Front" iliweza kusaidia kurekibisha mfumo wa wale viongozi waASP waliyokuwa mrengo wa kushoto. Siasa ya Umma Party ilikuwa kuwapiganiawanyonge na ilibahatika kuwa na mizizi katika tabaka la wafanyakazi na wakulima vile vile, hali hii ilizidi kupata nguvu kwa kuungwa mkono na Umoja wa Wafanyakazi wa FPTU (Federation of Progressive Trade Unions) ambao ulikuaUmoja wenye msimamo madhubuti, imara na wa kimaendeleo. Kuungwa mkono kwaUmma Party na FPTU kulikuwa na umuhimu mkubwa sana kwa vile Umoja huuulikuwa umeshatia mizizi katika umma wa wafanyakazi na wakulima na Umoja ambao ulikuwa unaaminika na kuwa na maingiliano mazuri na ZPFL (Zanzibar and Pemba Federation of Labour) Umoja wa Wafanyakazi uliyofanyakazi pamoja na ASP. Maingiliano haya hatimae yakazalisha Zanzibar Revolutionary Trade Unions. Kwa muda mfupi wa maisha ya Umma Party, kabla ya chama hicho kupigwa marufuku nana serikali ya ZNP, kiliweza kuunganisha wanasiasa na vijana wote wa mrengo wakati na wa kushoto. Wakati wa kuundwa Chama cha Umma nyoyo za watu wengizilifurahika na kuwa na tamaa kubwa ya chama hicho kuleta mabadiliko yakimaendeleo Zanzibar. Pindi ingelikuwa chama hicho hakikufungiwa na Hizbu miezisita tu baada ya kuundwa, basi Zanzibar leo ingelikuwa inajitawala wenyewe, ikiwana wataalam wake wote na utajiri wake wote mikononi mwake wenyewe kwa manufaaya kila Mzanzibari. Na maingiliano ye- tu na Tanganyika yangelikuwa ya kidugubaina ya nchi mbili huru zinazohishimiana, kutukuzana na kusaidiana kimaendeleo,na sio kutawaliana. Siasa ya chama cha Umma ilipendeza kwa haraka sana hasa katika jamii ya vijana na baina ya watu wa matabaka ya chini wa vyama vyote viwili vikubwa. Lengomojawapo muhimu ilikuwa ni kujaribu kuleta masikilizano mema hasa na mrengo wakushoto wa ASP na haikuchukuwa muda mrefu vyama vyote hivi viwili vikubwavikaanza kuingiwa na wasi wasi walipoona vijana na wafanya kazi wa sehemu zotembili wakikaribiana katika mfumo mpya wa uhuru na umoja. Kushirikiana huku na ASP, vyama vya wafanya kazi na vyama vya waandishi magazeti na wengineo vilileta imani na muamko mpya visiwani. Hapo pakaundwa United Front "muunganisho wa vyama na fikra tofauti " na muelekeo wa mapambano ukaanza kutia sura mpya. Huu ni wakati mmoja wapo muhimu sana katika historia yaZanzibar kwa ni kipindi hichi cha muda wa miezi sita, kutoka Juni, 1963 hadiJanuari 64, nchi nzima ulipambwa na jazba za kinajananchi zilizofanya damu zawana nchi kuchemka na kuwa na matumainio ya hali ya juu kabisa. Jambo muhimu lililofanya hamasa za kijananchi wa Kizanzibari ilikuwa ni uundaji wa Umma Party,kwani baada ya kuundwa chama hicho, mfumo wa upinzani ulichukuwa sura mpyakabisa. Hali hii ya kujitolea ilitokana na program ya Umma Party katika kuipangiaZanzibar mikakati ya kimapambano ya siku za usoni. Kuunganisha kwa vikosi mbalimbali vya utayarishaji mabadiliko yakuleta neema nchini uliwafanya viongozi mbalimbali wa vyama vilivyounga mkono ASP, kungana kwa dhati na Umma Party katikakuijenga Zanzibar mpya. ASP kwa wakati huo ilikwisha shindwa katika uchaguziwa 1963 na viongozi wake waliparaganyika na kutokuwa na msimao madhubuti, nakutokuwa na siasa na sera mkakati ya kupambana na serikali ya Hizbu. Kwa hivyokuchomoza kwa chama cha Umma Party na kuchukuwa dhamana ya kujengaupinzani mpya kwa kuunga nisha waandishi wa upinzani, vyama vya wafanyakazina wakulima, vijana na wanawake na viongozi "militant" wa ASP na Umma Party,ulifanya muamko wa Zanzibar kupata hamasa mpya. Wadhifa wa mwanzo wa umojahuu mpya ulikuwa kukuza elimu ya kisiasa na kupanga mbinu za kupambana,kuweka misingi mipya ya kufanya kazi za kichama na aina mpya ya mfumo wamapambano. Hali hii iliwezekana kutokana na ukakamavu na uzoefu wa mipango yakisiasa wa uongozi na wafuasi wa Umma Party. Upinzani mpya ukazalika na tamaaya kujikombowa ikazidi kutia nuru.

Serikali ya taifa

Muda ulikuwa mfupi kwa chama cha Umma kuweza kushiriki katika kampeni za kujiandaa kichama, kwa hivyo chama hicho hakikupata wakati wa kukuwa nakujisambaza zaidi. Nguvu za wana Umma hao zilikwishatumika kujenga siasa ya msingi ya kupigania uhuru. Umma kwa sababu hizo iliamuwa kutoshiriki katika uchaguzi wa 1963 na badala yake ilijipalilia kutowa elimu ya siasa ya kimsingi katika jukumu la kujaribu kuwaleta Wazanzibari wote pamoja. Kwa mara ya mwanzo tokea kuanza kwa siasa za kupigania uhuru palikuwa na tamaa ya Wazanzibari wote kuungana, hasa katika mambo fulani ya kimsingi. Wakati huo muungano wa ZNP na ZPPP ndio uliyokuwa ukiendesha serikali ya ndani na kufuatia uchaguzi wa 1963 vyama viwili hivyo vikaishinda ASP na kuendelea kuende-sha serikali peke yao, hadi kupatikana kwa uhuru Disemba 10, ingawa ASP ilipendekeza kuundwa kwa serikali ya kitaifa yaani ASP nayo kuwemo serikalini. ASP ilivunjika moyo sana kwa kutoshirikishwa katika uongozi wa nchi hasa kwa vile uhuru ulipiganiwa na vyama vyote, na mada ya uongozi wa nchi ni wadhifa wawananchi wote kwa jumla, bila kujali ufuasi wa chama fulani. Pindi pangelikuwa na serikali ya Kitaifa basi Zanzibar leo ingelikuwa nyengine na kuweza kupiga khatuwa kubwa sana, kwani kusingelikuwa na Muungano na nchi ingelitononeka. Katika serikali hiyo ya 1963, ni ZNP kwa kweli ndiyo hasa iliyokuwa ikiendesha serikali na Mohammed Shamte alikuwa kawekwa kama kilemba tu. Serikali ya ZNP, badala ya kujishughulisha na uongozi wa taifa kwa njia ya kiusawa na kihalali, kwa kweli ilishughulishwa zaidi na kuipiga vita Umma Party hata kuvisahau vyama vya ASP na ZPPP. Ilifanya hivyo kwa sababu ilihisi kwamba Umma Party ilikuwa na uwezo na ujuzi wa kuweza kupambana na ZNP na hatimae kuweza hata kuwachukuwa wafuasi wa ZNP, hasa kwa vile ni makada wa Umma ndio waliyoijenga ZNP na wakizijuwa mbinu na mipango yote. Kwa vile ZNP ilitambua ukweli huo. Chini kwa chini, kwa siri kabisa, ikaanza kupika majungu ya siri kwa kugawa silaha baina ya wafuasi wake chini ya uongozi wa wale vijana waliyofunzwa mambo ya kijeshi huko Misri, kati ya vijana hao walikuwemo baadhiya wana ZNP wa mwanzo waliyofariki katika mapinduzi ya 1964. Silaha hizo hazikutolewa kwa maksudi ya kupigia paredi. Moja kati ya njama zilizopangwa naserikali ya Hizbu ilikuwa ni kumkamata Babu, pamoja na viongozi fulani wa ASP, lakini Babu alizipata fununu hizo na kutoroka Unguja na kwenda Dar es salaam. Ilidhihirishwa baadae kwamba kulikuwa na listi ya watu 120 serikali hiyo ya ZNP alitaka kuwatia mbaroni, listi hiyo ilikamatwa baada ya Mapinduzi. Baada ya uhuru serikali hiyo ikapitisha sheria za kikandamizaji ambazo hata mkoloni Mngereza hakuzipitisha wakati wa ukoloni, nazo sheria hizo zilikuwa kinyume na dhidi ya haki za kibinaadam na demokrasia kwa jumla. Hapo ndipo haki na uhuru wa kutoa maoni kuanza kukandamizwa, uhuru wa kukutana na kuchapisha ukanyimwa, uhuru wa mtu kujiunga na chama atakacho ukaingiliwa kati, uhuru wa kusafiri ukapunguzwa na uhuru wa mahkama huru ukaingiliwa katikwa kuwa na kupalilia sheria ya kumweka watu vizuizini. Hatua zote hizi za kuvunja haki za kibinaadam zilikuwa zimepangiwa Umma Party, chama ambacho kilipigwa marufuku, kama ilivyotajwa hapo juu. Gazeti lake la Sauti ya Umma na ZANEWS kufungiwa na kupanga mipango ya kuwakamata viongozi wote wa Umma pamoja na viongozi wengine wa Upinzani, yaani wa ASP, FPTU na ZPFL. Mipango hii ndio kwa upande mmoja iliyosababisha na kuharakisha kufanyika kwa Mapinduzi(Hizbu wasimlaumu mtu kuhusu Mapinduzi kwani wame yapaliliya wenyewe). Hatuwa hizi za kikandamizaji zilizidi kuwaleta pamoja viongozi wa Umma na wamrengo wa kushoto wa ASP pamoja na vyama vyao vya wafanyakazi na waandishiwa magazeti pamoja na vijana. Kwa upande mwengine kuungana kwa Umma na mrengo wa kushoto wa ASP ambao ulikuwa na karibu wataalam wote wa ASP na wakati huo huo wakiwa ni Wazanzibari asilia, ulileta mgogoro katika uongozi wa ASP. Uongozi wa ASP nao ulikuwa na migogoro yake wenyewe hata kabla ya kuundwa kwa Umma Party. Itakumbukwa huko nyuma, kwamba tokea kuundwa kwa ASP katika mwaka 1957 kulikuwa na matatizo baina ya Washirazi na wale waliyokuwa na asili ya Bara na hapo ikabidi Nyerere aingie kati na kufudikiza fudikiza. Matatizo hayo hayakutatuka nahatimae kina Shamte wakaunda chama chao baada yakiongozi mmoja mashuhuri wa Shirazi Association, Sh. Ameir Tajo, kuadhiriwa katika mkutano wa hadhara wa ASP na kufukuzwa chama. Ingawaje mgogoro huu baina ya wenye asili ya kibara na ya Kizanzibari haukumalizika hapo kama tutavyoona huko mbele. Mvutano mwengine ulitokana na waliyosoma na wasiyosoma, mfano huu ulikuwa zaidi baina ya Karume, Othman Sharif na Abdulla Kassim Hanga. Waasis wa ASP waliyotoka tokea African Association walijiona kuwa na haki zaidi ya uongozi wa ASP. ASP ilikuwa na Umoja wa vijana wa aina mbili mmoja ukiwa wa YASU, yaani Young African Social Union, Umoja ambao ulijitambulisha kama chama cha "kijamii na kitamaduni" lakini kwa kweli kilikuwa chama cha vijana wa Kiafrika wenye muelekeo wao wenyewe nyeti wa kisiasa. Wanachama wake wote walikuwa ni waliyosoma na wazalia wa Kizanzibari. Kiongozwao alikuwa Othman Sharif, lakini Aboud Jumbe, Hasnu Makame na Mdungi Usi nikati ya waliyoshiriki katika Uongozi wa vijana hao. Chama hichi hakikujitambulisha wazi kuwa ni chama cha vijana wa ASP ingawa wote wao ama walikuwa ni wafuasi au waunga mkono wa Chama hicho. Sh. Ameir Tajo ndiye aliyowapatia msaada wakujenga jumba lao la YASU, huko Miembeni, baada ya Mapinduzi chama hicho kilipigwa marufuku, ingawa chama hicho kilikuwa kikitowa huduma kwa watoto wakiswahili ambao wengi leo wana elimu ya juu kabisa. Chama hasa cha vijana wa ASP kilijulikana kama Afro shirazi Youth League, ASYL. Viongozi wa chama hichi walikuwa ni wale waliyokosa elimu na wengi wao wakiwa na asili ya bara, ingawaje wafuasi wa chama hichi hawakuwa vijana wa kweli kama vile vijana wa YASU bali walikuwa ni watu wazima karibu wote wakiwa watabaka la chini kabisa, malumpa, walala hoi wakiwa wengi wao wasiyokuwa wazalia wa Zanzibar. Hawa walimuunga mkono Karume kwa sababu yeye mwenyewe hakuwa msomi kama wao, akiwa mtu wa tabaka la chini, asiyekuwa mzalia wa Zanzibar bali alikuja Zanzibar akiwa ni mtoto. Na Karume nae kwa upande wake akiwaamini ASYL kwa sababu hizo hizo, na siasa yao ilikuwa ni kutumia ugozi bila ya kuwa na mfumo, muelekeo au sera zozote maalum za kisiasa za kuinusuru Zainzibar. Zaidi ya mgawanyo huo, kulikuwa na chama cha wafanya kazi cha ZPFL ambacho ingawa kilikuwa na baadhi ya wazalia wa Bara katika uongozi wake, kilikuwa na mfumo afad hali wa kimaendeleo ukifananisha na mfumo wa ubaraka , ingawa viongozi wachache wa chama hichi ndio waliowauza kina Twala na Hanga. Kwa hivyo ndani ya uongozi wa ASP kulikuwa na migawanyo ya migongano ambayo imeathiri sana hali bora ya Visiwa vyetu.

Malumpa wa Zanzibar

Malumpa, "walalahoi" au watu walio tabaka la chini kabisa la jamii ni kwa desturi ni watu wenye malalamiko mengi zaidi katika jamii za kila aina. Tabaka hili, siku zote liko tayari kushiriki katika kuleta mabadiliko ya kijamii kwa sababu kama inavyosemekana ni tabaka ambalo katika mapambano ya ana kwa ana, halijali, kutoogopa wala kuwa na wasi wasi, kwa sababu huwa hawaogopi kupoteza maslahi yoyote , kwani wakipotezacho si zaidi bali ni minyororo yao ya kisiasa na kiuchumi . Hili kwa desturi ni tabaka linyonywalo zaidi, linalokandamizwa kuliko tabaka lolote na linaloteseka kikomo cha juu kabisa ukifananisha na matabaka mengine ya jamii. Tabaka hili likipata uongozi mzuri ndilo tabaka linaloleta mabadiliko ya kuendeleza maisha bora ya kila mwananchi. Ingawaje tabaka hili likikosa viongozia u uongozi bora linaweza kuleta athari kubwa mno katika jamii. Zanzibar karne za karibuni imekuwa ni nchi iliyofaidika na kunufaika kiuchumi.Watu wake walikuwa na kipato cha kutosha na kuwafanya kutokubali kutumwa. Kwa kawaida ijapokua Mzanzibari asilia alikuwa hali ya chini, aliweza kuwa na kipato cha kutosha cha kujiepusha kuingia katika tabaka la "ulumpa". Siku za uvunaji karafuu ilieleweka kwamba idadi ya Wazanzibari wote kwa jumla ilikuwa ndogo zaidi kushinda ile iliyohitajika katika vuno la karafuu, kwa hivyo Zanzibar ilibidi kuagiza wafanyakazi wa majira kutoka Bara la Afrika ya Mashariki na Kati, wengi wao kutoka Mrima/Tanganyika. Jambo lililowavutia majirani hawakuja kufanya kazi Zanzibar ilikuwa ni utajiri Zanzibar uliyokuwa nao kwa wakati huo, na kuweza kulipa mishahara mikubwa zaidi kuliko nchi jirani na wakati huo huo watu hao walikua hawatozwi kodi ya kichwa Zanzibar tofauti na kule walikotoka. Kwa mfano mishahara ya vibarua wa Zanzibar katika miaka 1930 nakuendelea ilikuwa ni sh. 30/ kwa mwezi, wakati mishahara ya kibarua au skwatawa Kenya haukufikia hata sh. 15/ seuze ile ya Tanganyika ambayo ilikuwa chini zaidi. Mishahara ikaendelea kupanda hadi 1948 wakati kibarua akipata sh. 3/30 kwa siku. Kutokana na kuagiza vibarua kutoka nchi za jirani idadi ya wakaaazi wa Zanzibar ilikuwa kama ifuatavyo: Kutokea mwaka 1923 hadi 1931 wafanyakazi wote waliyoingia Zanzibar walikuwa 21,852 na waliyoondoka katika muda huo huo 14,055, katika miaka ya 1927 na 1928 jeduweli za wahamiaji hazikuchapishwa. Baada ya hapo inakisiwa kwamba kiasi chawatu 2000 waliingia Zanzibar kwa mwaka, wengine wengi waliingia kwa magendo bila ya kujulikana na kuhisabiwa. Sensa zifuatazo zinaonyesha idadi ya wabara waliyokuwa Zanzibar. Katika mwaka 1924 kulikuwa na Wabara 64,828 Wazanzibari wenyewe wakiwa 119,360 (yaani Wabara kuwa z aidi ya thuluthi moja ya wakaazi wa Zanzibar ) sensa ya mwaka 1931 ilionyesha idadi ya kiasi cha Wabara 74,492 wakati sensa ya mwaka 1948 ilionyesha Wabara waliyoishi Unguja na Pemba kuwa watu 51,227 wakati Wazanzibari wenyewe wakiwa 148,480 yaani zaidi ya robo ya wakaazi wote kwa jumla na zaidi ya thuluthi moja ya Wazanzibari wote. Baada ya mgomo wa Wafanya kazi wa 1948 wahamiaji kutoka Bara hawakuwa wakija kwa wingi hasa kwa vile hata mishahara ilikuwa imepunguwa.

Mgomo wa 1948

Mgomo huo uliyotajwa hapo juu wa agosti-septemba 1948 ulikuwa ni wa wafanya kazi wa chini kabisa hasa wale wa bandarini, makuli, wachukuzi, vibarua, wafanyakazi wa P.W.D, hospitali na kadhalika. Kwa vile Zanzibar ikiagiza vibarua kutoka mabara, mgomo huu ulikuwa umefanywa zaidi na Wabara kwani wao ndio waliyokuwa sehemu kubwa kabisa ya tabaka hilo. Mgomo huo ulishajiishwa zaidi na mgomo wa Mombasa wa 1939 na wa Dar es salaam wa 1947. Kutokana na mgomo huo ukakamavu na msimamo imara wa wafanyakazi ukajichomoza na hatimae wengi wao walipokosa au kuachishwa kazi, wakaingizwa katika tabaka jipya, na kupata sura mpya ya kilumpa, maprolitari wasokuwa na kazi. Wagomaji hao, ingawaje walipokuwa wakigoma, waliungwa mkono na jamii nzima ya Kizanzibari katika madai yao halali na kupata misaada tofauti na hata mashamba, waliwaletea vyakula, na watu wengine wa jamii kama vile Watumbatu kukataa kuvunja mgomo huo kwa kufanya kazi baadala ya wagomaji hao, na akina mama wa Kizanzibari kuwapikia vyakula wagomaji hao. Malumpa hawa wakiwa wengi wao ni Wabara, kutokana na mgomo huu wakaanzisha kikundi kilichokuwa na upungufu wa mfumo, upungufu wa siasa, sera au mipango maalum, lakini watu hawa walikuwa ni watu wenye maslahi ya aina moja na waliyokuwa hawana uongozi madhubuti. Lengo lao kubwa lilikuwa si la kitaifa bali la kuongezewa mshahara tu, bila ya kuwa na mfumo wa kisiasa ya kitaifa. Baadae vyama vya wafanyakazi vilipoanzishwa watu hawa wakawa katika mstari wa mbele na washabiki wakubwa. Kutokana na hali ya tabaka lao la hali ya kuonewa kwa kunyonywa na kudhulumiwa, walipata maarifa na elimu fulani ya kisiasa kutoka katika mgomo huo. Na kama desturi, malumpa ni watu waliyokuwa tayari kuchukuwa khatuwa za kimapinduzi wakati wowote, ingawaje wakipata uongozi mbaya matokeo yake huwani balaa kubwa mno.

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Postagem Anterior Próxima Postagem